Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani

H.  1 Sha'aban 1441 Na: 1441 H / 03
M.  Jumatano, 25 Machi 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuhusu Kongamano la Usalama la 53 jijini Munich
(Imetafsiriwa)

Watu muhimu waliochangamka kutoka nyanja za kisiasa, sayansi na asasi za kijamii walikusanyika mnamo tarehe 14 hadi 16 Februari 2020 jijini Munich, Ujerumani, kushiriki katika kongamano la usalama la kila mwaka lililofanyika huko, chini ya anwani "wasiokuwa Wamagharibi" kujadili kwa mara nyengine tena kuzorota mfumo wa kiliberali wa kiulimwengu ulio anzishwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Hii ni pamoja na mgongano wa kifikra katika muundo wa mkakati wa Ujerumani, hotuba zilizotolewa na wawakilishi wa Ujerumani kuanzia na Rais wa Jamhuri hii, Frank-Walter Steinmeier, kupitia kwa Waziri wa mambo ya kigeni Heiko Maas, na kumalizikia na Waziri wa Ulinzi, Annegret Kramp Karrenbauer, zilionyesha kiwango cha hatari ya kutegemea inayoikabili njia ya sera za kigeni na usalama za Ujerumani.

Katika uwezo wake kama wadhifa wa juu, Rais Frank-Walter Steinmeier alichora mipangilio ya sera za kigeni na usalama za Ujerumani. Alilenga kwanza kubadilisha miundo jumla ya siasa za kimataifa, ambazo zilipelekea kutilia shaka katika mambo ambayo kwa muda mrefu yalitambulika kama mapendekezo, ambapo alisema: "Ninahofia kuwa tunashudia leo nguvu ya uharibifu wa siasa za kiulimwengu "....", kwamba wazo la '​​ushindani kati ya mataifa makubwa' sio tu wanatengeza karatasi za mikakati leo, lakini pia wanadhibiti ukweli mpya tunaoishi nao...". Baada ya Urusi na Uchina, "mshirika wa karibu" wa shirikisho la Jamuhuri ya Ujerumani - Amerika – sasa ametupilia mbali wazo la jamii ya kimataifa. Mtazamo finyo wa kitaifa utapelekea, kama alivyosema: "katikati ya hatari mpya za usalama, ushindani wa silaha za kinyuklia, na kuzidi kwa mizozo ya kimaeneo, hadi kushindwa kushughulikia masuala makubwa ya kibinadamu kupitia hatua ya pamoja." Ujerumani bado "imezungukwa na marafiki" kama alivyoiweka lakini Muungano wa Ulaya unakabiliwa na changamoto kubwa: "Ikiwa tutauangalia Muungano wa Ulaya leo, tutagundua upanuzi wa kiuchumi badala ya maridhiano, na tutagundua ongezeko la nyufa za kisiasa na kimfumo... kinyume na zamani, hatuwezi kuanza mwaka 2020 na dhana kuwa Mataifa makubwa yana nia ya mafanikio ya kuungana kwa Ulaya. Badala yake, kila mmoja wa wachezaji wakuu anaangalia maslahi yao, hata kama ilikuwa kwa gharama ya Umoja wa Ulaya, na hili sio jambo zuri kwa maendeleo yetu." Na kama alivyo sema, kuwa maendeleo yote mawili yanapaswa kushughulikiwa... lazima yaendelee kushikamana na wazo la jamii ya kimataifa, na kujitahidi kuunda mfumo wa kisheria wa kimataifa, na kuiimarisha Ulaya kama "muundo usioweza kuepukika kuthibitisha uwepo wa Ujerumani Ulimwenguni."

Katika kiwango thabiti, sera hii ya kigeni na usalama inaweza kufanikishwa tu kwa kuimarisha Muungano wa Atlantiki na sera ya pamoja ya kigeni na usalama ya Muungano wa Ulaya. Steinmeier alisema: "Kwa Ujerumani, uundaji wa Muungano imara wa Ulaya katika uwanja wa sera ya Ulinzi ni jambo la lazima, kama vile kupanua nguzo ya Ulaya katika Muungano huo." Waziri wa Kigeni Haikou Maas na Waziri wa Ulinzi Annegret Kramp Karrenbauer waliregelea kuzungumzia juu ya "mikakati miwili", huku Waziri wa Kigeni Maas akidai kuwa Ujerumani iko tayari kufanya mengi zaidi, ikiwemo juhudi za kijeshi:                                                                     

"Kwa kweli, Nafikiria kuhusiana na suala hili katika kujenga muungano wa usalama na ulinzi wa Ulaya kama nguzo imara ya Ulaya ndani ya NATO, na hili ndilo tunalifanyia bidii kwa pamoja na Ufaransa, na tunakubali ombi la Rais Macron la mazungumzo ya kimkakati juu ya suala hili." Lakini kushiriki huku kijeshi lazima kufuate mantiki fulani ya kisiasa: "Bila diplomasia, bila mkakati wa wazi wa kisiasa, na bila kujenga uwezo wa kijeshi katika maeneo mamoja, tunahatarisha – kwa hali ya juu – kuwa shughuli za kijeshi hazifanyi kazi, na baya zaidi zinaweza kuongeza majanga." Mstari mpana katika suala hili ni taarifa iliyotolewa na Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Ujerumani Peter Strzok, ambaye alisema: "Ulinzi wa usalama wa Ujerumani pia unafanyika katika milima ya Sindh na India." Sasa mstari huu mpana lazima upanuliwe, kwa sababu ulinzi wa usalama wa Ujerumani pia unafanyika "nchini Iraq, Libya na Sahel, pia kwenye meza za mazungumzo jijini New York, Geneva na Brussels", kama alivyo sema. Pia, Ujerumani na Ulaya zinahitaji kuweka uzito mkubwa katika mizani ya siasa za kimataifa", haya yalikuwa maneno ya Waziri wa Ulinzi Annegret Kramp Karrenbauer. Hili sio lazima tu katika muktadha wa mashindano ya mara kwa mara kati ya Amerika na Uchina, lakini pia kwa kuangalia "maeneo ya kusini mwa Ulaya – ambayo ni Afrika na Mashariki ya Karibu na Kati."

Mistari hii mipana ya sera za kigeni na usalama za Ujerumani zinaonyesha athari kubwa. Kwa upande mmoja, serikali ya Ujerumani inataka kufungua miradi kama vile mwito wa Rais wa Ufaransa Macron kufanya mazungumzo ya kimkakati kujenga sera huru za kigeni na usalama za Ulaya. Lakini sera huru ya Ulinzi ya Ulaya huenda ikafeli kwa kutokana na upinzani kutoka nchi za Mashariki mwa Ulaya, uhasama wa kihistoria unaweza pia kuongezeka tena: "Mtazamo wa Kijerumani na Kifaransa wa kujenga uwezo wa ulinzi wa Ulaya kando na Amerika utazua hofu miongoni mwa serikali ya Poland ya uthibiti wa Ujerumani juu ya Ulaya" kama ilivyo elezwa katika uchambuzi wa hivi karibuni katika The Journal of International Politics and Society (Jarida la siasa za kimataifa na jamii). Wakati huo huo, serikali ya Ujerumani inatafuta kuuimarisha muungano wa NATO na Amerika na kuimakinisha sera za kigeni na usalama za Ulaya kama nguzo ya Ulaya katika NATO. Hivyo basi, ugomvi utakaozuka kama matokeo ya hili na Ufaransa unaweza kupelekea kufeli kwa mradi hata kabla kuanza kwake. Pia, mjadala ulioko hivi sasa kuhusu uingiliaji kati wa kipeke yake wa Ulaya katika ghuba ya Arabuni, sera huru ya Amerika kuelekea Iran (sera ya shinikizo kali), inaonyesha mzozo wa kimaslahi, ambao ni thibitisho la tofauti zingine ambazo bila shaka zinatokana na Nidhamu za Muungano zinazogongana.

Zaidi ya hayo, njia zote mbili hufanya maslahi ya Ujerumani kuwa mateka wa mikakati iliyo feli katika Mashariki ya Karibu na Kati vile vile katika Bara la Afrika. Bahari ya Ulaya – yaani, nchi za Kiislamu- zinaona Amerika na Ufaransa kama dola kali ambazo zinataka kuhifadhi na kupanua ushawishi wao na maslahi ya kiuchumi, na kutekeleza mipango yao ya kisiasa katika mzunguko wa kimfumo na kithaqafa. Na ikiwa sera za kigeni na usalama za Ujerumani bado hazijabadilika katika mitego ya uingiliaji kati wa Amerika na Ufaransa, zitashindwa kama vilivyo shindwa vita vya hivi karibuni katika ardhi za kiislamu, iwe ni nchini Afghanistan, Iraq au Mali. Ukiongezea hilo hali ya hatari katika ardhi za Kiislamu, ambayo husababishwa haswa na ulazimishwaji wa nidhamu ngeni ya utawala juu yake baada ya Vita vya Dunia, nidhamu ambayo inakiuka kikamilifu kitambulisho cha Kiislamu na mpangilio wake wa maisha .Wanamikakati katika kumbi za Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Ujerumani wakati wa matukio ya Mapinduzi ya Bara Arabu walitakiwa kutambua kuwa serikali ziliopo katika ulimwengu wa Kiislamu zilishindwa kwa makisio zaidi, na kuwa ustawi wa kisiasa unaweza kupatikana tu katika eneo hili kwa kusimamishwa dola ya kweli ya Kiislamu. Sera kali ya kigeni inayotetea maadili ya Wamagharibi nchini Iraq, Libya na Sahel itapelekea kudumisha mizozo iliopo na uharibifu wa sifa nzuri ya Ujerumani katika eneo hili.

Kwa muktadha huu, Hizb ut Tahrir katika nchi zinazo zungumza Kijerumani inawaonya kwa haraka wafanyaji maamuzi katika kumbi za sera ya kimajimbo ya Kijerumani dhidi ya upanuzi wa vitendo vya kijeshi vya Ujerumani katika ardhi za Kiislamu. Badala ya kujaribu kuwinda maslahi ya kibinafsi ndani ya mzozo kati ya Ufaransa na Amerika na kama mshirika anayeibuka katika kamba za michezo yao ya kisiasa, ni bora kwa Ujerumani kukuza mkakati wake wenyewe na hatimaye kujikomboa kutokana na ushirika wake katika miundo ya Muungano na njia za Kisiasa za nchi zengine. Kwa sababu ya muungano wake wa kihistoria na Khilafah Uthmaniya, Ujerumani ina mizani ya mahusiano ambayo yanaweza kuchukuliwa kuwa faida ya kimkakati kwake, ukilinganisha na Amerika, Ufaransa, Uingereza, Urusi na Uchina. Katika mtazamo wa umoja ambao umeanza kuenea katika siasa za kimataifa, Ujerumani lazima ipange mkakati ambao utaweza kukabili changamoto hii na kuiwezesha kujenga mahusiano mazuri na ya kupanuka na nchi za Kiislamu zilizo jirani yake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Nchi Zinazo Zungumza Kijerumani

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani
Address & Website
Tel: 0043 699 81 61 86 53
Fax: 0043 1 90 74 0 91
E-Mail: shaker.assem@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu