Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  16 Rabi' I 1446 Na: 1446/04
M.  Alhamisi, 19 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uchaguzi ni Njia ya Kuendeleza Mfumo wa Kisekula ambao lazima Ubadilishwe kwa Kusimamisha Khilafah
(Imetafsiriwa)

Tangu kuzuka mapinduzi ya Umma nchini Tunisia mwishoni mwa mwaka 2010, Hizb ut Tahrir imesisitiza kuwa mradi pekee wa kihadhara wenye uwezo wa kuyafanikisha mapinduzi hayo na kufikia matakwa ya wanamapinduzi unatokana na kuupindua utawala wa kisekula na badala yake kuubadilisha kwa mfumo adilifu wa kisiasa, na hili linaweza tu kufanywa kupitia Uislamu, chini ya dola moja; dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Hizb ut Tahrir imekabiliana na majaribio ya ukoloni ya kuzalisha tena utawala ule ule kupitia chaguzi ambazo zimefanyika tangu uhuru wa nchi hii chini ya mwavuli wa katiba iliyoundwa na mwanadamu inayotenganisha dini na maisha. Hizb ut Tahrir imetahadharisha dhidi ya njia nzima ambayo ukoloni wa kimsalaba wa Kimagharibi umeainisha kwa ajili ya mapinduzi hayo, ikiwa ni pamoja na kuurudisha tena utawala ulioanguka kupitia kutunga katiba mseto, shirikishi ya kisekula isiyozaa chochote, bali vibaraka wanaodhibitiwa na nchi za magharibi, wanaolinda maslahi yao na kulinda mfumo wa kutunga sheria na kuliondoa taifa katika mabadiliko yenye tija yanayoegemezwa juu ya Uislamu.

Kwa hiyo, licha ya kauli mbiu zinazoenea leo kuhusu kupiga vita ufisadi, kuikomboa nchi hii na kuregesha uamuzi huo, uchaguzi ujao wa rais wa tarehe 6 Oktoba 2024 si chochote zaidi ya mchezo ambao wahusika wake ni mienendo ya kisiasa, yaani watawala na wapinzani, na mwelekezi ni ukoloni wa kimsalaba wa Magharibi. Kwa hivyo, sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia tunathibitisha ukweli ufuatao:

1- Watu walipofanya uasi, waliasi dhidi ya kila aliyehusika na misiba yao iliyosababishwa na Magharibi, vibaraka wake, na tawala za kikatiba zilizotungwa na mwanadamu ambazo hazitawali kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, na kwa hilo watu hawataki machafuko, lakini badala yake wanataka mabadiliko ya kina na makubwa kulingana na kitambulisho chao cha Kiislamu. Hili halitafanyika kupitia chaguzi chini ya mwavuli wa usekula, bali kupitia chaguzi halisi ambazo mwavuli wake ni Qur’an na Sunnah, katiba pekee ya Waislamu.

2- Tawala zinazotawala katika nchi za Kiislamu zimetokana na nchi za Magharibi, na kuendelea kwake ni mikono mwa nchi za Magharibi, kwa sababu tawala hizi ni dhamana tu kwa Wamagharibi kuendeleza ukoloni na utawala wao juu ya Waislamu.

3- Katika kila uchaguzi, tawala hizi huanzisha migogoro ili kuwaondoa watu kwenye mradi mkubwa wa Uislamu, na ambao maisha yao yanapotea na kuangamizwa vizazi vya Waislamu. Vita hivi vinaongozwa na kudhibitiwa na balozi za Magharibi, na hutawaliwa na mamlaka ya kimataifa na ya kikanda, hivyo matokeo ya uchaguzi ni kifuniko tu cha mchakato wa kufanya maamuzi ili kuipa uhalali wa uamuzi huru.

4- Imedhihirika kwamba nguvu za kweli za Umma katika nchi za Kiislamu lazima zisogee kukomboa utashi wao. Licha ya uhai na uimara wa vuguvugu la wananchi, utawala huo hauwezi kupinduliwa, na nchi haiwezi kukombolewa kutoka katika utiifu wa kisiasa wa nchi za Magharibi isipokuwa tu kwa watu wenye mamlaka kushikamana na watu wao, ili mzozo huo utatuliwe kwa manufaa ya taifa, ili iwe huru na kukombolewa kutoka kwa utumwa na utawala wa Magharibi.

5- Mwamko wa mataifa haupatikani kwa kubadilisha mtawala au kurekebisha katiba, bali ni kwa kupindua utawala mzima na sura zake zote za kifikra, kitamaduni na kisheria. Hii ndiyo njia pekee ya kuvunja minyororo ya Magharibi ya kikoloni, na kisha kuungana kwa msingi wa mradi wa wazi wa kisiasa unaotokana na Quran na Sunnah kama ilivyowasilishwa na Hizb ut Tahrir, na kusonga mbele na Hizb ut Tahrir na uongozi wake wa kisiasa kuelekea kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kufikia maslahi ya Umma na furaha yake katika maisha haya ya dunia na Akhera; kwa kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu