Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  23 Rabi' I 1445 Na: 1445 / 03
M.  Jumapili, 08 Oktoba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tunatoa Wito kwa Watawala! Changamkeni, Chukueni Hatua! Ikiwa si Sasa, Lini?

(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumamosi, Oktoba 7, Waislamu nchini Palestina na nchi zote za Kiislamu waliamkia habari za furaha na shauku kubwa kwa sababu mashujaa wa Palestina walizindua operesheni pana, kamili, na muhimu dhidi ya umbile la Kiyahudi takriban saa kumi na mbili unusu asubuhi. Katika operesheni hii, iliyopewa jina Kimbunga cha Al-Aqsa, Mujahidina wa Kipalestina kutoka Gaza waliingia katika maeneo yanayokaliwa kimabavu na kushambulia besi za kijeshi, magereza, vituo vya polisi, na maeneo ya kistratejia ya umbile nyakuzi la Kiyahudi. Waliwakamata Mayahudi waoga, ambao waliamini walikuwa salama chini ya Ngome ya Chuma, mitaani na mabarabarani, wakawadhalilisha, na wakawauwa mamia ya wanyakuzi huku wakiwakamata mamia zaidi.

Umbile la kigaidi la Kiyahudi, ambalo limepanua uvamizi wake, limewapokonya Waislamu ardhi zao, na kuwauwa watoto na wanawake wasio na hatia tangu 1948, wakishajiishwa na serikali oga za Kiarabu na ukimya wa watawala nchini Uturuki na nchi zengine za Kiislamu, wakati huu limejikuta likiwa halina msaada dhidi ya mashambulizi ya Mujahidina na limeanza kukimbia katika kila kona. Hali hii imefichua kwa ulimwengu mzima kiwango cha kweli cha udhaifu na uoga wa umbile la Kiyahudi. Huku serikali za wasaliti katika nchi za Kiislamu zikishindana kuhalalisha mahusiano na umbile nyakuzi la Kiyahudi, kuwakaribisha watawala wake wauaji na kushiriki katika mazungumzo ya kirafiki nao, watu wa Palestina na mujahidina mashujaa wameonyesha ulimwengu kuwa hali ya kweli na ya kimaumbile ni udhalilifu na ugumba unaokabiliwa na Mayahudi wavamizi leo.

Watu wa Palestina wamefanya kile kilichotarajiwa kutoka kwao, na sasa ni zamu yenu, Enyi watawala! Mayahudi waliokimbia kila pande kama paa aliyefazaika mbele ya operesheni hii iliyozinduliwa na Wapalestina mashujaa, watafanya nini mbele ya askari wa Uturuki na jeshi la Uturuki? Hatua mtakazochukua sasa zitakupeni fursa ya kuandika historia. Mtazungumzwa kwa karne nyingi katika vita hivi vitukufu ambavyo vinakaribia kutangazwa. Kama ambavyo ushindi wa Salah al-Din al-Ayyubi, aliyewafukuza Makruseda kutoka Al-Quds, kamwe haukuwahi kusahauliwa, ushindi huu mkubwa pia utakumbukwa kwa karne nyingi. Msiiogope Marekani, ambayo inalisaidia umbile nyakuzi la Kiyahudi! Msitilie maanani vitisho vya Rais aliyechanganyikiwa wa Marekani, Biden! Wala msisahau kwamba kuanguka kwa umbile nyakuzi la Kiyahudi kutawasababishia hofu kubwa zaidi!

Ewe Viongozi Jasiri! Hii ni fursa ya kihistoria kwenu! Mumeona kile Waislamu wanachoweza kufikia bila ya nguvu ya dola na kwa rasilimali kidogo. Wamewashangaza wavamizi na kuwafanya wakimbie bila kuangalia nyuma. Ikiwa mnataka, mnaweza kulifuta umbile hili nyakuzi kwenye ramani. Mnaweza kuandika majina yenu katika historia kwa herufi za dhahabu. Mkiwa mnataka kuchukua fursa hii ya kihistoria na kunyanyua hadhi yenu kwa Mwenyezi Mungu na Waislamu, chukueni hatua sasa, kwani ikiwa sio sasa, basi ni lini?! Hampaswi kamwe kuangalia nyuma! Waislamu wa Uturuki bila shaka watakuungeni mkono katika kila hatua mnayochukua kwenye njia hii.

Enyi Waislamu! Msidanganyike na wale wanaopuuza maumivu na udhalilishaji uliotokana na umbile nyakuzi la Kiyahudi! Uongo kwamba umbile la Kiyahudi lina nguvu sana sasa umefichuliwa, na imefichuliwa kuwa ni puto lililojazwa upepo na ni "dola" dhaifu. Hatua inayofuata ni kuiangusha chini na kuifagia kutoka kwa Ardhi Iliyobarikiwa ya Al-Aqsa. Lile litakalofanikisha hili ni Khilafah Rashida ambayo itasimama hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda. Ni dola ambayo itabomoa kuta na ngome za adui huyu muoga, kumaliza uwepo wake, na kuifuta kutoka kwenye ramani huku majeshi yake yakija yakitoka pande zote. Kwa hivyo, msitafute suluhisho la dola mbili, mpango wa Marekani kwa Palestina uliopendekezwa na Uturuki na nchi zengine kama suluhisho. Msikubali Palestina ndogo yenye mipaka iliyochorwa na Kafiri Marekani! Badala yake, takeni Khilafah kwa sababu suluhisho la pekee la Palestina ni dola moja ya pekee: Khilafah Rashida kwa njia ya Utume!

[وَيَقُولُونَ مَتى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيباً]

“na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Al-Isra:51].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu