Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  5 Safar 1444 Na: 04 / 1444 H
M.  Alhamisi, 01 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kundi la Tahrir Al-Sham Limemteka Nyara Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria Nasser Sheikh Abdul Hai
(Imetafsiriwa)

Mnamo Alhamisi, tarehe 1/9/2022, Vikosi vya Usalama vya Hay'at Tahrir Al-Sham vilimteka nyara mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Syria, Ustadh Nasser Sheikh Abdul Hai, mbele ya nyumba yake katika mjini wa Atarib; hii ilikuwa ni baada ya kauli zake dhidi ya wito wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, anayeutaka upinzani, kufanya maridhiano na dhalimu wa Al-Sham, na msimamo wa serikali ya Uturuki kuhusu utawala wa Bashar Al-Assad.

Enyi Waislamu katika ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham: Dhulma, unyanyasaji, ukandamizaji na kutawaliwaa kunakofanywa juu yenu; lengo lake ni kuvunja azma yenu, kukuwekeni kwenye mazungumzo ya kimataifa, na kukulazimishenu mukubali maridhiano na mnyakuzi wa heshima yenu, muuaji wa watoto wenu, na mvunjaji wa nyumba zenu.

Hapana shaka kwamba jumuiya ya kimataifa inajitahidi kuyazika mapinduzi ya Al-Sham, ambayo yameikalia kwa miaka mingi, na yametia mvi nywele za watawala wake, kwa kutumia zana zake kutoka kwa watawala vibaraka, ambao nao hutumia zana zao kutoka kwa viongozi wa mfumo uliounganishwa wa makundi.

Na hii hapa Hay'at Tahrir al-Sham akiendelea kuwatawala mashababu wa Hizb ut-Tahrir na kutawala shingo za watu, ili kumfurahisha bwana wake wa Kituruki na jumuiya ya kimataifa iliyo nyuma yake, kama viongozi wengine waliosalia wa mfumo wa makundi husika. Kile ambacho dhalimu wa Ash-Sham alishindwa kukifanya katika upande wa kunyamazisha sauti za ukweli na kusitisha mashambulizi dhidi yake, kinatekelezwa na mfumo wa makundi yaliyounganishwa kwa ukamilifu katika utabikishaji wa amri za mdhamini ambaye walimkabidhi uamuzi wao na kuweka rehani azma yao kwake.

Inajulikana vyema, tangu kale na kisasa, kwamba lau isingekuwa vibaraka na wasaliti hawa, wajukuu wa Abu Raghaal, Magharibi kafiri isingeweza kuingia katika nchi za Kiislamu, achilia mbali kukaa humo. Inafanya kazi kwa kuendelea kupandikiza vibarak na kuwanunua waoga; hadi ilipowaingiza madarakani, na hivyo hatima ya Uislamu na Waislamu ikawa mikononi mwa watu waliolaaniwa miongoni mwa wale wasio na khofu na utukufu wa Mwenyezi Mungu.

Moja ya majukumu ya lazima zaidi kwa Waislamu ni kuwapindua watawala hawa vibaraka, na kuuondolea Uislamu na Waislamu maovu yao, ambayo kwa ajili yake yalifanyika mapinduzi yale yanayoitwa Mapinduzi ya Kiarabu, lakini Magharibi Kafiri waliweza, kwa msaada wa watu wake kutoka miongoni mwa watu wetu, kuyazingira na kuyatibua mapinduzi haya, huku ikijitahidi kuyaavya mapinduzi ya Ash-Sham kupitia kwa wale waliouaza hadhi zao na wakaridhika kutumikia amri na maagizo yake, kwa hiyo musiwaruhusu kukuhadaeni na kuyatibua mapinduzi yenu chini ya jina lolote lile.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, makaazi ya Uislamu: Kimya chenu juu ya uhalifu unaotendwa dhidi yenu ni jinai dhidi yenu wenyewe, jinai dhidi ya mapinduzi yenu, na jinai dhidi ya mihanga yenu na damu ya mashahidi wenu, lazima mupaze sauti yenu juu dhidi ya kila anayefanya biashara na mapinduzi haya yatima, kwani Hudhaifah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, amesimulia kutoka kwa Mtume (saw) ambaye amesema:

«وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَتَأْمُرُنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلَتَنْهَوُنَّ عَنْ الْمُنْكَرِ، أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللَّهُ أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَاباً مِنْهُ ثُمَّ تَدْعُونَهُ فَلَا يُسْتَجَابُ لَكُمْ»  

“Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake! Hamtaacha kuamrisha mema na hamtaacha kukataza maovu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atakaribia kuwateremshia adhabu kutoka kwake, kisha mtamuomba wala hamtajibiwa.” [Imepokewa na Tirmidhi].

Munapaswa pia kutabanni uongozi wa kisiasa wenye utambuzi, uaminifu na unyoofu unaotabanni mradi wa wazi wa kisiasa unaochipuza kutokana na itikadi ya Kiislamu unaofanya kazi kuunganisha juhudi za kufikia lengo linalotarajiwa la kupindua utawala wa kihalifu na kusimamisha utawala wa Uislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Mwenyezi Mumngu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal:24].

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu