Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari

H.  29 Rabi' I 1440 Na: 1440 / 07
M.  Ijumaa, 07 Disemba 2018

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia Inatangaza Uzinduzi wa Kampeni
(وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللهِ حُكْماً)
“Na nani aliye mbora zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu”
(Imetafsiriwa)

Tunisia hivi sasa imo katika kipindi kigumu baada ya wale tuliowafikiria kuwa ni watawala kuyatelekeza majukumu yao msingi na kuziwachia dola za msalaba za kikoloni na wafanyikazi wake ndani ya Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa kuamua sera za kiuchumi, kifedha na kijamii mpaka nchi ikadhibiti usambaratikaji wa kiuchumi licha ya kwamba kulikuwa na madeni makubwa.

Kutokana na ushindani wa kisiasa nchini na kushughulishwa kwa vyama tawala kutokana na mizozo yao ya kindani badala ya kulifanyiakazi taifa. Na upande mwingine watu wamekata tamaa na nidhamu ya kisiasa na vyama vya udanganyifu, ambayo ilidhihirishwa kwa kuepuka upigaji kura za Manispaa zilizopita. Sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Tunisia tunatangaza kwa Ummah uzinduzi wa kampeni ya kisiasa ili kutoa muongozo kwa wale wanaofikiria kisiasa ili kuwapelekea kutoa suluhisho msingi juu ya matatizo ya Ummah na kuukomboa kutokana na aina zote za ukoloni na utumwa, kwa kusimamisha nidhamu ya kisiasa ya kiutawala, kiuchumi na kijamii kwa msingi wa Uislamu na vipengee vyake vya kisheria. 

Kampeni hii mpya, ambayo tumeichagulia kichwa:(وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللهِ حُكْماً)  “Na nani aliye mbora zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu” itaendelea kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kwa wiki kadhaa na itakuwa ni fursa ya kuonyesha uwezo wa nidhamu ya Kiislamu katika kuleta mabadiliko msingi ambayo Bwana wa Ulimwengu ametutaka sisi tujikombowe kutokana na madhalimu, vibaraka wakoloni na tuishi kwa hadhi na izza ndani ya nidhamu ambayo inahifahdi itikadi na ustaarabu wa Ummah na kudhamini haki ya kumchagua nani wa kutawala.

Enyi Waislamu ndani ya nchi ya Zaytouna:

Sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Tunisia tunawaalika mushirikiane nasi katika kampeni hii, na muweke wazi hisia zenu katika kuzikataa sera za kikoloni ambazo zinalenga kuitia katika utumwa nchi hii na watu wake, na mufanyekazi kwa bidii pamoja na mukhlisina na watu wa nguvu ili waweze kuinusuru Dini yao, watu wao na Ummah kwa lengo la kuingia katika historia na cheo kikubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kutokana na kuwaridhia kwake.

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa."  [Al-Anfaal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah ya Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu