Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  13 Dhu al-Hijjah 1443 Na: 11 / 1443
M.  Jumanne, 12 Julai 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Miaka 27 baada ya Srebrenica: Msamaha kutoka kwa Serikali ya Uholanzi

 (Imetafsiriwa)

Wakati wa ukumbusho wa kila mwaka wa mauaji ya halaiki huko Srebrenica Waziri wa Ulinzi, Kasja Ollengren aliomba "msamaha wa dhati" kwa niaba ya serikali kwa ndugu wa karibu na manusura wa mauaji ya halaiki huko Srebrenica. Kulingana naye, jumuiya ya kimataifa ilishindwa kulinda eneo la Srebrenica. Uholanzi kama sehemu ya jumuiya hiyo ya kimataifa iliwajibika vilevile kisiasa "kwa hali ambayo hili linaweza kutokea" kama ilivyoelezwa na Ollengren. Waziri huyo alirudia msimamo wa awali wa Uholanzi kwamba jumuiya ya kimataifa na Uholanzi zilishindwa kuwalinda wanaume 8000 Waislamu katikati mwa Ulaya dhidi ya mauaji ya halaiki. Mnamo 2002, Waziri Mkuu wa zamani Wim Kok alisema kutokana na matokeo ya ripoti ya NIOD juu ya dori ya Dutchbat huko Srebrenica, kwamba Uholanzi iliwajibika vilevile lakini haikuwa na makosa katika kadhia hiyo. Tangu wakati huo, tafsiri ya "jukumu sawia" ilibaki bila kubadilika. Yaani, jukumu la pamoja bila matokeo, kama vile kuwajibika kwa makosa yao wenyewe na kufidia jamaa wa karibu ambao waliopoteza jamaa zao wakati wa mauaji hayo ya halaiki.

Kilichobadilika kwa miaka yote hii ni kupunguzwa kwa dhima ya serikali ya Uholanzi kwa mauaji ya halaiki na msimamo upande wa Kikosi cha Uholanzi cha Dutchbat cha UN ambacho chini ya ulinzi wake wanaume wa Kiislamu walikabidhiwa kwa wanamgambo wa Serbia. Mnamo mwaka wa 2014 mahakama ya The Hague iliamua kwamba Uholanzi haikuhusika na vifo vya wanaume zaidi ya 8000 Waislamu, lakini ilihusika tu na kuwafukuza wanaume zaidi ya 300. Kwa maana nyengine, Dutchbat hakuhusika na hatma ya wanaume 7700 Waislamu ambao walichukuliwa na kuuawa. Mnamo mwaka wa 2017 mahakama hiyo hiyo iliamua kwamba uamuzi wa awali, yaani, kwamba serikali inahusika tu kwa vifo vya wanaume 300 Waislamu lakini kwamba uharibifu uliopatikana utafidiwa kwa asilimia 30 pekee. Hii ina maana kwamba dola ya Uholanzi inawajibika tu kwa asilimia 30 ya wahasiriwa ‘pekee’ 300 waliokuwa ndani ya kambi ya kijeshi ya Uholanzi. Wanajeshi wa Dutchbat pia walibaki wazi. Baraza Kuu liliamua miaka miwili baadaye kwamba serikali haiwajibiki kwa asilimia 30 lakini asilimia 10 kuhusiana na ulipaji kwa jamaa wa karibu. Dhima na kosa la serikali ya Uholanzi bado ilipunguzwa tena. Kutoka kwa kuwajibika kwa vifo vya wanaume zaidi ya 8000 na malipo kamili ya jamaa hadi kuwajibika kwa wanaume 300 na fidia ya 10% pekee kwa jamaa wa karibu. Nani anayejua ikiwa dhima hii ya serikali ya Uholanzi itapunguzwa hata zaidi katika siku zijazo.

Waziri Mkuu Mark Rutte pia ameomba msamaha kwa niaba ya serikali kwa wakongwe wa Dutchbat. Alisema kuwa serikali ya Uholanzi inawajibika kwa dhurufu ambazo wakongwe hao walipelekwa na kupokea fidia ya euro 5000 kama "ukosefu wa kutambuliwa na kuthaminiwa". Wakati ndugu wa karibu wa mauaji hayo ya halaiki baada ya miaka 27 bado hawajapata fidia yoyote. Ndugu wengi wa karibu ni wazee ambao baadhi yao tayari wameaga dunia.

Kile ambacho jamaa wa karibu walipokea baada ya miaka 27 ilikuwa ni msamaha kutoka Uholanzi. Endapo tutaupima msamaha huu kwa jinsi serikali ya Uholanzi ilivyoshughulikia hisia zake za uwajibikaji kuhusiana na mauaji hayo ya halaiki, tunaweza kuhitimisha kwamba msamaha huu sio chochote zaidi ya udanganyifu na kofi usoni mwa jamaa wa karibu. Hiki ni kisa chengine ambapo dola ya Magharibi inaonyesha umbile lao halisi na badala ya kuwajibika, wanapuuza sehemu yao katika umwagaji damu. Dola za kirasilimali hazithamini maisha ya mwanadamu, haswa ikiwa yanawahusu Waislamu.

Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu