Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  1 Shawwal 1444 Na: 1444 / 12
M.  Ijumaa, 21 Aprili 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Pongezi kwa Ummah wa Kiislamu kwa Idd ul-Fitr
(Imetafsiriwa)

Tumefika mwisho wa mwezi mwingine wa Ramadhan, mwezi wa Ramadhan ambao mwanzo wake ni rehema, katikati yake ni msamaha na mwisho wake ni kuepushwa na Moto wa Jahannam. Ndani yake pia kuna Lailatul-Qadr (Usiku wa Cheo) ambao ni bora kuliko miezi elfu moja. Tumeupitisha mwezi wa Ramadhan tukiwa tumefunga na kusimama katika swala kwa imani na kwa kutaraji malipo mema. Na tulisoma Qur’an, kutoa zaka, zakatul-fitr, sadaqa na amali nyinginezo kuwa njia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (swt). Huku macho yetu yakitoa machozi kwa sababu ya maafa yaliyotupata huko Kahramanmaraş na mateso ya Waislamu waliodhulumiwa katika nchi nyingine za Kiislamu. Maumivu, huzuni na machozi yetu yakawa kitu kimoja. Hata hivyo, hivi sasa sote tunaipokea kwa furaha kubwa Idd ambayo Mwenyezi Mungu amewapa waja wake waaminifu. Kwa mnasaba huu, tunatoa pongezi zetu za dhati kwa Waislamu wa Uturuki hasa na nchi za Kiislamu kwa jumla katika sikukuu ya Idd ul-Fitr, na tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) auletee kheri Ummah wa Kiislamu kwa Idd hii. Eid Mubarak.

Na sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Uturuki, katika mwezi huu wa Ramadhan, tumefanya amali ndani ya mfumo wa kampeni ya "Ramadhan Muda wa Naswaha" katika miji yote ya Uturuki. Tulitayarisha meza za futari zilizoenea, kwa neema ya Mwenyezi Mungu, kutoka Istanbul hadi Van, ambapo tuliweka mamia ya meza za futari katika sehemu ya mashariki ya Uturuki, huko Van, Siirt, Tatvan, Diyarbakir, Batman, Sanliurfa, Gaziantep, Adiyaman, Kahramanmaraş, Adana, Mersin, Hatay, Antalya, Konya na Karaman. Kirikkale, Aksaray, Aydın, Izmir, Bursa, Istanbul, Yalova, Kocaeli, Duzce, Sakarya na Ankara. Tulifanya mikutano na wageni katika programu za Futari iliyohudhuriwa na wawakilishi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO), viongozi wa maoni, wanazuoni, wanahabari na wasomi. Ambapo tulibadilishana naswaha kwa mujibu wa kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «الدِّينُ النَّصِيحَةُ» “Dini ni kunaswihiana.”

Vile vile tuliwakumbusha jinsi naswaha/ikhlasi inavyopaswa kuwa kwa Mwenyezi Mungu, Kitabu chake na Mtume wake, na kwamba tunapaswa kujifunza kutokana na maafa makubwa yaliyotupata hivi karibuni na tusiwe chombo cha ajenda chafu za kisiasa za Uturuki. Vile vile tulizingatia ukweli kwamba ajenda ya Waislamu iwe Uislamu, kwamba Uislamu utawale maisha, na kwamba ajenda yetu iwe ni kufanya kazi kwa ajili ya kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida, ambayo itatawala dunia kwa Uislamu, Dini ya rehma na uadilifu. Tulizungumzia kuhusu njia pekee ya kutoka katika hali hii wanayoishi Waislamu ni kuregea Uislamu na kuregesha mfumo wake wa utawala, chini ya Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Enyi Waislamu Waheshimiwa: Kama tulivyofanya katika mwezi wa Ramadhan, pia tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awapunguzie mateso ndugu zetu wote katika maeneo yaliyoathirika na Waislamu wote katika maeneo yanayodhulumiwa katika mwezi wa Ramadhan. Na kwamba Idd ilete furaha na amani kwa Umma wa Kiislamu kama zamani, na tunamuomba (swt), kwamba hii iwe Idd ya mwisho tunayoitoa bila ya Khilafah, na atujaalie neema ya kupokea Idd inayokuja chini ya kivuli cha Dola ya Khilafah Rashida ambayo Mtume (saw) alitubashiria sisi, Ameen.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu” [Ar-Rum: 4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu