Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tunisia

H.  6 Muharram 1443 Na: 1443/01
M.  Jumamosi, 14 Agosti 2021

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

)مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً)

"Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo." [Al-Ahzab: 23]

)Imetafsiriwa(

Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia kinamuomboleza mmoja wa wanachama wake, mbebaji wa da'wah na dada mwema:

Karima Sassi (Um Muhammad)

Ambaye alikwenda kwa Rehma za Mwenyezi Mungu Mtukufu huku akiwa amejitolea maisha yake kumtii Mwenyezi Mungu na kubeba ulinganizi wa kuregesha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Dada yetu, Karima Sassi, Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa thabiti, akidumu katika duara za Hizb na katika masomo ya elimu, akiwapenda dada zake, aliyejitolea kufanya kazi, akitazamia ushindi, akitarajia Khilafah, akiwa na matumaini ya kuishuhudia hadi roho yake iliporudi kwa Muumba wake.

Twamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amfinike kwa upana wa Rehma zake na amruhusu kuingia ndani ya pepo Yake kubwa, na amlipe kwa niaba yetu, Uislamu na Waislamu malipo bora.

Ni cha Mwenyezi Mungu kile alichotoa na ni cha Mwenyezi Mungu kile alichochukua, nasi tunasema tu yale yanayomridhi Mola wetu Mlezi pekee, utakatifu ni wake Yeye:

(إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعونَ)

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara: 156].

Msemaji Rasmi wa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tunisia
Address & Website
Tel: 
http://www.ht-tunisia.info/ar/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu