Afisi ya Habari
Uingereza
H. 8 Rajab 1441 | Na: 1441 H / 27 |
M. Jumanne, 03 Machi 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wahamiaji Nchini Ugiriki Wamefichua Uhalisia Uliooza wa Utaifa
Mipaka ya kizalendo ambayo inapigiwa debe na kulindwa na serikali za kirasilimali inapelekea mateso makubwa sana kwa watu. Kama si mipaka ya Wamagharibi, watu wasingeli gawanyika kiasi hiki cha kutisha, ambacho mtu mmoja anazaliwa upande wenye neema na mwingine anazaliwa eneo ambalo limezungukwa na ufukara na anakufa kutokana na njaa.
Kile kinachoitwa “janga la uhamiaji” ambalo Ulaya wanakumbana nalo dalili za ubaya wa maradhi haya ya utaifa, wakati ambapo mashua iliyobeba wahamiaji ikijumuisha wanawake na watoto inarudishwa katika bahari huku wakinyimwa maji ya kunywa eti kuwapa maji ya kunywa ni kuwaruhusu kutumia sehemu ya utajiri au fadhila za nchi husika. Hali mbaya kama hii inafanyika wazi katika kisiwa cha Ugirirki kiitwacho Lesbos, kama inavyotokea wazi na kushuhudiwa katika maeneo ya pwani za Ulaya muda huu.
Tabia hii ni tunda la usekula, ambao umejifunga na mgawanyo wa uongo wa kitaifa kati ya watu, na tangu muda huo dunia inaendelea kutaabika kutokana na hatua hiyo. Inakuwaje mpaka mdogo upelekee chuki kiasi hicho kwa binadamu wenzako? Na wengine katika wahamiaji hao hufanyiwa matendo ya kutisha na magenge ya wahuni kwa visingizio vya itikadi kali. Lakini bado wameshindwa kutambua kwamba hasira na chuki zao zimezaliwa kutokana na imani ya kwamba wanavyofanya ni sawa kwani wanalinda fadhila walizopewa na mpaka. Imani hii hii imebebwa na w wale wanaoshutumu na wanaoshutumiwa. Baadhi hawapendi kuona unyama huu ukifanywa mbele yao, lakini wameendelea kuukumbatia ubabe wa urasilimali ambao unaifanya sehemu kubwa ya dunia kuwa masikini na utumwani.
Kwa kuongezea, vita na mazingira magumu ya maisha ambayo wahamiaji wanayakimbia yamesababishwa moja kwa moja na serikali hizi za kirasilimali ili kuwalipa fadhila wale wanaishi upande wa pili wa mpaka wa Ulaya. Sasa hasira zinatoka wapi ikiwa hao wanaokuja wanakuja kutumia pamoja kile ambacho kilichukiliwa kidhulma kutoka kwao?
Fikra ya utaifa ni fikra iliyooza iliyobebwa na nidhamu iliyoko sasa ya kisekula na haina nafasi kwa binadamu wenye akili timamu. Uislamu hauruhusu mgawanyo wa kijinga kiasi hicho, kama kwani Mtume (saw) alisema,
«دَعُوهَا فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ»
“Achana nao, umeoza.”.
Muda umefika sasa kwa Waislamu kuufichua utaifa na namna unavyosababisha kuwatendea binadamu wenzako madharau.
Yahya Nisbet
Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Uingereza
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uingereza |
Address & Website Tel: +44 (0) 7074 192400 www.hizb.org.uk |
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk |