Afisi ya Habari
Wilayah Syria
H. 14 Sha'aban 1442 | Na: 012 / 1442 H |
M. Jumamosi, 27 Machi 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir / Wilayah Syria Yawasilisha Waraka Wake wa Tatu wa Kisiasa Pamoja na Kuingia kwa Kumbukumbu ya Miaka Kumi ya Mapinduzi ya Ash-Sham
(Imetafsiriwa)
Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Syria iliwasilisha waraka wake wa tatu wa kisiasa pamoja na ujio wa kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuvunjwa kwa Khilafah kwa mikononi ya mhalifu Mustafa Kamal, na kuingia kwa kumbukumbu ya miaka kumi tangu kuanza kwa Mapinduzi ya Ash-Sham chini ya kichwa: "Kusoma Uhalisia wa Mapinduzi; Uchunguzi na Tiba." Ikimuomba Mwenyezi Mungu (swt) uyafikie masikio yenye kusikia na akili zenye fahamu, baada ya Mapinduzi ya Ash-Sham kufikia hatua muhimu mno na nukta hatari ya mabadiliko, Hizb ilielezea njama ambazo Amerika imezisuka na kutekelezwa na dola zilizo chini ya mrengo wake na vibaraka wake, ambazo viongozi wa kikundi wamejisalimisha kwake na kufuata njia yake, na Hizb ikaelezea uhakika wa mzozo na mwendelezo wake na aina zake, na kubainisha ndani yake mbinu na njia zinazotumiwa kuyamaliza mapinduzi haya yatima.
Ndani yake, pia aliwasilisha usomaji wake juu ya uhalisia wa mapinduzi, na nini kilitokana na amali zilizofanywa na dola zilizo chini ya Amerika na dola vibaraka kwa suala la kuvunja mapinduzi, kugawanya watu wake, na kuwasambaza kwa mikoa minne; wakitofautiana kila mmoja katika umbo, lakini wakishabihiana katika kiwango cha yaliyomo na ufuataji wa kisiasa.
Na kuelezea sababu ambazo zilipelekea jamii ya kimataifa kutekeleza mbinu zote za uhalifu; Kuanzia kuzingirwa na vizuizi katika ngazi zote, chini ya kivuli cha uhalifu wa vikundi vya vikosi vya usalama, uporaji wa watengenezaji vivuko, ukiukaji wa heshima ya binadamu, kunyamazisha midomo ya walio huru, uhalalishaji wa wanasheria wa uhalifu wa viongozi, na watu kushughulika katika kwenda mbio kupata makaazi na kutafuta riziki, huku wakisubiri kikapu cha misaada nchini ambayo imegeuzwa kuwa kambi kubwa ambayo haiwakingi wakaazi wake na joto msimu wa kiangazi wala baridi ya msimu wa kipupwe.
Na ikabainisha ndani yake ni vifaa vipi ambazo ni lazima vipatikane ili kujilinda dhidi ya athari ya shambulizi hili kali la Amerika, na nini tunapaswa kufanya katika hatua hii muhimu, na ndani yake pia ilionyesha hatua za kivitendo ambazo lazima tuchukue kuleta mabadiliko tunayotaka katika mapinduzi haya na kuyarudisha katika mwelekeo wake sahihi, na ni madhara gani makubwa yanayotokana na juhudi kubwa zilizofanywa na Magharibi kuzivuruga akili za watoto wa Umma, na ni mambo gani ambayo hayana budi kwa watu wanapofanya mageuzi...
Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Syria ilihitimisha waraka wake wa tatu wa kisiasa kwa kusema: "Na sisi katika Hizb ut-Tahrir tunanyosha mkono wetu kwa watoto wa Umma wetu ambao wanaofanya mapinduzi katika Ash-Sham, na tunawaalika wafanye kazi nasi ili kuregesha uamuzi wa mapinduzi ulionyakuliwa, kuyaelekeza mwelekeo wake sahihi, na kuyaongoza moja kwa moja kuelekea kupindua serikali na kusimamisha Khilafah, ili tumridhishe Mola wetu na tuhifadhi haki zetu, na kurudisha utukufu wetu na kufanikisha maslahi yetu katika ulimwengu huu na Akhera.
[وَيُرِيدُ اللَّهُ أَنْ يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ * لِيُحِقَّ الْحَقَّ وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ]
"Na Mwenyezi Mungu anapenda ahakikishe Haki kwa maneno yake, na aikate mizizi ya makafiri * Ili ahakikishe Haki na auvunje upotovu na wangachukia wakosefu.” [Al-Anfal: 7-8]”
Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Syria |
Address & Website Tel: |