Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  14 Muharram 1444 Na: 03 / 1444 H
M.  Ijumaa, 12 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

(قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاء مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ)

“Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi.” [Aali-Imran: 118]
(Imetafsiriwa)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu alifichua mnamo siku ya Alhamisi kwamba alikuwa na mazungumzo mafupi na Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Syria, Faisal Miqdad, kando ya mkutano wa Harakati Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote uliofanyika Oktoba iliyopita katika mji mkuu wa Serbia Belgrade, na kusema: "Ni lazima tufikie maridhiano kati ya upinzani na utawala nchini Syria kwa namna yoyote. La sivyo, hakutakuwa na amani ya kudumu.” Katika kujibu swali kuhusu iwapo kuna mawasiliano kati ya Uturuki na utawala wa Syria katika ngazi za kidiplomasia na kisiasa, Cavusoglu alisisitiza kuwa mawasiliano kati ya pande hizo mbili kwa sasa yanahusu huduma za kijasusi.

Enyi Waislamu katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Ash-Sham: Kauli za Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Cavusoglu zinathibitisha dori ua kiutendaji ambayo serikali ya Uturuki inatekeleza katika huidumia Marekani, ili kumhifadhi mteja wake Assad, na katika kusisitiza kwake kuyazika mojawapo ya mapinduzi makubwa zaidi katika historia.

Kila mfuatiliaji wa matukio hayo anafahamu vyema kwamba utawala wa Uturuki umetaka tangu mwanzo kuyakabidhi maeneo yote ili kuyaregesha mikononi mwa dhalimu wa Ash-Sham, katika utekelezaji wa kile kinachoitwa suluhu ovu ya kisiasa ya Marekani, baada ya kukabidhi maeneo mengi, kunyang'anya maamuzi ya viongozi wa makundi, kuwapora utashi wao na kuwageuza kuwa mamluki. Wanatumikia maslahi yake na maslahi ya mabwana zake, na orodha ya uhalifu dhidi ya mapinduzi inaendelea ...

Yeyote atakayekutana na waziri wa mambo ya nje wa utawala wa kihalifu wa Syria, akakutana na ujasusi wa Syria, na kujiandaa kwa ajili ya mkutano au mazungumzo ya simu na dhalimu wa Ash-Sham, hapana shaka kwamba yeye ni mpangaji njama dhidi ya mapinduzi ya Ash-Sham, haijalishi hata kama anadai vyenginevyo, kwa hivyo kwa uchache uhusiano naye lazima ukatishwe.

Enyi Waislamu katika Ardhi ya Ash-Sham, makaazi ya Uislamu: Kuibuka kwa maandamano katika yale yanayoitwa maeneo yaliyokombolewa dhidi ya njama za utawala wa Uturuki na wito wake wa maridhiano na utawala huo wa kihalifu, kunathibitisha kuwa mapinduzi yangali yanawaka moto katika nyoyo za vijana wake, na kwamba bado yanadhamiria kuupindua utawala wa kihalifu, na kwamba yanafadhilisha kifo cha heshima kuliko kufikiria tu maridhiano ya aibu, na hatari naye. Pia yanathibitisha ushawishi mkubwa wa rai jumla wakati inapaza sauti yake na kusema neno lake, na kuwalazimisha wapangaji njama na maadui zake kujigeuza rangi kama kinyonga na kuchukua mbinu mpya ambazo hazitafuta aibu ya kufanya kwao biashara na damu na muhanga wa wanamapinduzi katika kuwatumikia maadui zake.

Hili linahitaji kila mtu kuwa katika kiwango cha tukio na kuwajibika, baada ya ukweli kufichuliwa kwa wachache ambao walikuwa bado wamefinika macho yao, kukata kamba na maadui zetu wote wanaongojea msiba wetu, wakiongozwa na serikali ya Kituruki, na kuwaunganisha na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuendeleza njia nyuma ya uongozi wa kisiasa wenye fahamu na ikhlasi, unaobeba mradi wa ukombozi kutoka kwenye kiini cha itikadi ya Umma.

Anachora ramani ya utendakazi kwa mji mkuu ili kuupindua utawala, kuwaondolea watu maovu yake, na kusimamisha utawala wa Uislamu kupitia Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na huku pua za maadui wa Mwenyezi Mungu zikisita kufanya hivyo. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيباً)

 “na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Al-Isra: 51].

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu