Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  29 Muharram 1444 Na: 02 / 1444
M.  Jumamosi, 27 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sera ya Wakimbizi ya Uholanzi kwa Mtazamo Tofauti

(Imetafsiriwa)

Kwa muda wa miezi kadhaa kuna uhaba wa kimuundo wa makaazi ya wakimbizi, uliosababisha mamia ya wakimbizi kuishi katika mazingira ya kinyama ambapo wanalazimika kuishi nje, bila chakula cha kutosha, vinywaji na huduma za usafi. Hivi majuzi, hata mtoto mchanga wa miezi mitatu alikufa. Ingawa haijulikani jinsi mtoto huyo alivyokufa, ukweli unabaki kuwa hali ya maisha katika makazi ni duni. Hakuna matarajio ya tatizo hili kutatuliwa katika siku zijazo. Hata Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) walikuja kusaidia kwa sababu walihitimisha kuwa hali katika kituo cha maombi cha Ter Apel ni mbaya sana kwamba watatoa msaada wa matibabu na kisaikolojia kwa wakimbizi. Ukweli kwamba shirika la misaada linalotoa msaada wa dharura katika maeneo yenye mizozo, kama vile majanga ya kimaumbile au mikurupuko ya magonjwa hatari, ni doa kwenye sera ya wakimbizi ya Uholanzi. Kama Judith Sargentini, mkurugenzi wa MSF Uholanzi alivyotoa mukhtasari, “Hili si janga la wakimbizi, ni janga la kisera.”

Kuna mgogoro wa sera ambao haujidhihirishi tu katika ngazi ya mitaa, lakini zaidi katika ngazi ya kitaifa, kwa kuwa ni ngazi ya kitaifa ndiyo iliyo na jukumu la kusimamia ipasavyo sera ya uhamiaji na wakimbizi. Sera hii ni rahisi; kabiliana na mtiririko wa wakimbizi, punguza  makaazi na toa hamu ya kuja Uholanzi, isipokuwa kwa ndugu zao wa Ukraine. Uholanzi inadumisha sera ya kupunguza idadi ya makaazi, bajeti ya kuwahifadhi wakimbizi na kupunguza idadi ya wafanyikazi. Endapo tutalinganisha hili na ulisia ulioko Ulaya na duniani kote, mizozo na migogoro mingi inatokea ambayo huendelea kuleta mtiririko wa wakimbizi kuliko mtu anavyoweza kusema sera hii itashindwa. Ni kana kwamba mtu anajaribu kupiga mbizi ndani ya maji bila kulowa. Kuukataa uhalisia huu, au kutamani Uholanzi isiyo na wakimbizi hakutabadilisha ulisia wa janga la wakimbizi.

Siasa hizi zisizoona mbali ambazo kwazo ulisia unakataliwa pia zinaweza kuonekana katika nyanja zengine za mgogoro wa wahamiaji na wakimbizi, na hiyo ndiyo hisa ya Uholanzi na nchi zengine za magharibi katika mgogoro wa sasa wa wakimbizi. Hili halijajadiliwa kwa kina wakati miungano mingi ya kijeshi ya magharibi ambayo Uholanzi inashiriki ilikuwa dhidi ya nchi ambazo sehemu kubwa ya mtiririko wa wakimbizi hutoka. Fikiria Afghanistan, Iraq, Syria, Somalia na Mali. Miundombinu ya nchi hizi zote ilipigwa risasi vipande vipande na maisha yakafanya kutowezekana ikiwalazimisha watu kukimbia na kutafuta maeneo salama ambayo yatawapa wao na familia zao matarajio zaidi ya mustakbali. Hii inafanya Uholanzi na nchi zingine za magharibi kuwa washirika wa mtiririko mkubwa wa wakimbizi.

Swali jengine muhimu katika suala la uhamiaji na wakimbizi ni kutazama kimya kimya jinsi washirika wa magharibi kama vile Marekani, Ufaransa na Uingereza wanavyotekeleza malengo yao ya kikoloni na kusababisha vifo na uharibifu katika nchi za Afrika. Kwa kupindua serikali mara kwa mara, kuwafanya watu kugeukiana wao kwa wao ili tu kumakinisha utawala wao na kupandikiza viongozi wafisadi ambao watalinda maslahi yao ya kiuchumi na kisiasa. Hili huleta mfumo mbovu wenye uongozi fisadi usiotumikia umma bali maslahi yao wenyewe. Hili husababisha mazingira ya kuzalisha ufisadi, upendeleo wa kikabila, kukata tamaa na ukosefu wa matarajio ya mustakbali, na kusababisha watu kutafuta ustawi na ufanisi wao kwengine.

Mgogoro wa wakimbizi ni matokeo yasiyo epukika ya sera ya kigeni ya kibepari ya magharibi na uingiliaji kati wake, uvurugaji na matarajio ya kikoloni katika nchi hizi. Sera ya uhamiaji na wakimbizi ya Uholanzi pia imeundwa kwa maono haya ya kibepari na sera ya kikoloni. Kuwahifadhi wakimbizi hakutazamwi kutoka upande wa utu wa binadamu bali kama uovu wa lazima, mkimbizi anatazamwa kama tishio la kihakika. Hivyo basi, baraza la mawaziri limeamua kulishughulikia suala la kuhifadhi wakimbizi kupitia timu ya shirika la majanga ya kitaifa ambayo inaratibiwa na Mratibu wa Kitaifa wa Usalama na Kupambana na Ugaidi (NCTV). Karibu nchini Uholanzi!

Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu