Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  16 Sha'aban 1444 Na: 1444/19
M.  Jumatano, 08 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tamko la Mwisho la Kongamano la Kila Mwaka la Khilafah 2023 "Kuporomoka kwa Dola ya Usasa na Hakuna Wokovu Isipokuwa katika Dola ya Khilafah"
(Imetafsiriwa)

Mkutano wa kila mwaka wa Khilafah 2023 ulijadili suala la kwanza nyeti na kuu; Uislamu na Khilafah zilikuwa ndio kitovu ambacho hotuba za wazungumzaji zilizunguka juu yake, kwani ni wajibu ambao Mwenyezi Mungu Amewaamrisha Waislamu wote, na kama hadhara badali pekee yenye uwezo wa kuutoa Ummah, na kwa hakika wanadamu wote, kutoka katika matatizo yao.

Baada ya kufungua kwa usomaji mzuri wa aya za Quran Tukufu, hotuba zilijikita katika nukta zifuatazo:

1- Dola ya usasa, ambayo ilibadilika-badilika baina ya utawala wa kidikteta na wa kidemokrasia, katika hali zote hizo mbili ni kizazi cha ukoloni kilichoasisiwa baada ya kuvunjwa Khilafah, na ambacho kingali kinatutawala mpaka sasa.

2- Dola ya usasa katika nchi za Kiislamu ni dola tegemezi, ambapo usimamizi wa mambo ya umma ulifungamanishwa na maslahi ya ukoloni na makampuni yake ya uporaji, ambapo maslahi ya watu wa nchi yalipotea na migogoro ikaenea hadi hali hiyo ikawa ni kama inavyojulikana na kila mtu.

3- Na kwamba usasa katika nchi za Kiislamu haukuwa ila ni njia ya kuuweka mbali Uislamu na kuutenganisha na maisha ya Waislamu ili watu wa nchi wabaki kuwa watumishi na watumwa wa makampuni ya kibepari.

4- Na kwamba usasa haukuwa chochote ila ni mchanganyiko mseto wa fikra mbovu za Kimagharibi zilizozalisha tabaka la kisiasa la kisekula ambalo ni zuri tu katika kutumikia Magharibi na mabwana kunyakua fursa kutoka kwa damu ya vijana wa Ummah ili masekula wavune matunda ya mihanga hiyo. Haya ndiyo yaliyokuwa matendo yao tangu kuvunjwa kwa Khilafah hadi Ummah ulipowafichua, na ndiyo mapinduzi yake yaliyoanzia Tunisia.

5- Hali ya kisiasa (watawala na upinzani), iliyoundwa na dola ya usasa na demokrasia, haina msaada na imepooza. Haiwezi kupata suluhu ya migogoro yote hii isipokuwa yale ambayo duru za kikoloni na vituo vyao vya utafiti vinaiamuru, na kazi yake kubwa ni kupiga vita mradi wa Khilafah na kuzuia kuanzishwa kwake, jambo ambalo linafanya isiwezekane kufikia wokovu.

6- Kufeli kwa dola ya kisasa, kashfa ya demokrasia, na mpasuko wa ubepari haviwezi kutafutiwa ufumbuzi kupitia kubadili sura, kuwahisabu baadhi ya mafisadi, au kufanya mazungumzo wanayodai kuwa ni ya kizalendo baina ya wanasiasa bandia.

7- Kwa kufichuliwa kwa demokrasia ndani na nje ya nchi na kupasuka kwa ubepari, hakuna tumaini lililobaki kwa wanadamu isipokuwa kurudi kwenye Uislamu, dini ya mwisho ambayo Mola wa walimwengu aliiteremsha kwa mwisho wa Manabii na Mitume. Hakuna matumaini yoyote kwa hilo isipokuwa Umma wa Kiislamu kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, ili kuikomboa nchi kutokana na mafungamano yote ya kikoloni, na kuchunga mambo ya watu kwa mujibu wa hukmu za Uislamu mtukufu.

8- Kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume maana yake ni kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu, kuunganisha Ummah chini ya bendera ya mtawala mmoja ambaye ni Khalifa wa Waislamu, kuondoa ushawishi wowote wa nchi za Magharibi na zana zao za ndani, kuregesha mamlaka yake juu ya uwezo wake na mali yake zilizoporwa, kurejesha mwamko wake na dori yake katika kueneza mwongozo na kuongoza ulimwengu kwa nuru tukufu ya Uislamu, na kusimamisha fardh kifaayah kwa Waislamu wote.

9- Khilafah ni mradi mtukufu na jumuishi wa kisiasa wa Mwenyezi Mungu unaounganisha Ummah katika chombo kimoja cha kisiasa ambamo ndani yake nguvu, rasilimali na mali za wanadamu zimeunganishwa. Hizb ut Tahrir kwa upande mmoja imebeba mradi kamili na uliounganishwa wa kimungu ambao iliuvua kutokana na wahyi, ulioandikwa katika vitabu vyake vingi, na kujumlishwa kisheria katika rasimu ya katiba, na ni mradi ambao unajiandaa kubadili uso wa dunia katika nyanja zote za maisha, katika siasa, utawala, uchumi, elimu, na mahusiano ya kimataifa...n.k.

10- Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia inahamasisha nguvu za Waislamu, kufanya kazi nayo kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, kutabikisha Sharia ya Kiislamu, na kukusanya Ummah katika kuunga mkono mradi wake wa kuchukua uongozi, na kutafuta nusra kutoka kwa watu wenye nguvu na wasioweza kuathirika ili kuifanya Tunisia kuwa kitovu cha Dola ya Khilafah, kwa kufuata mfano wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika kusimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina. Na matumaini yake kwa Mwenyezi Mungu ni makubwa kujitayarisha kwayo kutoka kwa watu wenye nguvu na wasioweza kuathirika wale ambao wataisaidia kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu ya ushindi na tamkini, na kutimiza bishara njema ya Mtume wake (saw) katika Hadith iliyopokelewa na Imam Ahmad:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ)

“Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Swala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” [Al-Hajj 22:41].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu