Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  25 Rabi' II 1444 Na: 07 / 1444
M.  Jumamosi, 19 Novemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Muamala kwa Shule za Qur'an:

Kwa Mara Nyengine Tena ni Dhihirisho la Sera dhidi ya Uislamu

(Imetafsiriwa)

Serikali imekubali mpango ambao Waziri wa Elimu Dennis Wiersma anataka kuutekeleza kwa shule za Qur'an, shule za wikendi na maeneo mengine ambayo 'elimu isiyo rasmi' inatolewa. Ufafanuzi kutoka kwa Wizara wa mpango huu wa kibaguzi ambao kwao Waislamu wanatengwa ni kwamba ndani ya elimu isiyo rasmi kumekuwa na kesi zinazodaiwa za shughuli ambazo 'zinapinga na uoanishaji, zinapinga demokrasia dhidi ya utawala wa sheria.'

Mpango kazi wa serikali ya Uholanzi wa kuingilia elimu rasmi ya kidini na nyanja ya kibinafsi ya Waislamu unaonyesha kwamba tuko katika hatua ya juu zaidi ya siasa za uoanishaji. Baada ya shule rasmi zilizo na sura ya Kiislamu kama Ibn Ghaldoun huko Rotterdam, Cornelius Haga Lyceum huko Amsterdam na Shule za Kiislamu za As-Siddieq kuamiliwa vikali, wakati sasa umewadia kwa taasisi zisizo rasmi za elimu ya Qur'an.

Ishara ya kuanzia kukabiliana na elimu isiyo rasmi ya Kiislamu katika shule za Qur'an Misikitini na ndani ya majumba ilitolewa miaka michache iliyopita wakati Idara ya Upelelezi na Usalama (AIVD) ilipoonya katika ripoti yake ya kila mwaka dhidi ya 'wahubiri wa Kiislamu wenye itikadi kali' na ushawishi wao kwa watoto wa Kiislamu wanaofuata masomo ya Kiarabu au elimu ya Qur’an. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, shughuli za baada ya shule au za ziada katika misikiti au vituo vya jumuiya ni mazingira yaliyo na uwezo wa kuzalisha  'fikra ya jihad' ambayo kwayo watoto wanalelewa kuwa magaidi watarajiwa, alisema Dick Schoof, Mkurugenzi Mkuu wa AIVD.

Ndio, umeisoma kwa usahihi, watoto wa Kiislamu wanaojifunza kusoma Quran wanawekwa katika kundi la magaidi watarajiwa! Serikali inafuata msururu huu wa fikra na kuzionyesha shule za Qur'an kuwa tishio. Kwa kufanya hivyo, elimu ya Kiislamu, kwa ubaguzi mno, inafanywa kuwa hatari. Hivyo basi, serikali hutumia maneno makali na ya kibaguzi inapozungumzia Uislamu na masuala ya umma wa Kiislamu kwani inatumia misamiati kama vile: ‘kupinga uoanishaji, kupinga demokrasia dhidi ya utawala wa sheria.’ Hivyo kusawazisha hatari na upingaji wa uoanishaji na upingaji demokrasia .

Wakati kuwa pinzani na uoanishaji na kuwa pinzani na demokrasia hakuna uhusiano wowote na hatari au kuhujumu jamii. Mtu anaweza kuwa dhidi ya uoanishwaji/umezwaji kwa sababu anataka kudumisha kitambulisho chake mwenyewe na hakinaiki na misingi ya mafundisho ya kidemokrasia bila kuleta tishio. Zaidi ya hayo, kuhifadhi kitambulisho na imani katika mfumo inahusiana na mawazo na ukinaifu. Haya kamwe hayawezi kulazimishwa. Kimsingi, wanafanya uoanishji na kukumbatia njia ya kufikiri ya kidemokrasia, kama sharti la kuishi pamoja. Basi kuna haja gani ya kuwepo ule unaoitwa uhuru wa kuzungumza, uhuru wa elimu na dini, ikiwa mtu hawakubali wale wanaofikiri tofauti na kumlazimisha kubadilika?

Lengo la propaganda hii ni kujaribu kubadilisha fikra za Waislamu. Njia mojawapo inayotumiwa na serikali ni kuwasilisha fikra ambazo Waislamu wana uhuru wa kufikiri. Kwa mfano, dhana kwamba kushikilia mitazamo inayopinga uoanishaji na kupinga demokrasia ni sawa na hatari na kutotaka kuishi kwa pamoja. Huu ni uongo kabisa. Kwa hiyo tunapaswa kulijadili suala hili kwa njia sahihi kwa kulaani uwongo wa dhana hii, kupitia kukataa kuikubali mipaka waliyotuwekea. Sisi kama jamii ya Kiislamu tunapaswa kuwa macho na njia za ujanja za sera ya uoanishaji. Kudumisha kitambulisho chetu na ukinaifu wetu inamaanisha kwamba tunapaswa kuchukua msimamo thabiti, bila kujali kile wanachofikiria kama Waislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu