Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  20 Jumada I 1443 Na: 04 / 1443 H
M.  Ijumaa, 24 Disemba 2021

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

 [مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Syria inaomboleza kwa Waislamu jumla na kwa watu wa Ash-Sham haswa, mmoja wa Mashababu wake mbeba dawah ambaye pia anajulikana kwa akhlaqi yake njema.

Dkt. Youssef Haj Youssef (Abu Al-Harith),

mnamo Ijumaa 24/12/2021.

Alitumia maisha yake kubeba ulinganizi wa kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu, kupitia njia ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume pamoja na ndugu zake katika Hizb ut Tahrir katika kipindi cha dhurufu zenye giza totoro ambapo alikabiliwa na mateso ya dhalimu wa Ash-Sham, Hafez al-Assad, hivyo alilazimika kuondoka katika nchi yake, Armanaz, na kuishi ugenini. Mwenyezi Mungu Mtukufu alimnusuru kutokana na ukamatwaji wa wafanyakazi wa hizb mwishoni mwa 1999.

Mwanzoni mwa mapinduzi, aliregea Ash-Sham baada ya kutokuwepo kwa muda mrefu na kuendelea kubeba dawah nyumbani, na kufanya kazi za kisiasa na vyombo vya habari, kwani alikuwa naibu mkuu wa Afisi ya Habari huko Ash-Sham katika siku za mwanzo za kuasisiwa kwake.

Ingawa aliondoka Ash-Sham, alibaki kuwa sauti ya vyombo vya habari inayobeba ulinganizi wa haki na sauti inayotetea mapinduzi ya Ash-Sham na kushauri familia na ndugu zake…

Tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia yake na ndugu zake, na tunamuomba Mwenyezi Mungu awatie moyo wa subira nzuri, na ambariki marehemu kwa wingi wa rehema zake; na kumkusanya pamoja na Manabii, wakweli, na Mashahidi na watu wema, na hao ndio maswahaba wema.

Jicho linalia, moyo unahuzunika, na hatusemi ila tu yale yanayomridhisha Mola wetu:

 [إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah: 156].

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Ujumbe wa Wanachama wa Hizb ut Tahrir katika Mazishi ya
Youssef Haj Youssef (Abu Al-Harith)

 
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu