Jumatatu, 04 Sha'aban 1446 | 2025/02/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  5 Rajab 1446 Na: Na: HTS 1446 / 41
M.  Jumapili, 05 Januari 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Khilafah: Mradi wa Mabadiliko wa Ummah na Taji la Faradhi zote
(Imetafsiriwa)

Chini ya mada hii, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ilifanya kikao chake cha kawaida, Kikao cha Masuala ya Umma, ambacho mwezi huu, mwezi wa Rajab, kilifanyika kukumbuka kumbukumbu ya kuvunjwa kwa Khilafah, inayofikisha miaka 104 tangu kuanguka kwake katika mwezi wa Rajab 1342 H.

Nyaraka mbili ziliwasilishwa kwenye kikao hicho. Waraka wa kwanza uliwasilishwa na Ustadh Hatim Jaafar, wakili na mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, wenye kichwa “Khilafah: Mradi wa Ummah wa Mabadiliko.” Alijadili nukta kuu tatu: asili na hadhi ya Khilafah, masharti ya Kongamano la Lausanne mnamo tarehe 22 Disemba 1922, sherehe za Bunge la House of Commons la Uingereza za kuvunjwa kwake, na kauli ya George Curzon, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza. Nukta ya pili ilizungumzia fahamu ya Ummah katika lugha na Shariah ya Kiislamu. Nukta ya tatu ilijadili mabadiliko, ikisisitiza kwamba Ummah ni mmoja na wenye nguvu kama mwili mmoja, ikiyafanya Mapinduzi ya Kiarabu kuwa maregeleo. Alisema kwamba ikiwa watu wangejibu maswali mawili muhimu: Sisi ni nani? Ni maradhi gani tunayougua, na yalianza lini? Wangefikia malengo yao, huku Khilafah ikiwa ndio mradi wa mabadiliko.

Mada ya pili iliwasilishwa na mwanachama wa Hizb Ustadh Yaqub Ibrahim, yenye kichwa “Khilafah: Taji la Faradhi zote.” Alieleza hadhi ya Khilafah na ufaradhi wake kwa dalili kutoka katika Quran, Sunnah, Ijmaa’ Sahabah (Makubaliano ya Maswahaba), na kanuni za kisheria za Kiislamu. Alitaja kauli za wanazuoni wanaoheshimika kuhusiana na hadhi na ufaradhi wa Khilafah na akazungumzia hofu ya viongozi wa dunia miongoni mwa makafiri kuhusu kuregea kwake.

Mwendesha kikao hicho, wakili Ustadh Muhammad Abdel Fattah kisha akafungua ukumbi kwa maswali na maoni. Michango mashuhuri ilijumuisha ushiriki kutoka kwa Ustadh Asim Al-Bilal, Naibu Mhariri Mkuu wa Gazeti la Akhbar Al-Youm. Jukwaa la kikao kisha lilijibu maswali na maoni.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu