Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  1 Muharram 1445 Na: 01 / 1445 H
M.  Jumatano, 19 Julai 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali za Syria na Iran Zaendelea na Msururu wa Uhalifu katika Aina zake Zote
(Imetafsiriwa)

Tovuti za habari ziliripoti habari za moto mkubwa ambao uliteketeza nyumba kadhaa za kale na maduka katika soko la Sarouja, magharibi mwa msikiti wa Umayyad jijini Damascus.

Ni muhimu kutaja kuwa moto huo ulienea katika Kituo cha Hati za Kihistoria, ambacho kinaendeshwa na Kitengo cha Hati za Kihistoria katika Kurugenzi ya Vitu vya kale na Makavazi ya serikali hiyo ya kihalifu. Moto huo uliteketeza zaidi ya hati milioni tano ambazo ni pamoja na majina ya familia, nasaba, na ukoo wa zamani wa zama za Uthmani.

Dalili zote zinaonyesha kuwa moto huu ni sehemu ya msururu wa vitendo vilivyofanywa na serikali za Syria na Iran kufanya mabadiliko ya idadi ya watu ndani na pambizoni mwa Damascus. Na hili linajiri baada ya uhalifu wa uharibifu na kuhamishwa kwa watu wake ndani yake, na kisha uhalifu wa kuteketeza hati zote ambazo zinathibitisha umiliki wa watu wa asili wa ardhi hii.

Ni uhalifu mbaya mpya ulioongezwa katika safu ya uhalifu uliofanywa na serikali za Syria na Iran na wanamgambo wao ili kuwapa uraia wanamgambo hawa ndani ya ash-Sham na kuwapa umiliki wa majumba/mali baada ya kuchoma kila kitu kinachofichua ukweli juu ya unyakuzi wao wa ardhi hii kuwa kisu kilichoingizwa ndani ya mwili wa watu wa ash-sham.

Kuwahisabu wahalifu hao ambao waliwauwa watu wa mapinduzi ya Ash-Sham na kuwafukuza majumbani mwao kutakuwa hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, mikononi mwa watu waaminifu wa Ummah huu, baada ya kuipindua serikali ya kihalifu na kusimamisha utawala wa Uislamu juu ya magofu yake.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ]

“Na siku hiyo waumini watafurahi * Kwa nusra ya Mwenyezi Mungu.” [Ar-Rum 30:4-5]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu