Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  9 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: 10 / 1443
M.  Jumatano, 08 Juni 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waislamu nchini India Wasimama kwa ajili ya Heshima ya Mtume (saw)

(Imetafsiriwa)

Msemaji wa Chama cha Bharatiya Janata cha India (BJP), Nupur Sharma alitoa matamshi ya matusi kuhusu Uislamu na juu ya Mtume (saw) na mkewe (ra) wakati wa mjadala wa televisheni. Baadaye mkuu wa idara ya habari ya Delhi, Naveen Kumar Jindal alichapisha tweet ya matusi kuhusu Mtume (saw). Kutokana na hali hiyo, Dola kadhaa za Ghuba na nchi nyingine za Kiislamu zililaani matamshi hayo ya matusi na baadhi yao walimwita balozi wao wa India na kuitisha misamaha. Hii ilisababisha kusimamishwa kazi kwa wasemaji wawili na kufuatiwa na msamaha.

Maandamano ya nchi za Kiislamu yanaonyesha kuwa jibu haliwezi kupuuzwa nchini India. Kwa kuwa India, kama nchi zengine zote, ni ya kisasa na inaendeshwa na maslahi ya kibinafsi. India ilichagua chini ya shinikizo fulani kushikilia maslahi yake ya kiuchumi na mengine ambayo inayo na nchi hizi na ililazimika kurudi nyuma. Kwa hivyo hili lilionekana kimataifa.

Nchini India, tangu ilipoingia madarakani mwaka 2014, BJP imeanzisha vita dhidi ya Uislamu na Waislamu, matusi ya hivi karibuni dhidi ya Mtume (saw) ni dhihirisho la hilo. Kuna ukandamizaji wa kinidhamu kwa jamii ya Kiislamu. Wafuasi wa BJP wanaojiona kama watetezi wanaojitangaza wa Ubaniani hutoa wito waziwazi wa kuchomwa kwa Waislamu wasio na hatia, bila kufunguliwa mashtaka. Waislamu hushambuliwa mara kwa mara na makundi ya Mabaniani. Wakati mwengine uchokozi unafanywa tu kwa kuonyesha muonekano wao wa Kiislamu.

Licha ya ukandamizaji wa kinidhamu wa Waislamu na BJP, nchi za Kiislamu zimedumisha uhusiano mzuri na India. Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, baniani mwenye msimamo mkali wa BJP, mara kwa mara amezizuru tangu aingie mamlakani mwaka wa 2014. Mahusiano ya kirafiki ya kibiashara na Dola zenye utajiri wa kawi za Ghuba yaliimarika wakati wa muhula wake.

Ikiwa shutma au ukosoaji mdogo tu wa nchi za Kiislamu unaweza kuwa na ushawishi katika jinsi India inavyoamiliana na Waislamu, kwa nini hili halikutumika mapema wakati Uislamu na Waislamu waliposhambuliwa. Kwa nini kuguswa sasa? Je, wametoa matakwa madhubuti dhidi ya serikali ya BJP yenye chuki dhidi ya Uislamu kuwalazimisha kuwatendea Waislamu haki kwa badali ya mahusiano ya kibiashara? Walifanya kinyume chake; Narendra Modi hata alipokea tuzo za juu zaidi za kiraia kutoka kwa serikali za Saudi Arabia mnamo 2016 na Imarati na Bahrain mnamo 2019.

Kwa hivyo kwa nini nchi hizi, zilizomtunuku Baniani mwenye msimamo mkali kwa mapambo na uhusiano wa kirafiki licha ya kampeni yake ya kupinga Uislamu, zinasimama kwa pamoja sasa?

Ilikuwa ni kwa sababu ya maandamano ya kishujaa ya Waislamu nchini India ambao walihatarisha maisha yao kwa kuingia mabarabarani na kulaani matamshi ya matusi ya Mtume (saw) ambayo hatimaye yalienea mitandaoni, ikiwemo katika nchi za Kiislamu. Hili liliwafanya viongozi wa nchi za Kiislamu kukumbwa na kutoridhika kunako ongezeka ndani ya Ummah na kuwalazimisha kubeba hisia zao na kuwapa wazo kwamba wao pia walikuwa wanasimama dhidi yao vilevile.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu