Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  23 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 09/1445
M.  Ijumaa, 31 Mei 2024

Wito wa Dhati kutoka Tanzania:

Majeshi ya Waislamu Lazima Yasonge Mbele Mara Moja ili Kuiokoa Gaza

(Imetafsiriwa)

Kufuatia kampeni inayoendelea dhidi ya mauaji ya kihaiki, maumivu na dhulma za Waislamu wa Gaza zinazofanywa kikatili na umbile nyakuzi la Kiyahudi kwa msaada wa Marekani na mataifa mengine ya Kimagharibi, Hizb ut Tahrir / Tanzania imejitolea Ijumaa ya leo katika kuendesha dua maalum kwa Waislamu wa Gaza katika misikiti mbalimbali ya Tanzania.

Dua ziliambatana na Khutba na kalima zenye kupaza sauti dhidi ya mauaji ya halaiki na kuwasilisha suluhisho la Kiislamu na faradhi ya Mwenyezi Mungu inayoyataka majeshi ya nchi za Kiislamu hususan Misri kuingilia kati mara moja kuliuangamiza kabisa umbile la Kiyahudi na kuwaokoa Waislamu wa Palestina na kuukomboa msikiti mtakatifu wa Al-Aqsa.

Pia, khutba na kalima ziliwakumbusha waziwazi Waislamu kwamba dhulma, mateso, mauaji ya halaiki ya Waislamu huko Gaza na kwengineko ni matokeo ya kutokuwepo kwa Dola ya Kiislamu (Khilafah) ambayo Waislamu duniani kote wana jukumu na faradhi wa kiwahyi ya kuisimamisha tena huku nukta kianzilishi yake ikiwa katika Ulimwengu wa Kiislamu ili kuzuia mauaji na dhulma kama hizo zisitokee tena.

Dua, Khutba na bayan zilifanyika katika baadhi ya misikiti ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga na kadhalika ambapo Sheikh Mussa Kileo, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir Tanzania aliongoza dua hizo katika Masikiti Rahma, Buguruni jijini Dar es Salaam.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awazidishie istiqama (uthabiti) ndugu zetu wa Gaza, akiwamiminia subra nyingi (uvumilivu) na Aharakishe Nusra (ushindi) wake kwao na Waislamu wote wa mashariki na magharibi - Ameen.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir
Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu