Alhamisi, 12 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  7 Jumada I 1446 Na: 1446 / 06
M.  Jumamosi, 09 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Tanzania Yatoa Wito kwa Majeshi ya Waislamu Kuiokoa Gaza

(Imetafsiriwa)

Kufuatia kampeni ya zaidi ya mwaka ya mkaliaji kimabavu umbile la Kiyahudi, ushenzi na dhulma kwa Waislamu wa Gaza na ardhi jirani za Waislamu zinafanywa kwa msaada wa Marekani, na mataifa mengine ya Kimagharibi na ushirikiano wa vibaraka katika ardhi za Waislamu.

Jana 08 Novemba 2024, Hizb ut Tahrir / Tanzania ilifanya visimamo baada ya swala ya Ijumaa katika sehemu mbalimbali kupinga ukatili wa umbile la Kiyahudi na kutoa wito kwa majeshi ya Waislamu hususan Misri, Jordan, Syria, Uturuki, Saudi Arabia nk, kusonga mara moja ili kuwaokoa Waislamu wa Gaza.

Visimamo vilifanywa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania kama vile, Zanzibar, Mwanza, Tanga na kisimamo kikubwa zaidi kilifanywa viungani mwa Dar es Salaam nje ya Msikiti wa Kwa Bimtumwa eneo la Tandale.

Mapema kabla ya kisimamo cha jiji la Dar es Salaam, mmoja wa wanaharakati wa Hizb alitoa khutba ambapo aliwakumbusha na kuwaonya wanazuoni, watawala vibaraka wa Waislamu, Umma na majeshi ya Waislamu juu ya madhara makubwa kwa kuwatelekeza Waislamu wa Gaza ambao wanachinjwa na umbile la Kiyahudi.

Kisimamo cha Dar es Salaam kilichohudhuriwa na vyombo kadhaa vya habari pia kiliunganishwa na dua ikiongozwa na Sheikh Mussa Kileo, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir Tanzania, huku Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania, Masoud Msellem akiwasilisha ujumbe maalum kwa majeshi ya ulimwengu wa Kiislamu kama ifuatavyo:

UJUMBE KUTOKA HIZB UT TAHRIR TANZANIA KWA MAJESHI YA MISRI, JORDAN, SYRIA, UTURUKI, SAUDI ARABIA

Enyi Majeshi! katika Nchi za Waislamu,

Gaza tayari imeshaharibiwa na sasa ni Lebanon, munangoja nini ili mujitokeze kutoa nusra yenu ya kijeshi?!

Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu umbile la Kiyahudi likisaidiwa na kuungwa mkono kikamilifu na Marekani na nchi nyingine za magharibi, na linaendelea kufanya mauaji ya kikatili ya halaiki, kubomoa majengo na miundombinu mjini Gaza.

Sio tu kwamba adui huyu ameendelea kutekeleza mauaji kama hayo nchini Lebanon, lakini anashambulia Iran na Syria. Je, ni udhalilifu aina gani munaojiweka ndani yake na Ummah wote wa Kiislamu, bila kuchukua hatua yoyote ya kuhisika?

Ndani ya mwaka mmoja, biladi sita za Waislamu zimeshambuliwa; Palestina, Lebanon, Syria, Iran, Iraq na Yemen huku mkiwa hamuna habari.

Kadhia hii ina pande mbili pekee; upande wa maadui wa Uislamu, upande wa pili ni ule wa Umma wa Kiislamu. Je, mungeshirikiana na nani na kusimama naye? Je, mafungamano yenu na Ummah si mafungamano ya imani ya Kiislamu? Je, munafikiri muko salama vya kutosha kiasi kwamba maadui wasingeendelea kushambulia nchi nyingine za Waislamu na hata kukushambulieni?

Ole wenu! Adui hataridhika kamwe, na jibu linalohitajika kwake ni risasi pekee sio kujisalimisha.

Imeripotiwa kuwa watu 43,000 wameuawa shahidi mjini Gaza au kwa mujibu wa vyanzo vyengine idadi hiyo ni karibu 200,000 na 7000 au idadi isiyojulikana ya watu hao wako chini ya vifusi na zaidi ya 100,000 kujeruhiwa, huku zaidi ya 80% ya nyumba zikiwa zimeharibiwa.

Manusura mjini Gaza wanazurura huku na huko, wakiwa wamezingirwa na jeshi la Kiyahudi na kuzuiwa kupata misaada. Hakuna chakula, maji, au huduma za matibabu. Mbali na kupigwa mabomu, pia wanakufa kwa njaa. Karibu hospitali zote na vituo vya matibabu vimebomolewa.

Enyi Majeshi katika ulimwengu wa Kiislamu! Je hawa sio ndugu zenu?

Zaidi ya misikiti 600 imebomolewa.

Bila shaka, hivi ni vita vya wazi dhidi ya Uislamu.

Enyi Majeshi katika ulimwengu wa Kiislamu!

Je, ni fahari gani kubwa zaidi kwa Muislamu kuliko ushindi katika medani ya jihad au kufa shahidi? Je, hamjui kwamba kuachana na jihad katika hali hii ni moja ya madhambi makubwa yanayoangamiza?

Adui bado ana kiu ya kumwaga damu takatifu ya Waislamu. Haridhiki tu na kuyapiga mabomu majengo pekee; badala yake, anaendelea kulipua hata mahema ambayo waathirika dhaifu miongoni mwa wanawake na watoto wamejihifadhi nayo.

Enyi Majeshi katika ulimwengu wa Kiislamu,

Ikiwa mtaacha kuwasaidia ndugu zenu, munadhani nani atajitokeza kuwasaidia?

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُواْ فِي سَبِيلِ اللّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الآخِرَةِ إِلاَّ قَلِيلٌ * إِلاَّ تَنفِرُواْ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلاَ تَضُرُّوهُ شَيْئًا وَاللّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” (Al- Tawba: 38-39)

Enyi wapenzi majeshi katika ulimwengu wa Kiislamu, msiogope chochote, kwani Ummah wote uko nyuma yenu. Hakika jeshi la Mwenyezi Mungu daima litanusuriwa na kushinda.

[وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ]

“Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.” (37:173) Mwisho.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aharakishe Nusra (ushindi) wake kwa Gaza na Waislamu wote wa mashariki na magharibi - Amin.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu