Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  7 Jumada I 1441 Na: 1441 / 06
M.  Alhamisi, 02 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 Wacha Ummah Usimame dhidi ya Taasisi hizi Ovu na Uzuie Mipango Yake

(Imetafsiriwa)

Kundi la mashirika linadhamiria kufanya mandamano saa sita mchana, Alhamisi 02/01/2020, kudai kutiwa saini kwa Makubaliano ya Kuondoa Aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW), na kusema kwamba maandamano hayo yatakutana na Waziri Mkuu na Waziri wa Sheria kukabidhi ujumbe huo, na kutangaza kuwa mashirika yote yaliyoshiriki katika maandamano hayo yanajumuisha “The Strategic Initiative for Women in the Horn of Africa,” The Initiative of No to the Oppression of Women, the Women's Union, vile vile kamati za upinzani na mkusanyiko wa Kendakat kusini mwa Khartoum. (Gazeti la At-Tayyar)

Kitengo cha Wanawake katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan kingependa kuweka wazi ukweli ufuatao:

Kwanza: Jamii za kutetea haki za wanawake zinazodai makubaliano ya CEDAW zinajiwakilisha zenyewe peke yake kwa sababu matakwa ya kufanyiwa kazi makubaliano haya yaonyesha utiifu na kumuiga Kafiri Mmagharibi anaye pinga Uislamu kwa kutuhumu vifungu vyake vya kubagua wanawake. Kwa hivyo, waliandaa masharti ya makubaliano haya kulenga mwanamke wa Kiislamu kuwazuia wanawake wa Kiislamu kushikamana na vifungu vya sheria kwa kulingania kwa uwezo wa mwanawake kudhihirisha miili yao na kukomesha usimamizi wa kisheria wa wanaume juu yao katika kulenga wazi familia ya Kiislamu, kuhamasisha wanawake wa Kiislamu dhidi ya vifungu vya Uislamu, na kufanya kazi kutunga sheria ambazo zitaasi vifungu vya Shari’ah ya Kiislamu, kwa kuepukana na maadili mema ili maisha yake yaendane kulingana na mtazamo huria wa Kimagharibi, na ushawishi wa mara kwa mara kutetea kile kiitwacho uhuru, wakati wakionyesha mara kwa mara kuwa mabustani ya starehe yako katika mwenendo wa maisha ya Kafiri Mmagharibi, na kuwa kubaki nyuma ni kubaki chini ya kanuni za sheria ambazo zinazuia uhuru wa mtu binafsi!

Pili: Jamii hizi za watuhumiwa wa utetezi wa haki za wanawake zinasaidia njia za kupotosha wanawake, na kuanguka kwao katika dimbwi la uozo na ufisadi kwa kuwaelimisha wao thaqafa na fahamu za Kimagharibi kwa miito yenye kuvutia! Kama vile kudai kuunga mkono wanawake, kuwajulisha wao haki zao, kuwasaidia wao kujithibitisha, na kuimarisha utambulisho wao ili kuboresha jukumu lao katika maisha! Wakati ukweli ni kwamba wanamtaka mwanamke kuwa picha potofu ya wanawake wa Kimagharibi kupitia miito yenye kuvutia kwa umaarufu wa kirongo, ili aanguke kwenye shida za kila wakati.

Tatu: Shughuli za vyama hivi zimeongezeka, wanaposambaza sumu zao kwa madai ya kurekebisha wanawake wa kijijini, kueneza ufahamu wa afya ya uzazi, na utumiaji wa kondomu kwa kisingizio cha kupambana na UKIMWI, pamoja na kueneza thaqafa ya kijinsia, kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi yao, na kauli mbiu nyingine zinazoonekana kupendeza juu ya uso. Kazi ya vyama hivi imesababisha wanawake wajinga kuasi dhidi ya maadili ya Uislamu, familia, baba, na desturi jumla zilizoshawishiwa na Uislamu, na kupelekea kuenea kwa uovu, ukahaba, talaka, ujane, na shida nyingine ambazo zinawaathiri wanawake kimsingi.

Watu wa Sudan lazima wawe waangalifu na jamii hizi za kutetea haki za wanawake, ambazo hazihitaji kuzitambua kuwa ni bidhaa za Wamagharibi, ikiwa ni suala la imani ambayo wameitegemea (usekula), au nidhamu ambayo wanaifuata, ambayo ni nidhamu ya kirasilimali, ambayo imejifunga na uhuru. Hii inadhihiri katika mipango wanayoitekeleza, na masuala wanayoyazua, na vyanzo vyao vya Kimagharibi vya kufadhili uhadaifu na wauaji wa siri. Kitabu, Spotlight on the Sudanese Feminist Movement, kilieleza msaada huu katika taarifa ya Ubalozi wa Amerika, ambapo Ubalozi huo ulitangaza msaada wa kila mwezi wa dolari 35,000 kwa moja ya miungano ya wanawake inayoongoza nchini Sudan, vile vile mradi wa "Kuondoa tabia zenye kudhuru afya ya familia" uliopitishwa na muungano wa Babiker Badri Scientific Association for Feminist Studies unafadhiliwa na American Public Welfare Association.

Miungano hii ya utetezi wa haki za wanawake lazima ienue mikono yao kutoka katika heshima yetu, kwani tunaamini kabisa kuwa tuna jukumu kubwa katika maisha haya. Mwanamke katika Uislamu ni mama, mke, na heshima ambayo lazima ihifadhiwe. Na hakika Uislamu hauzingatii mama, dada, binti, na mke kama watumwa kwa wanaume kama ilivyo katika miungano hii inayotokamana na Wamagharibi. Badala yake, unaelezea wale ambao wanawaheshimu kwa ukarimu na wale wanaowadhalilisha kwa ubaya, na kuwalazimisha wanaume kuwatunza, kwa sababu Mtume (saw) amesema:

«وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلي أَهْلِ بَيْتِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»

“Na mwanamume ni mchunga wa familia yake na anataulizwa juu ya uchungaji huo.” Na kuzingatia kifo kwa ajili ya kumlinda mwanamke na kumhifadhi kama Shahadah (shahidi) kwa maneno ya Mtume (saw):

«وَمَنْ قُتِلَ دُونَ أَهْلِهِ فَهُوَ شَهِيدٌ»

“Na yule anayeuwawa wakati akitetea familia yake ni shahidi.”

Enyi Waislamu:

Simameni dhidi ya taasisi hizi ovu, na kuzuia mipango yao kwa kuwazuia wanawake na binti zenu kutokamana na kuzuru miungano hii, na kuhudhuria amali na matukio mabaya ya kuangamiza. Wacha sisi tuwaimarishe kwa thaqafa tukufu ya Kiislamu, na fahamu za busara za Kiislamu, haswa vifungu vya sheria vinavyohusiana na wanawake katika haki na majukumu yao, na jukumu lao muhimu katika maisha. Wacha wanaume na wanawake wote wafanye kazi pamoja na wanaofanyakazi ya kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili ya uongofu kwa njia ya Utume, ambayo itawalinda wanawake, familia, jamii, na kwa hakika wanadamu wote kutokamana na taasisi hizi, wafuasi wao, na wafadhili wao.

Msemaji Rasmi wa Kitengo cha Wanawake katika 

Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu