Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  21 Rabi' I 1444 Na: 04 / 1444
M.  Jumatatu, 17 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Barua ya Mwaliko kutoka kwa Manispaa ya Amsterdam: Sera Dhahiri ya Uoanishaji!

(Imetafsiriwa)

Manispaa ya Amsterdam imealika bodi kadhaa za misikiti kutia saini taarifa ya kuunga mkono ambapo misikiti inalaani ghasia na ubaguzi dhidi ya jamii ya LGBTQ+. Barua hii ya Amsterdam kutoka kwa Meya Femke Halsema kwenda kwa ‘bodi zote za misikiti jijini’, ilikuja kujulikana baada ya Lody van de Kamp, rabbi (mwanachuoni wa Kiyahudi), kueleza hadharani ukosoaji wake dhidi ya kitendo hiki cha kibaguzi katika safu yake.

Hii imesababisha msururu wa ukosoaji kutoka kwa bodi za misikiti wiki iliyopita ambapo ilimlazimu Meya Femke Halsema kufutilia mbali mkutano ambao ulipangwa mnamo Jumatano, tarehe 19 Oktoba. Safu na majibu ya bodi chache za misikiti yaliyofuata yanaonekana kuwa na athari za kuzuia usimamizi wa unyanyapaa kutoka kwa manispaa ya Amsterdam. Tukiangalia nyuma kuhusu hili tungependa kukushirikisha pointi chache.

Halsema anadai kuwa hakuna ubaguzi na kwamba mashirika mengine yatafikiwa vilevile. Lakini, hakuna hilo kwa sasa. Ukweli unabaki kuwa ombi hili liliwekwa kwa misikiti pekee na sio kwa mashirika mengine (ya kidini). Hata kama kuyafikia mashirika mengine ni jambo ambalo wanapanga kufanya, swali linabaki kwa nini misikiti inapewa kipaumbele.

Hata zaidi, kwanza ni nini misikiti inaalikwa? Je, misikiti ina uhusiano gani na vurugu dhidi ya jumuiya ya LGBTQ+? Kwa kualika misikiti kutia saini taarifa ya pamoja, manispaa ya Amsterdam inauhusisha Uislamu na vurugu dhidi ya jumuiya ya LGBTQ+. Na kwa kualika misikiti pekee, ukiritimba wa vurugu pia unawekwa kwa jamii ya Kiislamu. Wakati manispaa ya Amsterdam bila shaka inajua kwamba misikiti haihubiri vurugu, kwa nini basi imewekwa juu ya vurugu hizo?

Ingawa, taarifa ya uungwaji mkono inasisitiza kipengee cha unyanyasaji dhidi ya jumuiya ya LGBTQ+, ujumbe wa kweli ni kwamba misikiti inapaswa kuchukua msimamo kuhusu ubaguzi dhidi ya jumuiya ya LGBTQ+. Ikiwekwa tofauti, manispaa inaitaka misikiti kuhalalisha mtindo wa maisha wa LGBTQ+ ndani ya jamii ya Waislamu.

Hili linahusisha kwamba wahubiri au Muislamu wa kawaida wasiwezi kuelezea kwa kukosoa au vibaya kuhusu LGBTQ+, kwa sababu itachukuliwa kuwa ni ubaguzi.

Pia, propaganda kali za LGBTQ+ za serikali ya Uholanzi hazikataliwa na Waislamu pekee bali na makundi mengine mengi yasiyo ya Kiislamu katika mujtamaa.

Licha ya hayo, wanaendelea kuwanyooshea kidole cha lawama Waislamu. Tofauti pekee kati yao na jamii ya Kiislamu ni kwamba kukataliwa kwa LGBTQ+ kunafanywa kwa sababu za Kiislamu badala ya mazingatio ya kimila au hata ya kidini ambayo yamepachikwa usekula. Hili linathibitisha vita vinavyopiganwa dhidi ya Uislamu na ajenda ya kisiasa ya kuingiza usekula jamii ya Waislamu; unaruhusiwa kuwa Muislamu, lakini tu kwa mujibu wa ufahamu wa fikra ya kisekula pekee.

Ajenda ya jiji la Amsterdam haijatenganishwa na sera ya kitaifa ya uoanishaji ambayo inatekelezwa kwa miaka mingi dhidi ya Waislamu na kwa ajili ya kukubaliwa kwa jumuiya ya LGBTQ+. Lengo la sera hii ya uoanishaji ni kwamba Waislamu waivae fikra ya kisekula na kuuelekea Uislamu kwa mtazamo wa kisekula.

Licha ya ususiaji wa misikiti mingi, msemaji wa Halsema alisema kwamba hatimaye ‘chache’ kati ya takriban nyumba sitini za ibada za Kiislamu jijini Amsterdam zilikuwa tayari kuja. Swali ni je, misikiti mingapi ingekuja lau tangazo la kuungwa mkono lisingepokea ukosoaji kama huo wa umma? Uhalisia ni kwamba manispaa, polisi, haki na misikiti huwasiliana na huwa na mazungumzo ya mara kwa mara juu ya masuala haya na katika baadhi ya matukio, hata wameshiriki katika mipango ya ushirikiano (ikiwa ni pamoja na mipango yenye utata ya misimamo mikali).

Uwezo wa uhusiano huu usio na usawa unaonyeshwa kama ifuatavyo. Sera ya upinde wa mvua ya Amsterdam ya 2019-2022 inasema kwa mfano: "Tutaongeza mtazamo wetu juu ya kukubalika ndani ya kikundi lengwa cha LGBTIQ+ chenyewe cha tamaduni-mbili" na: "Tutachochea uwepo wa watu wa kuigwa wanaoonekana kupitia maeneo yanayofikika, kama vile vituo vya jamii, misikiti na vituo vya kitamaduni.” Misikiti imeelezwa hapa kana kwamba ni mali binafsi za manispaa ambayo inaweza kuitumia kufikia malengo yao.

Kwa hivyo, inasema katika barua ya mwaliko kwamba manispaa ya Amsterdam inahutubia bodi za misikiti kwa yafuatayo: "Mkutano huu ni ufuatiliaji wa mkutano wa tarehe 9 Mei 2022 wa wanachama wa Triangle na wajumbe wa bodi ya misikiti ya Amsterdam katika Msikiti wa Taqwa. Wakati wa mkutano huo tulijadili ulinzi wa jumuiya ya LGTIQ+ na kuhusu mchango ambao misikiti inaweza kutoa ili kuimarisha usalama wa kundi hili. Meya anapenda kujadiliana na bodi za misikiti jinsi ya kulitilia mkazo zaidi suala hili."

Hii inaonyesha kwamba miradi kama vile taarifa ya uungaji mkono LGBTQ+ haikuja kwa ghafla au kuwasilishwa ndani ya ombwe. Msemaji wa Halsema anaitaja kama "mchakato tete", ambayo inamaanisha kuwa mwaliko wa mkutano haungeweza kuwa wa ghafla.

Msemaji huyo pia anaeleza kuwa wazo la tamko hilo la kuunga mkono linatokana na mikutano ya mara kwa mara na bodi za misikiti na polisi, haki na meya. Miezi kadhaa iliyopita kulikuwa na majadiliano juu ya taarifa ambayo jumuiya zote za kidini katika jiji hili zingepaswa kuunga mkono. "Bodi za misikiti hapo awali zilitaka kufikia wazo la pamoja kwanza kabla ya kuzifikia dini zengine. Kwa hiyo, wao walipokea mwaliko kwanza.”

Hii ni sababu mojawapo inayoifanya jamii ya Kiislamu kuwa macho na kukosoa uhusiano uliopo kati ya bodi ya msikiti wao na serikali. Bodi za misikiti zinapaswa kuwa wazi na macho ili zisitumike na serikali kwa sera ya uoanishaji.

Msimamo wa pamoja ambao bodi za misikiti wameuchukua umeonyesha kuwa kile tunachowalingania kwacho Waislamu ni nguvu. Tunapaswa kudumisha hili na kusukuma kwa njia ya kimfumo na muundo.

Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu