Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tunisia

H.  9 Rabi' I 1443 Na: 1443/08
M.  Jumamosi, 16 Oktoba 2021

 Msimamo wa Hizb ut Tahrir wa Kuelezea Upuuzi wa Usekula Unaouhofisha Ukoloni na Wafuasi Wake

 (Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Ijumaa, 15 Oktoba 2021, Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia iliandaa visimamo baada ya swala ya Ijumaa katika mji mkuu wa Tunisia na miji ya Kairouan na Sfax; kuzungumzia upuuzi wa usekula na njia ya kisiasa inayovuruga nchi, kukiwa hakuna tofauti kati ya njia ya kabla na baada ya taratibu za Julai 25. Kauli mbiu kama "Hapana kwa demokrasia, hakuna kwa udikteta, bali Khilafah wa Kiislamu" zilipazwa, na kisha hotuba zilitolewa za kutoa wito wa ukombozi wa nchi kutokana na utawala wa Magharibi na zana zake za ndani na kukataliwa kwa Usekula, pamoja na viungo vyake viwili, mfumo wa kidemokrasia wa bunge na mfumo wa urais wa kidikteta, na kuufanya Uislamu pekee uwe ndio msingi wa utawala na sheria, kupitia kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume.

Visimamo hivyo vilifanyika mbele ya Msikiti wa Al-Fath katika mji mkuu wa Tunisia, Msikiti wa Lakhmi huko Sfax, na Misikiti ya Al-Ghufran na Al-Naqra huko Kairouan, baada ya mamlaka ya utawala kukataa ombi la kufanywa visimamo hivyo katika viwanja na kuugeuza Ukumbi wa Manispaa na Barabara ya Al-Thawra katika mji mkuu huo kuwa kambi za usalama ili kuzuia utitiri wa washiriki wa visimamo hivyo, kisha ikatuma kikundi cha magari ya usalama hadi Msikiti wa Al-Fath kuzuia watu kukusanyika kwa ajili ya maandamano hayo. Pia, Mashababu wa Hizb ut Tahrir walikamatwa huko Sfax, ambao baadaye waliachiliwa siku hiyo hiyo.

Hatua hizi za kutapatapa na majaribio makali ya kuitenga Hizb ut Tahrir na kuzuia mradi halisi wa Kiislamu kutowafikia umati, wakati wakiacha wamiliki wa miradi ya Kimagharibi kuionyesha viwanjani huthibitisha bila shaka yoyote kuwa serikali nchini Tunisia hazipo isipokuwa kwa uamuzi wa nchi za Kimagharibi kwani zinavyowakilisha dhamana ya uhai kwa nchi na watu chini ya utawala wa Magharibi, kupitia kuupiga vita Uislamu na kuuweka mbali na utawala na sheria na kutokana na kuathiri umati.

Enyi Watu nchini Tunisia:

Bourguiba na Ben Ali walitawala kulingana na mfumo wa urais kwa miongo mingi, na baada yao Tunisia iliishi chini ya utawala wa kidemokrasia wa bunge hadi Rais Kais Saied alipowapindua mnamo Julai 25 kuanzisha tena utawala wa urais, kulingana na katiba ambayo haitofautiani na katiba zilizotungwa na wanadamu zilizolazimishwa na dola za kikoloni juu ya Umma wa Kiislamu baada ya kuvunjwa kwa Khilafah na kutengwa kwa Uislamu kutoka kwa utawala na sheria. Hakuna tofauti kati ya katiba kabla au baada ya mapinduzi, kwani Umma haukuvuna kutoka kwa utawala wao chochote isipokuwa taabu, dhiki, utovu wa usalama, na mizozo ya kisiasa na kiuchumi. Suluhisho la kile tulicho ndani yake ni kufafanua upya kwa usahihi na kwa uwazi vipimo vya mapinduzi na kusisitiza kwamba ni kupindua mfumo mzima, ukombozi kutokana na ushawishi wa Magharibi mkoloni, kisha kukutanisha na kuunganisha msingi mmoja pekee wa mradi wa kisiasa ulio wazi uliovuliwa kutoka kwa Qur'an na Sunnah ambao Hizb ut Tahrir inauwasilisha, na kusonga mbele pamoja na Hizb na uongozi wake wa kisiasa kuelekea kumridhika Mwenyezi Mungu Mtukufu, kufikia malengo ya mapinduzi na maslahi na furaha ya Ummah hapa duniani na kesho Akhera, na kuregesha hadhi na utukufu wa zamani wa Umma kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tunisia
Address & Website
Tel: 
http://www.ht-tunisia.info/ar/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu