Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  6 Jumada II 1444 Na: 09 / 1444 H
M.  Ijumaa, 30 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waanzilishi na Wahandisi wa Ugaidi Wakutana Kupambana na Walichokiita Ugaidi na Kuyaavya Mapinduzi ya Ash-Sham
(Imetafsiriwa)

Moscow na Ankara zilitangaza kuwa mawaziri wa ulinzi na wakuu wa idara za kijasusi za Urusi, Uturuki na Syria walifanya mazungumzo jijini Moscow mnamo Jumatano, 28/12/2022. Shirika la Habari la Urusi, likinukuu Wizara ya Ulinzi, lilisema "walijadili njia za kutatua mgogoro wa Syria, tatizo la wakimbizi, na juhudi za pamoja za kupambana na vikundi vya itikadi kali nchini Syria."

Enyi Waislamu katika ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham: Kukutana kwa utawala wa Uturuki na dhalimu wa utawala wa Ash-Sham ni hatua ya juu katika kuyaavya mapinduzi ya Ash-Sham, na mapinduzi haya yatima yanaweza kushuhudia vipindi vyake vya mwisho. Mkutano huo uliofanyika kati ya mawaziri wa ulinzi wa Syria, Uturuki na Urusi una maana kubwa hasa wakati wakuu wa idara za kijasusi za nchi hizo tatu wanapokutana kwa wakati mmoja.

Viongozi wote wa mfumo wa makundi ya kijeshi unaohusishwa kwa majina yake anuwai, ambao wameweka rehani uamuzi wao kwa utawala wa Uturuki na kuuchukua kama uongozi wao wa kisiasa, watajua kwa kuchelewa kuwa ni zana za muda tu ambazo zitatupiliwa mbali baada ya kumalizika kwa dori yao ya mpito. Hii ina maana kwamba vipengee vyote vinalengwa, kwani si chochote bali ni zana ambazo zinapishana, na kwamba kuwepo au kutokuwepo kwao kunahusishwa na uamuzi wa wafuasi wao, na hii imethibitishwa na taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Cavusoglu, alipoeleza utayari wa utawala wake kuhamisha udhibiti wa maeneo ambayo majeshi ya Uturuki yapo kwa dhalimu wa Ash-Sham.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, nyumba ya Uislamu: Dori ya utawala wa Uturuki na uongozi wake wa kisiasa imefichuliwa kwa wale waliouamini miongoni mwa viongozi wa mfumo wa makundi, na kwamba unayasukuma mapinduzi ya Ash-Sham katika kifo chake. Hili linahitaji watu wa mapinduzi ya Ash-Sham, pamoja na vipengee vyake mbalimbali, wachukue hatua haraka ili kuyaokoa mapinduzi yao yatima, lakini hili linaweza tu kufanywa kwa kukataa uongozi wa sasa wa kisiasa ambao utawala wa Uturuki umeutengeneza, na kupitia kutabanni uongozi mpya wa kisiasa unaoyaongoza mapinduzi ya Ash-Sham kuelekea kufikia malengo yake na kushikamana na misimamo yake. Kila mtu anafanya kazi dhidi ya mapinduzi yetu na anataka kuyaavya na kutupilia mbali mihanga mikubwa ya watu wetu.

Ni wajibu wenu, enyi waadilifu, kufanya kazi ya kuunganisha juhudi na nguvu zenu mbele ya yale ambayo Makafiri wa Magharibi wanapanga njama dhidi yenu, hasa kwa kuporomoka kwa dhalimu wa Ash-Sham na migogoro anayoishuhudia, utawala wa Urusi kuzama kwenye kinamasi cha Ukraine, na utawala wa Iran kushughulishwa na matatizo yake ya ndani. Msiposonga pamoja, mtalipa gharama kwa pamoja, kwa hiyo unganeni na muunde makundi na mabaraza ya kimapinduzi, na fuateni kila njia inayowakutanisha na unganisheni juhudi zenu nyuma ya uongozi wa kisiasa wenye fahamu na wa dhati ambao una mradi, kutoka kwa ndugu zenu na watu wenu, kwa sababu harakati ya kibinafsi haina tija, na ikiwa tutatembea bila ya muongozo bila ya kuwa na mradi ulio wazi, basi juhudi na mihanga yetu itakuwa kwa ajili ya miradi ya wengine. Turegesheni uamuzi wetu na tufuate muongozo na utambuzi ili kuinusuru dini yetu na wanaodhulumiwa miongoni mwa ndugu zetu, na malengo yetu ya kwanza yawe ni kufanya kazi ya kuupindua utawala wa kihalifu na kusimamisha utawala wa Kiislamu kwenye magofu yake katika kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na kwa wema na heshima hiyo, nawafanye kazi wenye kufanya.

Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَى وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]

“Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Al-Ma’idah 5:2].

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu