Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 12 Safar 1443 | Na: 1443/06 |
M. Jumapili, 19 Septemba 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia inamuomboleza mmoja wa wanachama wake, mheshimiwa na mbebaji ulinganizi:
Belqasim A’mari (Wilaya ya Sidi Bouzid)
ambaye alifariki mnamo Jumamosi, 11 Safar 1443 H sawia na 18/9/2021 M, akiwa na umri wa miaka 68, ambayo aliitumia kumtii Mwenyezi Mungu na kubeba ulinganizi wa kuregesha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Belqasim A’mari alikuwa mmoja wa wale waliojiunga na safu za Hizb ut Tahrir miaka ya themanini ya karne iliyopita, na alidhuriwa kwa kufanya kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Alisimamishwa zaidi ya mara moja na mamlaka tawala kwa sababu alikuwa amebeba Dawah. Hakubadilika wala kugeuka badala yake alibaki thabiti juu yake, akiwa amebeba dawah, mlinzi mwaminifu wa Uislamu, aliwapenda wanachama, akifurahi kwa ushindi, akimuomba Mwenyezi Mungu (swt) aishuhudie Khilafah hadi alipokufa huku akiwa kwenye njia hiyo.
Ewe Mwenyezi Mungu, msamehe na umrehemu, na umpe makaazi katika Pepo Zako pana, na upandishe daraja ya katika mbingu ya juu kabisa pamoja na manabii, wakweli, mashahidi na wema, na hao ndio wandani bora. Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye tutarudi.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara: 156].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |