Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  24 Dhu al-Hijjah 1444 Na: 13 / 1444 H
M.  Jumatano, 12 Julai 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Madai ya Tovuti ya France 24 ni ya Uongo na ya Kashfa katika Jaribio la Mbaya la Kuficha Harakati ya Amani katika eneo la Kaskazini lililo Kombolewa
(Imetafsiriwa)

Katika ripoti ya kushangaza ya vyombo vya habari juu ya ukamataji na maandamano ambayo yamefanyika katika maeneo yaliyokombolewa kwa zaidi ya miezi miwili, waangalizi wa France 24 walitushangaza kwa mkusanyiko wa uwongo wa makusudi ambao chaneli kama France 24 haifai kufanya isipokuwa ikiwa wahariri wake bado wangali chini ya athari ya mshtuko wa maandamano yaliyozuka katika nchi yao iliyokumbwa na mgogoro. Endapo tutapuuza makosa ya kimbinu katika kuandaa ripoti, kama vile kutaja vijiji na miji iliyoasi kwa majina tofauti, kama walivyoita Al-A'tma badala ya Atmeh, Deir Al-Hasan badala ya Deir Hassan, Al-Sharara badala ya Al-Sahara, Al-Sarmada badala ya Sarmadah, na Hamas badala ya Hama, pia ilitajwa kuwa tume inadhibiti maeneo ya Al-Hasakah, ambayo ni jirani na Aleppo na Hama, na taarifa zote mbili sio sahihi. Tunasema: Ikiwa tulipuuza makosa haya ya kimbinu na tukasimama kutaja uongo mkubwa katika ripoti hiyo, ambapo hadithi ya kubuni imesukwa kuhusu matukio. Ambapo ripoti hiyo iliifafanua Hizb ut Tahrir kama “kundi la ndani la Kiislamu lenye wapiganaji... Hizb haikuwa chini ya uhangaishaji, lakini tangu Februari mwaka jana ilianza kubeba silaha... Baada ya wapiganaji wake kufyatulia risasi gari la usalama na kumuua mmoja wa wanachama wake, msako ulianza!” Tukizungumzia hadithi hii ya uongo, tunasema:

Kwa kuanzia, Hizb ut Tahrir sio kundi la kijeshi la ndani, na haina wapiganaji, kama ripoti ilivyotaja. Badala yake, ni chama cha kisiasa cha kimataifa, na hakina mrengo wenye silaha. Wanachama wake hawakubeba silaha Februari iliyopita, au Februari nyingine yoyote! Zaidi ya hayo, wanachama wa Hizb hawakuhangaishwa na kukamatwa na Hay'at Tahrir al-Sham katika miezi hii miwili pekee, kama ulivyotaja, bali kwa miaka iliyopita, tangu wakati viongozi wa Hay'at Tahrir al-Sham. (HTS) walipoamua kufuata mradi wa Magharibi unaolenga kuyamaliza mapinduzi. Ama kuhusu kampeni hii ya ukamataji, haikuanza baada ya tukio la mauaji lililotajwa kwenye ripoti, bali kabla yake. Na kisa kilichotajwa kwenye ripoti kuhusu mauaji hayo ni kisa kile kile cha mtu asiyejulikana aliyejifunika uso wake, Diaa al-Omar. Ama kuhusu ukweli, mnaweza kuupata kwa kwenda tu mitaani katika vijiji hivi vya waasi na kumuuliza mtakayemkuta huko, sio kwa kukariri kama kasuku yale waliyoyasimuliwa waongo kwenye vyombo vyao rasmi vya habari!

Hatimaye, tunasema kwamba mkitaka kuandika ripoti nyingine za vyombo vya habari kuhusu suala hilo, mnaweza kuusifia uhalisia jinsi ulivyo bila kudanganya na kupotosha ukweli. Vyenginevyo, ni bora kwenu kuwaacha watu waliokoloniwa kutokana na maovu yenu, na mjishughulishe na migogoro ambayo Ufaransa ya kikoloni inateseka nayo.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu