Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tunisia

H.  2 Rabi' II 1442 Na: 1442/17
M.  Jumanne, 17 Novemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali Yarefusha Ufungaji wa Misikiti ili Kuendeleza Mapambano na Dini ya Mwenyezi Mungu

(Imetafsiriwa)

Kutoka kwa Abu Umamah Al-Bahli (ra), kutoka kwa Mtume (saw) kwamba amesema:

«لَتُنْقَضَنَّ عُرَى الإِسْلَامِ عُرْوَةً عُرْوَةً، فَكُلَّمَا انْتَقَضَتْ عُرْوَةً تَشَبَّثَ النَاسُ بالتِي تَلِيهَا، وَأَوَّلُهُنَّ نَقْضاً الحُكْمُ وَآخِرُهُنَّ الصَلَاةُ».

"Hakika mafundo ya Uislamu yatafunguliwa moja baada ya moja, na kila fundo moja likifunguliwa watu watakamata linalofuata, na fundo la kwanza kufunguliwa ni Hukmu na la mwisho ni swala".

Watawala wa Tunisia wamefikia kiwango kikubwa katika ujasiri wao dhidi ya dini ya Mwenyezi Mungu; baada ya kuutenga kwao Uislamu kutoka katika utawala, na kuitowesha kwao sheria ya kweli ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa dola na jamii, na kuupiga vita Uislamu kwa jina la kupambana na ugaidi, hawa hapa leo wanaharibu alama zilizosalia za Uislamu, kwa kufunga misikiti na kuzuia swala za Ijumaa na jamaa kwa kisingizio cha kupunguza maambukizi ya janga la Korona, ambapo inachukuliwa kuwa moja ya dhuluma kali zaidi kwa Dini ya Mwenyezi Mungu. Misikiti ni nyumba za Mwenyezi Mungu, na hakuna aliye na milki ya kuzifunga, kwa hali yoyote, hivyo basi itakuwaje ikiwa lengo limekusudiwa kwa dhati yake?! Uamuzi wa serikali mnamo Oktoba 29, 2020, ulilenga kufunga misikiti na sio shughuli zingine nyingi za maisha, na ndilo linalothibitisha kuwa janga la Korona limekuwa kigingi cha kuondoa alama zilizosalia za Uislamu; ambapo vipi mtu mwenye akili timamu anaweza kusadiki kuwa serikali inatafuta usalama wa watu kwa kufunga misikiti huku ikiwaruhusu kukusanyika mbele ya idara za umma na katika vyombo vya uchukuzi, sehemu kubwa za kibiashara, vilabu vya pombe nk?!! Halafu je, kwani wanaokwenda misikitini hawakufuata hatua za usalama, kwa nini serikali haikuwaachilia kutoka kwa utaratibu huu kama ilivyofanya kwa wengine?!! Au Uislamu ndio kiungo dhaifu katika nchi hii?!! 

Enyi Watu wa Tunisia: 

Hakika madai ya serikali ya kuchunga usalama wenu kutokana na maambukizi ya janga hilo ni upuuzi mtupu, kejeli, na hoja za uongo ambazo hazimpumbazi yeyote, na hakika kurefusha ufungaji misikiti hadi 6 Desemba 2020 M, licha ya maandamano dhidi ya kufungwa kwake na matakwa ya watu wema ya kufunguliwa kwake, inathibitisha kuwa serikali inaendelea katika ukaidi wake licha ya watu kupinga hatua zake ovu.

Na hakika sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia tunatoa wito:

 1- Watoaji maamuzi ni lazima wachunge kutokana na ukaidi wao na warudishe akili zao, wamche Mwenyezi Mungu Mola wao, na kurekebisha amri yao kwa kuharakisha kufungua nyumba za Mwenyezi Mungu na kutangaza toba yao kwa uhalifu huu mkubwa, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَى فِي خَرَابِهَا أولئك مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿.

"Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa. Duniani watapata hizaya na Akhera watapata adhabu kubwa." [Al-Baqara: 114]

2- Maimamu na makhatibu wamche Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wafungue misikiti, na wasishirikiane na yeyote katika dhambi hili. Mtume (saw) amesema:

«لَا طَاعَةَ لِمَخْلُوقٍ فِي مَعْصِيَةِ الْخَالِقِ».

"Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba".

 3- Umma uliosalia, utangaze kwa Mwenyezi Mungu kuwa mbali kwao na uovu huu, na kila mtu afanye awezalo kuwalazimisha wasimamizi warudi nyuma kutokana na uhalifu huu mkubwa.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿.

 "Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa." [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tunisia
Address & Website
Tel: 
http://www.ht-tunisia.info/ar/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu