Jumamosi, 14 Muharram 1446 | 2024/07/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  2 Dhu al-Hijjah 1445 Na: 1445 / 10
M.  Jumamosi, 08 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Tanzania Yafanya Visimamo vya Kuyataka Majeshi ya Waislamu Kuiokoa Gaza

(Imetafsiriwa)

Kufuatia kampeni ya Hizb ut Tahrir / Tanzania inayoendelea dhidi ya mauaji ya halaiki, ukatili, maumivu na dhulma za Waislamu wa Gaza zinazofanywa kinyama na umbile vamizi la Kiyahudi kwa uungaji mkono wa Marekani na mataifa mengine ya Magharibi.

Hizb ut Tahrir / Tanzania ilifanya visimamo baada ya swala ya Ijumaa (7 Juni 2024) katika sehemu mbalimbali kukemea ukatili wa umbile la Kiyahudi na kuwasilisha suluhisho la Kiislamu juu yake.

Wazungumzaji katika visimamo hivyo mbali na kulaani kampeni hiyo ya mauaji ya umbile la Kiyahudi kwa Waislamu wa Gaza, pia wamewakumbusha na kuwataka Waislamu haswa majeshi ya ulimwengu wa Kiislamu kusonga mbele mara moja kuwaokoa Waislamu wa Gaza kwani ulinzi wa maisha ya Waislamu ni faradhi muhimu ya Mwenyezi Mungu kwani ilisisitizwa na Mtukufu Mtume (saw) katika mwezi kama huu (Dhu al-Hijjah) katika Hija yake ya Kuaga.

Visimamo vinne vilifanyika katika jiji la Dar es Salaam nje ya Msikiti wa Lindi na Msikiti wa Idrissa yote ikiwa huko Kariakoo, Msikiti wa Kichangani huko Magomeni na Msikiti wa Dar us Salaam huko Kigamboni. Pia vyengine vilifanyika katika mikoa ya Mtwara na Mwanza.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) Aharakishe Nusra (ushindi) Wake kwa Gaza na Waislamu wote wa mashariki na magharibi - Amin.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu