Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  3 Rajab 1441 Na: 06 / 1441 H
M.  Alhamisi, 27 Februari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi Ndugu Hasan Duwaik Abi Adnan
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Syria inatangaza kwa Umma wa Kiislamu kifo cha mmoja wa mashababu wake, Hasan Duwaik Abi Adnan ambaye alifariki kuelekea kwa Mola wake usiku wa Alhamisi sawia na 27/02/2020 wakati wa bomu la uhalifu na chuki, huko mjini Al Atareb upande wa magharibi mwa Aleppo, ambapo malipuzi yaliishambulia nyumba yake, na akafa kama matokeo yake, Mwenyezi Mungu amrehemu.

Abu Adnan - tunamchukulia yeye na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi - kwamba alikuwa mmoja wa wafanyikazi imara katika safu za Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Alibaki katika magereza ya Bashar na sela zake za ujasusi kwa miaka mingi. Baada ya kuachiliwa, aliendelea kutekeleza jukumu lake la kubeba dawah, na alifanya kila juhudi kutoa ushauri na maono ili kuyaweka Mapinduzi ya Ash-Shaam nje ya nchi zinazo husishwa na Amerika. Wito wa kukata mahusiano na nchi za kuunga mkono na za kula njama; na kuvunja mistari mekundu iliyo chorwa, ambayo ilimuweka wazi kwa vitisho na kukamatwa mikononi mwa Makao makuu ya Ukombozi wa Al-Sham (Hay'at Tahrir al-Sham), lakini hilo halikumuogopesha wala kumtisha yeye, badala yake aliendelea kuzungumza na kulingania ukweli kwa uvumilivu na akiwa na matumaini ya thawabu kwa Mwenyezi Mungu hadi kifo kilipomjilia.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu ambariki kwa rehema nyingi; kukaa katika mabustani yake ya nafasi; amkubali yeye miongoni mwa mashahidi; na kuharakisha usimamishaji wa dola ya Khilafa Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itamaliza wahalifu; na kutekeleza sheria za Dini, Yeye (swt) ndiye Mlezi na mwenye uwezo wa hilo. Na wala hatusemi isipokuwa yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika! Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika, kwake yeye tutaregea.”

 Ahmad Abdul Wahhab

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu