Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 25 Rabi' II 1446 | Na: 1446/06 |
M. Jumatatu, 28 Oktoba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia kinazindua kampeni yenye kichwa “Ufisadi wa Elimu Unatokana na Ufisadi wa Serikali, na Marekebisho Yanahitaji Mabadiliko ya Utawala.”
(Imetafsiriwa)
Kwa kuzingatia mgogoro mkubwa unaoathiri sekta zote muhimu nchini kutokana na ushawishi mkubwa wa wakoloni wanaodhibiti taasisi zake kuu, kuzorota kwa sekta ya elimu kumekuwa na athari kubwa sana. Kuzorota huku kunaathiri kila mtu nchini Tunisia— kina baba, kina mama, walimu, na wanafunzi vilevile—kutokana na mshikamano wake tata na pande nyingi zinazopishana. Kurudi shule hivi majuzi kuliashiria sura nyingine katika msururu wa shida, uchovu, upungufu, na kufadhaika kwa wazazi, wanafunzi, na walimu vile vile.
Wakati huohuo, utawala wa sasa unaendelea kufuata sera za ajira hatarishi na kuwanyonya walimu kimali na kimaadili, na hivyo kutengeneza mazingira yenye mashaka yenye hisia za ukandamizaji, dhulma, na mateso.
Katika mazingira ya shule yasiyo salama, ambapo wafanyibiashara wa dawa za kulevya na wahalifu wanazurura, sambamba na miundombinu mibovu na michafu inayoashiria kuporomoka kwa kile kinachoitwa “Dola ya Uhuru” hali ya udanganyifu na sarabi, kuna mitaala ya kizamani iliyosheheni fikra zenye sumu zenye chuki dhidi ya Aqidah (itikadi) ya Kiislamu. Hii imesababisha kutojua kusoma na kuandika na ubora duni wa elimu, na kufichua kufeli kwa serikali kufikia malengo msingi ya elimu: kujua kusoma na kuandika, na kujenga Aqida sahihi ya Kiislamu.
Kwa kuzingatia haya yote, tunaweza tu kuashiria uwazi na ukamilifu wa picha hii: kafiri mkoloni anayedhibiti hatamu za mamlaka nchini Tunisia anataka kudumisha hali ya mvutano, msukosuko na uchovu nchini, na elimu ikiwa ni moja ya njia za kufikia lengo hili.
- Dola ya kitaifa iliyoanzishwa na Bourguiba haiwezi tena kutoa usalama, elimu, au kudumisha hadhi ya binadamu, ambayo ni matokeo ya kimaumbile na yanayotarajiwa kwa wale wenye kufikiri na kutafakari.
- Kinachojengwa juu ya batili kiasili ni batili. Dola iliyojengwa juu ya kanuni ya kutenganisha dini na maisha, na ambayo ujenzi wake unaathiriwa—kama sio kusimamiwa—na kafiri wa kikoloni, haitarajiwi kuwatumikia watu wake; badala yake, ni kama upanga juu ya vichwa vyao, ikiwauza kwa manufaa ya wengine.
- Kwa hivyo, lazima tuviite vitu kwa majina yake halisi: dola ya kitaifa ya Bourguiba imeanguka.
- Kinachotuhusu katikati ya msukosuko huu ni swali: Je, tunaletaje mabadiliko? Na je, tunatokaje katika mgogoro huu?
Katika muktadha huu, Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kinazindua kampeni yenye kichwa: “Ufisadi wa Elimu Unatokana na Ufisadi wa Serikali, na Marekebisho Yanahitaji Mabadiliko ya Serikali.”
Kampeni hiyo, InshaAllah, itashughulikia maeneo matatu yafuatayo:
- Mizizi na historia nyeusi ya mbinu ya elimu ya Bourguiba nchini Tunisia.
- Natija na matokeo ya sera ya elimu ya kisekula, lugha ya Kifaransa na mgogoro wa kimaadili na kifikra unaoathiri vijana wa leo.
- Suluhisho: mbinu ya kielimu inayoegemezwa kwenye Uislamu, inayosimamiwa na Khilafah—hii itapatikana vipi? Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى * وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]
“Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika. * Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Ta-Ha:123-124].
Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |