Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  23 Rajab 1444 Na: 10 / 1444 H
M.  Jumanne, 14 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tetemeko la Ardhi Limefichua Sura Halisi ya Jumuiya ya Kimataifa na Mashirika Yake ya Kimataifa

(Imetafsiriwa)

Watu wa Ash-Sham waliamka alfajiri siku ya Jumatatu, 6/2/2023 na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa nyuzi 7.8 kwenye kipimo cha Richter, ambalo lilidumu kwa karibu dakika mbili, na kuacha uharibifu wa kutisha katika maeneo mengi ya miji ya Syria, kwani idadi ya waliokufa katika tetemeko hilo ilifikia 3,581, na zaidi ya majeruhi 12,400. Hii ni hadi jioni ya Jumatatu, tarehe 13/2/2023, huku shughuli za utafutaji zikiendelea kutoa miili ya waliokufa.

Enyi Waislamu katika ardhi iliyobarikiwa ya Ash-Sham:

Tetemeko hilo la ardhi limefichua sura halisi ya jumuiya ya kimataifa na mashirika yake ya kimataifa, ambayo yalipuuza maafa makubwa yaliyowakumba watu wa Ash-Sham. Pia ilifichua uhalisia wa mifumo haribifu ya vibaraka na serikali zinazopo. Badala ya kukimbilia kufungua vivuko na kutuma vikosi vya kutoa misaada, walivifunga huku wakitoa kisingizio kuwa barabara zilizokuwa wazi ni za kupitisha tu maiti za watu wa Ash-Sham, wale waliokufa nchini Uturuki. Kisha walisimama bila ya hatua yoyote na kuongeza muda wa kuziingiza timu za uokoaji hadi siku ya tano ya tetemeko la ardhi, yaani baada ya matumaini ya kupata manusura kufifia, katika jitihada za kuongeza idadi ya vifo. Kisha walipoamua kupeleka msaada kaskazini mwa Syria, walijaribu kuituma kupitia genge la dhalimu wa Ash-Sham katika kujaribu la kuregesha mfumo wa mauaji na uhalifu.

Mchunguzi wa tabia ya jumuiya ya kimataifa na jinsi ilivyoshughulikia maafa; atatambua kwamba, Jumuiya ya Kimataifa inataka kuongeza mateso ya watu wa Ash-Sham na kuwazidishia mashinikizo katika kujaribu kuvunja utashi wao na kuwatiisha katika sera zake, hususan baada ya vuguvugu kubwa katika maeneo yaliyokombolewa, wakikataa maridhiano na dhalimu wa Ash-Sham.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, Makaazi ya Uislamu:

Mumeuthibitishia ulimwengu wote kwamba muna uwezo wa kukabiliana na matatizo na kuzishinda dhiki kwa umoja wenu, na kwamba imani yenu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na katika ahadi na ushindi Wake (swt), ni madhubuti mithili ya milima madhubuti. Haya ndiyo yanayowatia hofu Wamagharibi makafiri; ambao mpaka sasa hajaweza kuvunja utashi wenu na kuua ari ya mapinduzi katika nafsi zenu, basi msiombe usaidizi na misaada isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu (swt), kwani nchi za makafiri zimeungana tu kuupiga vita Uislamu na Waislamu, kuwaua na kuwapora mali zao. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّى يَرُدُّوكُمْ عَنْ دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا)

“Wala hawatoacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza.” [Al-Baqara: 217].

Huu ndio uhalisia wao na hili ndilo lengo lao. Basi shikamaneni nyote kwa kamba ya Mwenyezi Mungu peke yake na unganeni katika kumtii Yeye. Kazi yenu na iwe ya pamoja na iliyo na mpangilio, kwani ni kazi yenye tija. Hivi ndivyo mulivyohisi katika msiba huu mkubwa. Na ufuate uongozi wa kisiasa unaofahamu, mwaminifu na wa dhati ambao unaotabanni mradi wa wazi wa kisiasa unaotokana na itikadi (Aqidah) ya Waislamu ili kukuongozeni kwenye usalama katikati ya mawimbi haya ya maporomoko. Katika hilo yako mafanikio na ustawi,

(فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ وَأَنْتُمُ الْأَعْلَوْنَ وَاللَّهُ مَعَكُمْ وَلَنْ يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ)

“Basi msiregee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mtakao shinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu.” [Muhammad: 35].

Kwa kumalizia, tunawaambia watu wetu wanaoteseka katika ardhi ya Ash-Sham: Mwenyezi Mungu ayafanye malipo yenu kuwa makubwa zaidi, awasamehe maiti zenu, awaponyeni machungu yenu, awaponye majeraha yenu, na awatieni moyo wa subira na faraja, na hutusemi tu yanayomridhisha Mola wetu Mlezi:

(إنا لله وإنا إليه راجعون)  

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.”

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu