Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  28 Rabi' II 1446 Na: 1446 / 05
M.  Alhamisi, 31 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

IMF Kusifia Uchumi wa Tanzania ni Kuficha Uovu wa Shirika hilo

(Imetafsiriwa)

Kauli ya karibuni ya Mkurugenzi Mtendaji wa IMF kwa Afrika bwana Willie Nakunyanda aliyoitoa Washington DC katika makao makuu ya IMF kwa ujumbe wa Tanzania, kwa kusifia, kupongeza na kuurembaremba uchumi wa Tanzania si chochote zaidi ya kebehi na dharau kwa Tanzania, wananchi wake na watu wa nchi changa kwa ujumla. Kauli hiyo inalenga kuficha nyuma ya pazia lengo baya, la kikoloni na la dhulma la taasisi za IMF na Benki ya Dunia (Bretton Woods Institutions).

Ikiwa Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba ulikuwa jijini Washington ukiungana na mawaziri wengine wa fedha wa Afrika katika jukwaa lao linaloitwa ‘Caucus Africa’ lililoundwa na shirika la IMF mwaka 1963, ambapo IMF hukutana na jukwaa hilo mara moja kwa mwaka katika makao makuu yake Washington ili kulipatia jukwaa hilo la (mawaziri wa Afrika) maelekezo na maagizo mbalimbali ya sera za kiuchumi na kifedha kutoka kwa IMF na Benki ya Dunia. Basi inakuaje tena mataifa hayo ikiwemo Tanzania yaambiwe yana uchumi wao huru, kiasi cha kusifiwa na kupongezwa?

Taasisi mbili hizo (IMF na Benki ya Dunia) ziliasisiwa na dola za kibepari zikiongozwa na Marekani mara baada ya Vita vya Pili vya Dunia, ambapo kwa taasisi hizo Marekani imejimilikisha ubwana na ukiritimba mkubwa wa sera za kiuchumi na kifedha kilimwengu kwa kukomesha matumizi ya fedha kwa kipimo cha dhahabu na kuufanya uchumi wa kilimwengu kutawaliwa na dolari yake ya Kimarekani pekee.

Kwa upande mwengine, kuundwa kwa taasisi mbili hizo (IMF na Benki ya Dunia) kumeleta majanga ya kijamii na kiuchumi kwa kuzidhoofisha nchi changa ikiwemo Tanzania, kuzitenza nguvu nchi changa na kuzilazimisha mzigo usiohimilika wa madeni chini mpango wa (mashirika hayo) unaoitwa ‘Mpango wa Marekebisho ya Kimuundo’ (The Structural Adjustment Program) Mpango uliopelekea hali ngumu ya maisha na uchumi tete ndani ya Tanzania na sehemu nyingine (katika nchi changa).

Uovu wa taasisi hizo ambazo ni wakala wa wakoloni unadhihirika wazi kila mahala hususan nchi changa.

Muda umewadia kwa wanafikra makini katika nchi changa ikiwemo Tanzania kutafiti suluhisho mbadala la kiuchumi kando na ubepari na vyombo vyao vya kikoloni, wajitenge mbali na uchumi huo na vyombo vyao, kisha wachukue mfumo bora na wa kiuadilifu wa Uislamu ambao haunyonyi wala kudhulumu si katika uchumi wala katika miamala mingine.

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir

Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu