Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  4 Jumada I 1446 Na: 1446/07
M.  Jumatano, 06 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kushiriki katika Mafunzo ya Kijeshi pamoja na Adui wetu ni Fedheha kwa Majeshi yetu na Usaliti kwa Watu wetu mjini Gaza
(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 1/11/2024, Wizara ya Ulinzi ilitoa taarifa ikisema: “Tunisia itakuwa mwenyeji, kuanzia Novemba 4 hadi 15, wa zoezi la majini la kimataifa “PHOENIX EXPRESS 24”, kwa ushirikiano na Kamandi ya Marekani ya Afrika, kwa ushiriki wa takriban wanajeshi 1,100 na waangalizi wanaowakilisha nchi dada na rafiki 12, ambazo ni Algeria, Libya, Morocco, Mauritania, Senegal, Uturuki, Italia, Malta, Ubelgiji, Georgia, na Marekani, pamoja na Tunisia, nchi mwenyeji.”

Kwa kuzingatia kauli hii, ambapo uongozi wa jeshi la Tunisia, nchi ya Kiislamu, unatangaza bila ya aibu kwamba inaviweka vikosi vya jeshi chini ya uongozi wa majeshi yenye uadui, sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia tunathibitisha yafuatayo:

• Amerika ni nchi adui ambayo kwa kweli inapigana nasi kwa sababu inaongoza vita vya kuwaangamiza watu wetu huko Gaza. Inalisaidia umbile la Kiyahudi na kulinusuru kwa fedha na silaha na kulipatia uhai, ili liweze kuwaua Waislamu na kuwatesa vikali.

• Watu wetu wanaodhulumiwa huko Gaza damu zao zimemwagwa kwa bei nafuu, na maadui wa karibu na mbali wamewashambulia. Wanangojea mtu wa kumfukuza adui huyu, lakini watawala na viongozi wa majeshi yao nchini Tunisia, Algeria, Morocco, Libya, Mauritania na Uturuki wanayafunga majeshi ya Waislamu kufanya mafunzo pamoja na adui bega kwa bega katika muungano wa aibu na fedheha ambayo yenyewe ni fedheha; kuunga mkono adui na kuwaangusha ndugu na familia!

• Miondoko hii ya kijeshi ni sehemu ya mpango wa Amerika katika kanda, ambayo inahitaji; kwanza, uwepo wa kijeshi kwa ajili ya kuyazima majeshi ya Waislamu, ili yasiharakishe kupigana na umbile la Kiyahudi, bali wayabadilishe kuwa vikosi vya kuzuia vyenye kulinda umbile hilo na magenge yake, na kuigeuza Tunisia kuwa kituo cha operesheni ambapo majeshi ya kanda hii yanatumiwa kuhudumia ajenda zake katika kanda na duniani. Wanaoitwa “watawala” katika nchi zetu wamewawezesha kuwa na uwanja wa harakati ambao ulianza kidogo na sasa unapanuka, huku mafunzo yakisimamiwa na AFRICOM kila mwaka.

• Taarifa ya Wizara ya Ulinzi inadai kuwa inashirikiana na Kamandi ya Marekani ya Afrika. Je, inajuzu kuwasaidia adui wakati wa vita?! Je, nchi inayodai ubwana inawezaje kutumia vikosi vyake vya majeshi kuwatumikia maadui wa watu wake chini ya pazia ya ulinzi na mafunzo ya kijeshi na kiusalama?!

Enyi Waislamu, Enyi viongozi watukufu na walio huru: Watawala wa kanda hii wameshirikiana na adui wakati wa vita, na badala ya kuyaelekeza majeshi yao kuelekea Palestina ili kuwasaidia watu wake na kuwaokoa kutokana na kuchinja na kuuwawa, wamewaweka chini ya uongozi wa adui. Katika wakati ambapo Mayahudi wanachinja ndugu, watoto na wanawake kwa silaha za Marekani na Ulaya, watawala wa eneo hili wanawatumia askari na maafisa wetu kulinda umbile la Kiyahudi na kulinda maslahi ya Magharibi! Hivyo ni kitu gani ambacho umbile la Kiyahudi itakiogopa, ikiwa majeshi ya Waislamu yatakuwa chini ya uongozi wa hawa wakorofi?!

Enyi majeshi ya Waislamu: Ndugu zenu wanauawa huko Gaza na nyinyi mnashirikiana na muuaji wao! Je, mutakaa kimya kuhusu wale ambao wamekutumieni vibaya kuwatumikia maadui wa dini, umma na nchi yenu?! Munawezaje kukubali utawala huu ukabidhi vituo vyenu vya madaraka ambavyo ndio chimbuko la ulinzi wenu bila nyinyi kuwawajibisha?! Munawezaje kukubali kujumuishwa katika muungano huu wa kisaliti?!

Enyi Majeshi ya Waislamu: Leo nyinyi mna machaguo mawili: ima kukaa kimya na kutosheka na yale yanayofuata katika maangamivu na udhalilifu hapa duniani, na aibu na majuto Siku ya Kiyama, au kusonga na kuchukua hatua dhidi ya waharibifu hawa na kuwazuia wasiiburuze nchi kwenye shimo, na kusonga kwa haraka na kwa ufanisi kuwanusuru watu wenu huko Gaza ili kulitokomeza umbile halifu la Kiyahudi.

[وَلَيَنصُرَنَّ اللهُ مَن يَنصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ]

“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Hajj: 40]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu