Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani

H.  15 Jumada I 1441 Na: 1441 / 02
M.  Ijumaa, 10 Januari 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 Kuhusu Mpango wa Serikali wa Chama cha Watu wa Austria na Chama cha Kijani
(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 2 Januari 2020, baada ya mazungumzo ya miezi miwili, mpango wa umoja wa serikali kati ya Chama cha Watu wa Austria na Chama cha Kijani uliwasilishwa, na siku mbili baadaye Mkutano mkuu wa Shirika la Chama cha Kijani ulikubali mpango huo na idadi kubwa ya asilimia 93.18 ya wajumbe. Mpango huu, ambao Uislamu umetajwa mara 16, ni tamko la wazi la vita juu ya maisha ya Kiislamu nchini Austria. Inaendeleza sera ya ukandamizaji wa serikali iliyopita.

Hata utangulizi wake unabeba ulazima wa kujumuishwa, ambao umetegemea nguzo ambayo jamii inaweza kuwepo na kudumu kwa msingi wa kitamaduni moja pekee. Kwa maana nyingine, mtazamo wa maisha wowote na nidhamu yoyote ya kitamaduni zinazokwenda kinyume na mtazamo au nidhamu iliyoko lazima zishughulikiwe: aidha kwa kuuleta karibu au kuuondoa. Utambulisho wa Austria lazima ulindwe kupitia "sera kali ya uhamiaji na ujumuishaji", kama ilivyo kwenye taarifa. Wakati ambapo, "kukubalika kwa nidhamu ya kitamaduni na kisheria ya Austria na Ulaya" pia "kutenganisha dini kutoka kwa serikali" na "usawa wa kijinsia" ni matakwa ya kufanikisha hili.

Maelezo haya yanaelezewa na kufafanuliwa kwa taratibu kadhaa katika maeneo mengi ya kisiasa, kutoka marekebisho ya nidhamu ya mahakama, kupitia utamaduni wa ukumbusho wa enzi ya Nazi, hadi usalama wa ndani. Hata hivyo, hatua kubwa zaidi zilizoelezewa na mpango huo ni katika eneo la ujumuishaji na sera ya elimu. Kama maandishi yanaanza na taarifa kwamba Austria ni "nchi wazi ya Kikristo" ambayo "imejifunga kwa misingi ya ubinadamu na ufahamu." Sharti msingi la uwiano wa jamii na "ushirikiano uliofanikiwa" ni uwepo wa "maadili na kanuni zilizoshirikiwa, ambazo huchukuliwa na kutambuliwa na wote – ikiwemo wahamiaji..." Kisha inasema: "Ukiukaji wowote wa msingi wa nidhamu ya kidemokrasia na nidhamu ya maadili ya kidemokrasia ya serikali yetu huru hauwezi kukubalika au kuzingatiwa kulinganishwa kwa njia yoyote ile, bila kujali chama hicho kilichotoa au hoja inayo ambatana nayo." Ili kuhakikisha hili, elimu ya dini katika shule lazima itayarishwe kwa namna ambayo inahimiza ujumuisho na "kuiongoza kutoka kwa mtazamo wa elimu ya kitaifa." Makala zilizotolewa kufundisha dini ya Kiislamu zilitajwa, na yaliyomo ndani yake yanapaswa kuchunguzwa na Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Idara ya mambo ya Kidini kwa suala la uwepo wa yaliyomo ambayo husababisha mkanganyiko kutoka kwa maoni ya maadili ya kikatiba. Ili “kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa mbali na kulazimishwa kwa namna yoyote iwezekanavyo (kwa mfano, kuvaa Khimar), imeamuliwa kuongezwa kwa marufuku ya kuvaa hijab kwa wanafunzi hadi wafike umri wa miaka kumi na nne, na kukaza udhibiti wa vituo vya utunzi wa watoto (hususan vile vya Kiislamu) kama vile vya chekechea, shule za kibinafsi, nyumba za wanafunzi, na vituo vya elimu". Haya yote hutumikia kufanikiwa kwa malengo ya elimu ya Austria na kukabili udanganyifu na usambazaji wa itikadi zinazopingana na misingi ya kikatiba, kama vile uhamasisho wa kidini wa msimamo mkali wa kisiasa (siasa ya Uislamu)", kama ilivyoainishwa katika makubaliano ya serikali ya muungano.

Hatua hizi zote ni dalili wazi ya kiwango ambacho "Jamhuri ya Waalbania" imeazimia kuchukua ili kufikia udanganyifu wao wa kiimla wa kuunda jamii yenye mtizamo sawa. Sera ya usalama wa kijani ya serikali itakuwa na maelezo yenye ushawishi mkubwa na uingiliaji kati mpana katika uhalisia wa maisha ya Waislamu na nidhamu yao ya kifikra na kihisia. Njia zilizotumiwa katika makubaliano kama msemo wao: (ushiriki wa maadili na kanuni, zinazozingatiwa na kutambuliwa na kila mtu – ikiwemo wahamiaji ...) pasi na shaka yoyote ni kuwa utambulisho pekee ambao una haki ya kuwepo ni utambulisho wa Kiaustria.

Ujumla huu wa nidhamu ya maadili na kuuzingatia kuwa ni uhalisia wa upweke wa Mwenyezi Mungu utazua suala la kuunganishwa kwa kiwango cha suala nyeti, ambalo kwa upande mwingine litazalisha vurugu kutoka katika makundi yote ya jamii. Pia, muktadha ambao mada ya ujumuishaji inazungumziwa inathibitisha muundo huu wa kufikiria. Maregeo ya mara kwa mara kwa vipengee vya kisiasa na kiusalama na kuundwa kwa mandhari ya tishio la uhalifu inaonyesha kuwa Austria inakabiliwa na mzozo wa kweli wa kihadhara, ambapo mshindi mmoja tu anaweza kutokea. Kwa hivyo, hatua hizi zilizoainishwa na mpango wa serikali hazilengi kupata usawa wa maslahi kati ya vikundi tofauti vya kijamii. Badala yake, kwa itikadi yake inatafuta sera ya ujumuishaji na mazoea ya kulazimishwa, ambayo inalenga sana kugawanya na kuyeyusha wengine! Dalili muhimu zaidi ya makubaliano ya kupinga Uislamu katika siasa za Austria ni kwamba Chama cha Kijani, kilichojivunia uwazi wake duniani, pia kimefuata njia ya mgongano wa kiitikadi wa kidini. Chama hicho kimeingia kwenye njia ambayo picha za uadui hutolewa na kufinikwa na nyingine, na kiko tayari hata kuzusha mzozo wa kihadhara katika madarasa ya shule na chekechea. Kwa hivyo, kinachukua sera ya kitaifa ya kukubaliana na serikali ya zamani na kufuata sambamba na wale wanaotakiwa kuwa washirika wake wakuu: Hofer, Strache, and Kickl!

Kwa kuzingatia matukio haya mabaya, Hizb ut Tahrir atika Nchi Zinazozungumza Kijerumani inawalingania Waislamu katika nchi zote hizi kukabili ukweli huu mchungu. Hususan, Vyama, Misikiti, na Wajumbe katika jamii ya Kiislamu, wote lazima hatimaye watambue kuwa njia mbadala ambazo ziliwekwa na nidhamu ya kisiasa iliyoko kusimamia maslahi ya jamii zimefungwa kwa Waislamu. Uchochezi wa kimfumo kwa miongo kadhaa, usambazaji wa maoni ya kupinga Uislamu, na mijadala ya kuchukiza walioisimamia yote imefanywa kwa vikundi vyote vya jamii, ambayo ili sababisha kuibuka kwa ushawishi kuwa Waislamu wamejumuisha kinyume na upinzani wao uliopo wa kibinafsi kama Wamagharibi, na ushawishi huu umeenea katika vyama vyote na vyuo vyote vya jamii hadi ikawa wazo kuu la kuongoza. Kwa hivyo, Waislamu wote lazima wasimame imara dhidi ya harakati za kimfumo za utambulisho wa Kiislamu na maisha. Na Hizb ut Tahrir inawalingania nyinyi, Waislamu, kuchuku msimamo thabiti na uliowazi unaoonekana kwa maoni ya umma mbele ya shambulizi hili kali, na kujihusisha sana katika mjadala huu unaoendelea, na kutangaza wazi kukataa kwenu kanuni ya ujumuishaji ya kulazimishwa. Ni kwa njia hii tu tunaweza kuunda mwamko kati ya jamii jumla kuwa vitendo hivi vya kupinga Uislamu ni dhulma na sio halali, ili tuweze kuukabili upendeleo katika jamii na kuzuia hatari inayokaribia ya mzozo wa kihadhara.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Nchi Zinazo Zungumza Kijerumani

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani
Address & Website
Tel: 0043 699 81 61 86 53
Fax: 0043 1 90 74 0 91
E-Mail: shaker.assem@yahoo.com
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: Kuhusu Kongamano la Usalama la 53 jijini Munich »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu