Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  7 Muharram 1444 Na: 01 / 1444
M.  Ijumaa, 05 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali Sasa Yazitumia Benki Kuwafunga Waislamu Kifedha

(Imetafsiriwa)

NRC Handelsblad ilichapisha makala mnamo tarehe 2 Agosti 2022 ambapo walifichua kwamba benki za Uholanzi zilizuia pasi na haki akaunti za benki za mashirika ya Kiislamu kwa miezi kadhaa. Benki za wateja wa kibinafsi wenye jina la Kiislamu pia zilizuiwa bila ya ilani yoyote.

Inaonekana kana kwamba sasa sera ya benki za Uholanzi ilikuwa sehemu ya kile kinachoitwa kukabiliana na ugaidi wa kifedha. Benki hutumia kila aina ya kanuni ili kufuatilia wale wanaoitwa " wanaowezekana kuwa magaidi" ambao hufanya miamala ya kutiliwa shaka. Akaunti za benki hualamishwa hata hivyo karibu kila mara pesa zinapohamishwa kwa shirika la Kiislamu ambalo hakuna hata tuhmu moja au shtaka dhidi yake.

Kulingana na NRC, benki zinashinikizwa na serikali ya Uholanzi kuongeza kile kinachojulikana kama kukabiliana na ugaidi wa kifedha. Kwa sababu hiyo, misikiti nchini Uholanzi, mashirika ya kujitolea na mashirika mengine yanalengwa kiholela, na kuyazuia kupata rasilimali zao za kifedha. Mashirika kadhaa yaliyoathiriwa yanaeleza jinsi benki zilishindwa kutaja ni kwa nini zilizuiwa kutokana na akaunti zao za benki hadi zilipopokea barua inayosema kwamba yalishukiwa kufadhili ugaidi. Kando na hayo, wale walioathiriwa, wanapaswa kujibu maswali kadhaa yasiyo ya lazima na ya kina kuhusu miamala, hata kama miamala hiyo inayosemwa ilikuwa kidogo kama euro 2.50. Serikali na benki hazioni aibu kuuliza, wakati wa mchakato huu, maswali kadhaa ya kudhalilisha na kumlazimisha Muislamu kutoa ushirikiano ili kuweza tena kuifikia akaunti yake ya benki.

Kufuatilia miamala ya kifedha kwa kisingizio cha kukabiliana na ugaidi wa kifedha kwa kweli ni kusaka visingizio dhidi jamii ya Waislamu na mashirika yake. Serikali inajua vyema kwamba mabilioni ya miamala hufanywa kila mwaka na hilo haliwezekani kivitendo kwa serikali wala benki kutofautisha ni miamala gani kati ya hii inakusudiwa kwa mashirika hayo yanayochukuliwa kuwa ya kigaidi. Kwa maana nyengine, pamoja na kwamba serikali inajua kuwa gaidi wa kifedha hapatikaniki, bado serikali inazishinikiza benki kupekua rekodi za wateja wao kutafuta wale wenye jina la ukoo la Kiislamu au miamala kwa mashirika ya Kiislamu.

Kwa mara nyingine tena, mfumo wa Kirasilimali umedhihirisha umbile lake halisi. Ule unaoitwa uhuru wa kibinafsi na uhuru wa kumiliki ni kauli mbiu tupu za kupumbaza umma tu. Akaunti za benki za Waislamu zinapatilizwa kuzuiwa bila ushahidi wowote na bila shtaka madhubuti haliwezi kupigwa vita mahakamani. Ukweli ni, Waislamu wanawindwa kifedha wanapolipa zakat, sadaqa, fidya au kafara kwa shirika ambalo serikali hailipendi.

Ni katika Dola ya Khilafah pekee, ambapo kila raia ana haki ya kulindwa dhidi ya dhulma. Mali ya kibinafsi ya raia sio njia ya kupigana vita vya itikadi ya kisiasa dhidi ya raia wake. Katika dola ya Khilafah, kanuni ya kutokuwa na hatia hadi athibitishwe kuwa na hatia daima inafanya kazi. Katika dola ya kisekula, raia ni mwe nye hatia hadi ithibitishwe kuwa hana hatia. Hili si chochote ila ni ukandamizaji na matumizi mabaya ya mamlaka.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu