Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  23 Rajab 1441 Na: 1441 H / 20
M.  Jumatano, 18 Machi 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuzuia Kuenea Kwa Virusi vya Korona ni Jukumu la Kisheria

Kujibu janga la virusi vya korona inahitaji nidhamu kamili ya utunzaji inayofanyakazi katika ngazi zote, ambapo ustawi wa watu wote ndio jambo la msingi. Njia ya maisha ya Kiislamu imeandaliwa vizuri kutunza mambo ya watu, na imani na maadili yake, na nidhamu ambazo zimejengwa juu yao.

Mtume wa mwisho aliyetumwa kwa wanadamu, Muhammad (saw) ameripotiwa kusema:

«أَلاَ كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ فَالأَمِيرُ الَّذِى عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُمْ وَالْمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى بَيْتِ بَعْلِهَا وَوَلَدِهِ وَهِىَ مَسْئُولَةٌ عَنْهُمْ وَالْعَبْدُ رَاعٍ عَلَى مَالِ سَيِّدِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُ أَلاَ فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»

“Kila mmoja wenu ni mlinzi na kila mmoja anajukumu kwa anaowasimamia, Imamu ambaye ni kiongozi wa watu ni anajukumu kwa usimamizi wake, na mwanamume anajukumu kwa watu wa nyumba yake na anahesabiwa kuhusiana nao, na mwanamke anajukumu kwa nyumba ya mumewe na watoto wake na anahesabiwa juu yao, na mtumwa anajukumu juu ya mali ya bwana wake na anahesabiwa juu ya mali hiyo, na kila mmoja wenu ni mlinzi na kila mmoja wenu anahesabiwa kuhusu jukumu lake.”

Ummah wa Waislamu, ambao utatolea ushahidi wanadamu wote siku ya kiyama, unajukumu la kishera kusaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu na kila mtu anapaswa kuwekeza juhudi zake kuelekea upande huo.

Kila mtu anapaswa kuchukua kwa umakini ushauri wa wataalamu ambao wanalenga kukomesha kuenea kwa ugonjwa huo, kutenda ipasavyo, ili janga hilo lisiingie kila nyumba likawacha mateso mengi, Mwenyezi Mungu atuepushie.

Kwa hivyo tunapaswa kuyachukua mambo yafuatayo kwa mazingatio ya umakini:

1. Udharura wa kufuata muongozo wa usafi wa mazingira, kama vile kunawa mikono mara kwa mara na kwa makini, kutogusa uso, mdomo au macho bila kunawa, na kukaa mbali na wagonjwa au wale ambao wana dalili za ugonjwa, kama vile kukohoa au kiwango cha juu cha joto.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alishauri: «لاَ تُورِدُوا المُمْرِضَ عَلَى المُصِحِّ» “Musiweke mgonjwa pamoja na wazima” na «فِرَّ مِنَ الْمَجْذُومِ فِرَارَكَ مِنَ الْأَسَدِ» “Mkimbie mwenye ukoma kama vile unavyomkimbia simba.”

2. Kukaa nyumbani kadri mtu anavyoweza, haswa kwa watoto, wazee na wale wenye matatizo ya kiafya. Wale ambao lazima watoke kwa ajili ya kazi wanapaswa kufuata utaratibu wa kujitenga na usafi wa mazingira kuzuia kuenea au kupata ugonjwa. Mikono inapaswa kuoshwa vizuri kabisa kabla ya kuchanganyikana na familia, ili usiwaambukize.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) pia alisema: «لَا ضَرَرَ وَلَا ضِرَارَ» “Lazima kusiwe na madhara wala kudhuriana.”

3. Jiweke mbali na mikusanyiko iwezakanavyo, kufuta matukio yote ambayo yanaweza  kufutika.

4. Epuka mgusano wa karibu kama kubusu na kupeana mikono iwezekanavyo.

5. Wale ambao wana ugonjwa au dalili zake lazima wawekwe karantini na lazima wafuate hilo.

6. Kutosafiri bila ya dharura na kuchukua tahadhari zote ikiwa ni lazima.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:

«إِذَا سَمِعْتُمْ بِالطَّاعُونِ بِأَرْضٍ فَلاَ تَدْخُلُوهَا، وَإِذَا وَقَعَ بِأَرْضٍ وَأَنْتُمْ بِهَا فَلاَ تَخْرُجُوا مِنْهَا» “Mutakaposikia kuhusu tauni katika ardhi, basi musiingie katika ardhi hiyo; na ikiwa uko katika ardhi na ikaingia tauni, basi musitoke katika ardhi hiyo.”

Aisha (ra) aliuliza kuhusu tauni, kwa hivyo Mtume (saw) akamwambia:

«أَنَّهُ كَانَ عَذَابًا يَبْعَثُهُ اللَّهُ عَلَى مَنْ يَشَاءُ، فَجَعَلَهُ اللَّهُ رَحْمَةً لِلْمُؤْمِنِينَ، فَلَيْسَ مِنْ عَبْدٍ يَقَعُ الطَّاعُونُ، فَيَمْكُثُ فِي بَلَدِهِ صَابِرًا، يَعْلَمُ أَنَّهُ لَنْ يُصِيبَهُ إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَهُ، إِلَّا كَانَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ الشَّهِيدِ»

“Ilikuwa ni adhabu ambayo Mwenyezi Mungu anawatumia wale awatakao. Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa ni huruma kwa waumini; kwa kuwa hakuna mja anayekutana na tauni, lakini akakaa na kuvumilia katika ardhi yake, akijua kuwa hakuna kitakachomkuta isipokuwa kile ambacho Mwenyezi Mungu amekiandika, isipokuwa atapata thawabu kama zile za shahidi.”

7. Epuka kueneza uvumi na ripoti zisizotegemewa za habari zinazopelekea hofu na matokeo mabaya.

8. Wale wenye uzoefu na uwezo wanapaswa kuwa tayari kutoa msaada kwa wale wanaohitaji.

Ummah wa Waislamu, wakati wa kukabili janga hili, unalikabili kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na kuchukua tahadhari zinazohitajika, kujihami kwa kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, kumtegemea Yeye, kutafuta msamaha Wake, na fahamu za Aqeedah ya Kiislamu ambazo humpa utulivu muumini wakati anapokabiliwa na Amri ya Mwenyezi Mungu. Ugonjwa ni Amri ya Mwenyezi Mungu kuzitahini imani za waumini, na tunamatumaini kuwa sio adhabu kutoka Kwake. Ni mwaliko kwa watu kutafuta msamaha Kwake, kutenda matendo mema na kutafuta matibabu na kujua hakika kuwa hakuna yeyote anayeponya isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kama vile virusi, ulafi wa warasilimali hautambui mipaka. Dola za kirasilimali zinazoongoza leo zimeuleta ubinadamu kwenye ukingo wa maangamivu mara nyingi, hujali tu kupata faida, bila kujali hali ya watu au maandalizi ya majanga kama haya. Kwa kuongezea, wameujenga uchumi wa ulimwengu mzima kwa deni kubwa, kwa kuufanya kuwa dhaifu kuwa unaweza kuanguka wakati wowote, wakati suluhisho lao pekee ni kutoa deni zaidi, tu kuchelewesha ajali isiyoepukika na kuzidisha ukubwa wake katika mchakato.

Wanadamu wote wanakabiliwa na janga hili na wanahitaji sana utunzaji wa kweli kutoka kwa dola ambayo inasimamia mambo ya watu kikweli. Tunahitaji dola ambayo inathamini ubinadamu na sio vitu vya mada na faida pekee. Ubinadamu unahitaji Khalifah ambaye ataushughulikia ugonjwa kama suala la kimsingi la kibinadamu na sio suala la kiuchumi.

Ulimwengu unahitaji uongozi mpya wa kiulimwengu kutuongoza kutoka kizani kutupeleka kwenya nuru.

Yahya Nisbet

Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu