Ijumaa, 29 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  24 Rabi' II 1446 Na: 1446 / 04
M.  Jumapili, 27 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ukiritimba wa Kisiasa wa Vifaa vya Ujenzi Zanzibar:
Pigo Jengine kwa Masikini

(Imetafsiriwa)

Hivi karibuni, serikali ya Zanzibar ilipiga marufuku usafirishaji na matumizi ya mawe katika shughuli za uashi.

Marufuku hiyo ilitangazwa na Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Hassan Shaibu Kaduara, ambaye alisisitiza kuwa uamuzi wa kuzuia matumizi ya rasilimali za mawe umefikiwa kutokana na uharibifu wa mazingira unaoendelea.

Waziri huyo alidai kuwa serikali imekuwa ikipokea bugudha kubwa kutoka kwa wananchi (bila kutaja ni kina nani na mahali walipo), juu ya athari za mazingira zinazotokana na uchimbaji wa mawe. Hivyo, wananchi wanaombwa kutumia vitalu vya saruji katika kipindi cha marufuku badala ya mawe hasa katika ujenzi wa majengo yao.

Agizo la Serikali ya Zanzibar la kutumia vitalu vya saruji badala ya mawe katika ujenzi wa misingi ya nyumba ni kejeli kwa wananchi kwa vile inajua fika kwamba bei ya vitalu hivyo ni kubwa kutokana na awali kuingiza siasa uchimbaji wa mchanga wa ujenzi mwaka 2017, hali iliyopelekea kupanda juu mno kwa bei ya rasilimali hiyo.

Uzoefu unaonyesha wazi kwamba kuingizwa kwa mikono ya kisiasa katika vifaa msingi vya ujenzi husababisha uhaba bandia, bei ya juu na mfadhaiko na pia huleta mzigo usioweza kubebeka katika sekta ya uashi hasa kwa watu wa kawaida.

Mkono wa sasa wa kisiasa katika matumizi na uchimbaji wa mawe ya ujenzi hauna tofauti na ule wa awali kwenye mchanga wa ujenzi. Yote miwili ikimaanisha malengo maovu ya ukiritimba wa serikali na ulimbikizaji wa manufaa kwa wanasiasa na wasaidizi wao kwa gharama ya maumivu na bei ya juu kwa watu maskini.

Takwimu za Serikali za 2017 kuhusu suala la mchanga wa ujenzi zinafichua zaidi uwepo wa uovu wa serikali katika mandhari hii.

Ilisemekana mnamo mwaka 2017 kuwa Zanzibar ilibakiwa na hekta 14 tu za mchanga wa ujenzi, huku sekta yake ya ujenzi inatumia zaidi ya hekta 10 kila mwaka.

Swali linaloulizwa hapa ni je, tangu 2017 hadi sasa, hizo hekta 14 za mchanga zilizobaki, bado zipo au zimeisha?

Kwa kuwa watu bado wanaendelea kujenga. Inasikitisha sana kwamba serikali ya Zanzibar badala ya kurahisisha mambo na kuweka mazingira ya hamasa ambayo yangewawezesha wananchi wa kawaida kumiliki nyumba zao, inazifanyia biashara ya juu michanga na mawe ya ujenzi kwa visingizio vya uongo vya ‘uhaba’ wa mchanga, ‘uharibifu wa mazingira’ bila kusahau kisingizio chengine cha ubadhirifu cha kulinda ‘maeneo ya uwekezaji’ kupitia njia hiyo, inatekeleza unyakuzi wa wazi wa ardhi na viwanja kwa ukandamizaji wa wananchi katika maeneo kama vile Bweleo na Fumba (Unguja Mjini, Wilaya ya Magharibi ‘B’) ambayo yaliimarishwa kwa miaka mingi kutokana na ardhi iliyokufa na kugharimu watu pesa nyingi, nyakati na jasho.

Sisi katika Hizb ut Tahrir/Tanzania tunapenda kutaja mambo matatu kufuatia suala hili:

1. Tunaitahadharisha kwa dhati kabisa serikali ya Zanzibar kuepusha kufadhaisha zaidi sekta ya ujenzi inayofanya maisha ya mtu wa kawaida kuwa magumu zaidi hasa katika harakati zao za kumiliki nyumba. Kwa kufanya na kusababisha hali ya ugumu na ukali katika maisha ya watu ni dhulma za wazi kwa raia na khiyana kwao na itahesabiwa vikali na Mwenyezi Mungu Mtukufu kesho Akhera na kufanya mambo kuwa magumu zaidi katika maisha haya. ‘Aisha (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akiomba dua nyumbani kwangu: «اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئًا فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَاشْقُقْ عَلَيْهِ وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئًا فَرَفَقَ بِهِمْ فَارْفُقْ بِهِ»  “Ewe Mwenyezi Mungu! Wafanyie ukali wale wanaoutawala Ummah wangu kwa ukali, na wafanyie upole wale wanaoutawala Ummah wangu kwa upole.” [Imepokewa na Muslim].

2. Dhuluma hizi zinatokana na tabia ya maumbile asili ya mfumo wa kibepari na serikali zake za kidemokrasia kote duniani. Mfumo huo unadai kuwa uko katika nafasi ya kuwatumikia wananchi, lakini badala yake ukweli ni kunyonya manufaa zaidi kutoka kwa migongo ya watu. Hii ina maana ubepari hauna sifa ya kutawala wanadamu, kwani ni mfumo wa kurundika riba kwa gharama yoyote ile hata ikiwa inadhuru raia.

3. Ni dola ya Khilafah Rashida pekee (ambayo inapaswa kusimamishwa tena katika ulimwengu wa Kiislamu) iliyo sifa zote za usimamizi wa uadilifu, uaminifu katika kuwatumikia wanadamu kwa haki bila ya kujali rangi zao, dini au asili yao.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu