Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tunisia

H.  20 Muharram 1443 Na: 1443/03
M.  Jumamosi, 28 Agosti 2021

Kais Saied Aziba Uhalifu wa Kuvidhibiti Vikosi Vyetu vya Jeshi ili Kutumikia Mizozo ya Kimataifa kupitia Kumshambulia Mpinzani Wake wa Kisiasa, Spika wa Bunge Lililosimamishwa
(Imetafsiriwa)

Kais Saied, Kamanda Mkuu wa Jeshi nchini Tunisia, hakuwaaga maafisa wetu na majeshi kutoka kitengo chetu cha helikopta za kijeshi, Alhamisi, Agosti 26, 2021 katika kambi ya jeshi huko Al-Awina, katika kutekeleza uamuzi uliotolewa tarehe 13/7//2021, ambapo Bunge na Rais wake liliidhinisha wakati huo kutuma vikosi vya jeshi ng'ambo ... hakuwaaga kwenda kuwasaidia watu wetu nchini Palestina na Gaza, ambao watu wao wamezingirwa na kuuawa, na hakuwatuma kusuluhisha mzozo baina ya Waislamu nchini Yemen, wala hajali kuhusu ndugu zetu wa Turkestan Mashariki wala watu wetu huko Burma, lakini badala yake aliwatuma kwa idhini ya bunge na rais wake kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa, nchi iliyokumbwa na mizozo ya kikabila na jinsi, iliyochochewa na ushawishi mbaya wa Ufaransa, na uingiliaji wa dola zengine za kikoloni na mamluki wao. Jukumu ambalo Kais Saied alikubali kwamba jeshi la Tunisia litafanya huko ni kulinda "raia" kutokana na vitendo vya makundi yenye silaha. Wasiwasi wa makundi hayo yenye silaha nchini Afrika ya Kati leo, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ni Waislamu wachache ambao wanakabiliwa na mchakato wa mauaji ya halaiki yanayofanywa na Wakristo walio wengi, na wanadai haki zao halali za utawala adilifu na maisha bora. Haki zao zinakiukwa huku kukiwa na usaidizi wa wazi kutoka Ufaransa, na kubeba kikosi cha Tunisia kuwa uso wa ndugu zao Waislamu. Mojawapo ya majukumu ya watoto wetu maafisa na wanajeshi ni kulinda wafanyikazi na mali ya Shirika la Umoja wa Mataifa huko, ambalo ndio mzizi wa shida zetu zote na uhalalishaji wa mashambulizi ya maadui wa Umma wetu dhidi yetu kila mahali. Pia linasaidia michakato ya upokonyaji silaha, kupunguza uhamasishaji na uoanishaji upya.

Lakini, rais wa nchi, wakati akishinikiza watoto wa jeshi letu kutumikia mipango ya kikoloni na mizozo ya kimataifa na kusaidia vikosi vya uovu ambavyo vinafanya kazi kuzika mapambano ya watu kwa ajili ya kujikomboa kutokana na udhalimu wa ukoloni chini ya udanganyifu wa Umoja wa Mataifa na kutabanni maneno ya maadui, aliridhika kutokana na ngawira kwa kurudi kwa vikosi vyetu vya jeshi kutoka kwa huduma hii "kwa ushuhuda wa shukrani na kuridhiwa" Na hakupata chochote, huku akizamishwa katika "mahusiano ya kimataifa" kwa kuwahusisha maafisa na wanajeshi wetu katika aibu hii. Kais Saied hakupata chochote cha kutawaza misheni zao isipokuwa kuvipotosha vikosi vya jeshi kwa kuwaingiza katika mizozo yake ya ndani na wapinzani wake wa kisiasa kwa kupepesa macho kutoka kwa spika wa bunge lililosimamishwa, ili kuficha uhalifu anaousimamia katika misimu yake yote.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[لَا تَجِدُ قَوْماً يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءهُمْ أَوْ أَبْنَاءهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ]

“Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao.” [TMQ Al-Mujadila: 22].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tunisia
Address & Website
Tel: 
http://www.ht-tunisia.info/ar/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu