Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  1 Rajab 1444 Na: 09 / 1444
M.  Jumatatu, 23 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uchomaji Quran ni Kielelezo cha Sera ya miaka Mingi dhidi ya Uislamu

(Imetafsiriwa)

Kiongozi wa kundi linalopinga Uislamu la Pegida alirarua, akakanyaga na kuchoma moto Quran Tukufu wakati wa maandamano nje ya bunge la Uholanzi. Ukatili wote huu ulifanyika kwa idhini ya meya wa The Hague na chini ya uangalizi na ulinzi wa polisi. Swali ni je hili tunapaswa kulionaje? Je, hii ni hatua ya mtu mmoja mpumbavu au kuna zaidi yake? Na tufanye nini?

Ni vyema kutambua kwamba vitendo hivyo vya kuudhi sana na vya kipumbavu vimezidi kuwa vya kawaida katika nchi za Magharibi. Haya ni baadhi ya matukio ya hivi karibuni ili kutoa wazo la jambo hilo:

Wiki iliyopita, Quran Tukufu ililengwa na chama cha mrengo wa kulia cha Denmark-Swedish kinachopinga Uislamu, Stram Kurs ('Njia Imara'). Quran Tukufu ilichomwa moto wakati wa maandamano nchini Uswidi.

Mnamo mwaka wa 2022, nchini Norway wakati wa maandamano ya kundi la itikadi kali la SIAN, ambalo linasimama kukomesha usilimishaji wa Norway, Quran Tukufu ilichomwa moto.

Mnamo mwaka wa 2020, Quran Tukufu ilinajisiwa hadharani katika nchi mbalimbali za Skandinavia kwa kuipasua, kuitemea mate na kuipiga teke.

Mnamo mwaka wa 2018, Macron hata alikuwa na ujasiri wa kuchapisha ilani ambayo ilitiwa saini na wasomi na wanasiasa mashuhuri 300, akiwemo yeye mwenyewe, ambapo alitoa hoja kwamba Qur'an Tukufu inachochea vurugu na kwamba aya za Qur'an Tukufu zinapaswa kuondolewa.

Mashambulizi haya yote ya kidhahiri juu ya Qur'an Tukufu yalifanyika kwa idhini ya mamlaka na chini ya usindikizaji wa polisi. Waziri Mkuu wa Norway alitetea haki ya waandamanaji ya kuinajisi Quran, na leo mamlaka za Uswidi na meya wa The Hague wanatetea haki ya kuandamana dhidi ya Uislamu na kuinajisi Quran. Itakuwa ni ujinga kudhani kwamba mashambulizi dhidi ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu yanaweza kuhusishwa tu na watu wachache wapumbavu, kwani aina hizi za vitendo vya kuudhi vinaweza kutendeka kwa idhini na msaada wa walio mamlakani. Zaidi ya hayo, hisia za chuki dhidi ya Uislamu zimeweza kustawi katika mazingira yaliyoanzishwa na sera za miongo kadhaa za nchi za Magharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Mashambulizi dhidi ya Uislamu na Qur'an Tukufu kwa hiyo hayatakoma. Na kwa hivyo, lazima tuzifanye sauti zetu zisikike juu na wazi. Iwapo sisi kama waumini hatutasimama kukitetea Kitabu cha Mwenyezi Mungu tunachokiona kuwa ni Uongofu wa Mwisho kwa wanadamu, Neno la Mwenyezi Mungu, kitenganishi baina ya haki na batili, nani atafanya hivyo? Kukaa kimya sio chaguo!

Kusimama kwa ajili ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu si tu ni faradhi ya kidini bali pia ni haja ya lazima kwa sababu tabia ya kutulia na kukaa kimya itawashajiisha tu maadui wa Uislamu na kuwapa motisha kuendelea.

Kwa hiyo ni lazima tunyanyuke kwa wingi na kutumia njia zote za kistaarabu na zinazoruhusiwa ili kuweka wazi kwamba tutasimama daima kwa ajili ya Uislamu na matukufu ya Uislamu. Hili litatuma ishara ya wazi na isiyo na shaka ya wapi mipaka yetu ya kuvumiliana iko, na wakati huo huo kutoa ushahidi kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwamba sisi ni waumini na wafuasi stahiki wa Kitabu Chake.

Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu