Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  11 Sha'aban 1444 Na: 1444 / 11
M.  Ijumaa, 03 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuvunjwa kwa Khilafah mnamo Machi 3, 1924 M ni Janga Kuu la Karne!
(Imetafsiriwa)

Pindi Khilafah ilipovunjwa na Wakoloni wa Magharibi wakiongozwa na Uingereza na kwa msaada wa wasaliti wa Kiarabu na Kituruki mnamo Machi 3, 1924 M, ngao ya Waislamu ilivunjwa, nchi yao iligawanyika, na wakawa katika hatari ya mashambulizi ya makafiri wa kikoloni kutoka pande zote. Umma wa Kiislamu ukawa yatima baada ya kuvunjwa Khilafah ambayo kwa muda wa karne kumi na tatu ilikuwa imewapa walimwengu mfano bora wa uadilifu, amani, usalama, nguvu, elimu na hekima. Kwa hiyo, Waislamu walipoteza dola yao inayo ongoza duniani, na wakagura kutoka kwenye izza hadi udhalilifu, na kutoka kwenye utajiri hadi kwenye ufukara.

Kuvunjwa kwa Khilafah ni janga kubwa zaidi la karne hii ambalo liliwasibu Waislamu. Kwa sababu Khilafah sio dola ile ambayo inafutika kiurahisi katika historia, ni dola inayowakilisha uongozi wa kisiasa wa Umma wa Kiislamu, yenye kuunganisha pamoja, na Magharibi mkoloni imejitahidi kwa karne nyingi kuivunja. Maumivu, dhulma, umasikini na kukata tamaa ambayo Waislamu wamekumbana nayo katika kipindi cha miaka 99 bila ya Khilafah inathibitisha ukubwa wa janga hili. Katika zama za Khilafah, ni nani angefikiri Mayahudi kuunyakua Msikiti wa Al-Aqsa?! Nani angesubutu kufikiria unyama uliofanywa Algeria, Libya, Kashmir, Chechnya, Bosnia, Afghanistan, Iraq, Arakan (Rakhine), Turkestan Mashariki, na Syria?! Nani angetarajia ufukara huu uliowasibu Waislamu licha ya utajiri wao wa dhahiri na wa kufichika?! Ni katika kipindi gani chengine cha historia Waislamu waliachwa bila mchungaji kwa kiwango hiki?!

Sababu kuu ya kuteseka kwetu leo ni kwamba hatuna Khalifa Mwongofu ambaye angeiunganisha nchi yetu, kuufanya Ummah wetu dhaifu na maskini kuwa na nguvu na utajiri, na kumaliza siku zetu bila ya mchungaji. Rehma na amani iwe juu yake amesema: «إِنَّمَا الإمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Imamu ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwake”.

Kama ambavyo kuwepo kwa Khilafah ni muhimu na ni faradhi kwa Waislamu, kwa Makafiri ni hatari mno. Kwa sababu Khilafah itakuwa na dori yenye ufanisi katika kuwakomboa Waislamu na kuangamiza mipango ya Kafiri Magharibi. Na wakati Khilafah itakuwa ndio tumaini la wanaodhulumiwa, itakuwa ni jinamizi la madhalimu na wahalifu. Hakuna nguvu itakayoweza kuzuia kusimama kwa Dola ya Khilafah Rashida ya pili, hiyo ni ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na mwamko wa wanadamu waliozama kwenye kimbunga cha Urasilimali.

Rehma na amani iwe juu yake amesema:

«تَكُونُ النُّبُوَّةُ فِيكُمْ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلاَفَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً عَاضّاً، فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلاَفَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

Kutakuwa na Utume kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha Atauondoa apendapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume na itakuwepo kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu iwepo, kisha Ataiondoa apendapo kuiondoa, kisha utakuwepo Ufalme wa kurithishana, utakuwepo kwa muda atakayo Mwenyezi Mungu uwepo, kisha Atauondoa apendapo kuuondoa, kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu, utakuwepo kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu uwepo, kisha atauondoa atakapo kuuondoa, na kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume”.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu