Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  23 Jumada II 1441 Na: 04 / 1441 H
M.  Jumatatu, 17 Februari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Utawala wa Uturuki Unaendelea Kutekeleza Jukumu lake Kikamilifu
Kuyarudisha Tena Mapinduzi ya Ash-Sham katika Safu ya Utawala wa Kihalifu

(Imetafsiriwa)

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar alitangaza kuwa nchi yake itachukua hatua zote dhidi ya wale ambao hawatekelezi usitishaji mashambulizi huko Idlib, pamoja na wenye misimamo mikali, akisisitiza kuwa Ankara "itawalazimisha wao kutekeleza."

Shirika la Anatolia lilimnukuu Akar akisema kuwa Uturuki itatuma vikosi vya ziada vya kijeshi huko Idlib "kwa lengo la kufanikisha kukomesha kwa mashambulizi na kuifanya iwe ya kudumu," akiongeza kuwa Ankara "italifuatilia eneo hilo."

Hakuna shaka kuwa Kafiri Mmagharibi anafanya kazi kwa bidii tangu mwanzo wa mapinduzi kuwarudisha tena watu wa Ash-Sham kwenye utumwa; kumlinda kibaraka wake asing’olewe. Ilitumia namna na njia zote ikitegemea vifaa vyake kutekeleza hili, kutoka kwa watawala vibaraka, haswa watawala wa Waislamu katika nchi zinazoizunguka Ash-Sham, kama watawala wa Iran, Qatar, Emirates, Saudi Arabia and Uturuki, wale ambao walikuwa na jukumu kubwa katika mambo ambayo yametimia, na labda jukumu la hatari zaidi lilikuwa sehemu ya utawala wa Uturuki iliyoweza kupunguza uongozi wa makundi na kuyadhibiti kwa nguvu. Na walishindwa hata kuhama baada ya kupoteza uamuzi na utashi wake, na hata kupanga njama na Utawala wa Uturuki kukabidhi maeneo na utekelezaji wa makubaliano. Utawala wa Uturuki bado unatekeleza jukumu lake kikamilifu na kutoa taarifa hapa na pale ukidai wasiwasi wake juu ya damu ya Waislamu katika Ash-Sham; na mbio zake za kumaliza mateso yao.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, Makao ya Uislamu

Watawala wa Uturuki hawatofautiani sana na viongozi wa makundi; wao, kwa upande wao, hawamiliki uamuzi wao na matakwa yao, isipokuwa kwa kiwango walichoruhusiwa na mabwana zao, na kwa hivyo utawapata wakiongezeka katika mikutano, ushirikiano na kuwasiliana na serikali zote za Amerika na Urusi katika ngazi zake zote

Kile kiitwacho suluhisho la kisiasa la Amerika ndio kile ambacho Kafiri Mmagharibi anakitafuta kuwalazimishia na kuwawekea watu wa Ash-Sham kwa lazima, na bila shaka sio hatari ndogo kuliko uamuzi wa kijeshi, yote ni sawa licha ya kuwa ni aina tofauti, na taarifa zilizotolewa na Waziri wa Ulinzi wa Uturuki ni katika kuandaa suluhisho hili.

Kuna wale ambao wanaendelea kufanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya mapinduzi ya Ash-Sham kubadili njia yake na kufuata njia ya sawa, na kuna wale ambao wanafanya kazi usiku na mchana kumaliza hatua ya utawala wa kulazimishiwa na kuiendea Khilafah ya Uongofu kwa njia ya Utume ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitupatia bishara kuihusu, ambayo itamaliza mateso ya Waislamu na kutekelezewa wao sheria ya Mola wao ambayo ni furaha ya duniani na akhera. Kwa hivyo musiiambatanishe mioyo yenu kwa yeyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu (swt); na ni lazima musiwaamini maadui wa Mwenyezi Mungu kutoka katika serikali ya kibaraka ya kihalifu; na jueni kuwa uokovu wenu na uokovu pekee wa Waislamu ni kufanya kazi kwa bidii na ukweli pamoja na wanaofanya kazi ya kusimamisha Khilafah ya Uongofu kwa njia ya utume, na mwisho mwema ni kwa wale wanaotenda mema.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu