Jumatano, 08 Rajab 1446 | 2025/01/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  26 Shawwal 1441 Na: 1441/55
M.  Jumatano, 17 Juni 2020

Tanzia kwa Mbebaji Ulinganizi

 [ولَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ]

“ Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri”
(Imetafsiriwa)

Kwa macho na nyoyo zilizojawa na machozi zilizo ridhia qadhaa ya Mwenyezi Mungu, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan inaomboleza msamaha kwa Sheikh (kwa idhini ya Mwenyezi Mungu):

Mohammed Al-Sayir Omar

Ambaye alitumia ujana wake katika kulingania kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume na kufanya kazi maisha yake yote ili kunyanyua bendera ya la ilaha illa Allah Mohammed Rasulullah (saw) (Hakuna Mola Apasaye Kuabudiwa kwa Haki Isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)) kwa subira, akipitia madhara aliyo yapata akiwa katika magereza ya madhalimu na vituo vyao vya uzuizi ili kuunga mkono haki bila ya kuchoka wala kuchoshwa hadi akatimiza muda maalum hapa ulimwenguni jana asubuhi, Jumanne, 25 Shawwal 1441 H sawia na 16/6/2020.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amrehemu na kumsamehe na kumweka katika mabustani yake mapana ya Pepo pamoja na mitume, waumini na mashahidi na watu wema kwani hakika hao ndio marafiki wazuri, na kutupa sisi na familia yake subira na faraja njema. Wanaume hufa lakini matendo yao mema hubakia na kuzungumzia utukufu wa vyeo vyao katika hali tofauti tofauti.

 [إنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea”

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb it Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu