Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  7 Jumada II 1445 Na: 1445 / 08
M.  Jumatano, 20 Disemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Istanbul Inakuwa Sauti Moja kwa ajili ya Gaza

"Khilafah ndio Itakayoiokoa Palestina!"
(Imetafsiriwa)

Mauaji ya halaiki yanayofanywa na umbile la Kiyahudi dhidi ya Waislamu mjini Gaza, ambayo yamefikia siku yake ya 73, yanaendelea kwa msaada wa Marekani na nchi za Magharibi za kikafiri, na kimya cha watawala waoga wa nchi za Kiislamu ambao wanashirikiana na wakandamizaji. Kifo kinaendelea kutiririka kwa Waislamu huko Gaza, iliyogeuzwa kuwa rundo la kifusi na umbile la Kiyahudi, kwa kutumia tani 53,000 za mabomu. Nyumba, misikiti, mahospitali, shule, kambi, na kila mahali panakabiliwa na mvua kubwa ya mabomu. Kufikia sasa, idadi ya mashahidi waliouawa imezidi 19,000, huku takriban 8,000 kati yao wakiwa ni watoto wadogo na wachanga. Karibu watu 7,000 wangali hawajulikani waliko, miili yao ikibaki chini ya vifusi vya majengo yaliyoanguka au iko barabarani. Huku ulimwengu, kwa miezi miwili na nusu iliyopita, ukishuhudia picha za Waislamu waliouawa. Hakuna mtu anayesikia kilio cha kina mama, baba, na watoto wanaopiga kelele kwa kukata tamaa, na hakuna mtu anayejibu wito wa "Mko wapi, Enyi Waislamu, enyi watawala, enyi majeshi?".

Sisi, katika Hizb ut Tahrir Wilayah Uturuki, tuliandaa matembezi makubwa kuanzia Msikiti wa Bayezid jijini Istanbul hadi Bustani ya Sarachane ili yawe ni sauti kwa ajili ya Gaza dhidi ya ukatili huu, kuwakumbusha watawala kuhisabiwa kwao na Mwenyezi Mungu, na kuyaita majeshi ya Waislamu kuiokoa Gaza. Maelfu ya Waislamu, wanaume kwa wanawake, wazee kwa vijana, na watoto, walishiriki katika matembezi yetu chini ya kichwa "Moyo Mmoja, Sauti Moja kwa ajili ya Gaza." Wawakilishi kutoka mashirika anuwai yasiyo ya kiserikali (NGOs), pamoja na vyama vya Wapalestina na waandishi wa habari, pia walishiriki katika Matembezi hayo. Baada ya swala ya Adhuhuri, tulianza matembezi kwa kuanza msafara katika Uwanja wa Bayezid, tukipeperusha bendera za umoja zilizoambatana na Takbira, kuelezea mshikamano pamoja na watu wa Gaza na kutangaza kwamba hatutaiacha kadhia ya Palestina peke yake.

Ama kuhusu programu yetu katika Uwanja wa Sarachane, tulitoa wito kwa watawala, haswa, na kwa wanazuoni na Waislamu wote kwa jumla. Tuliwaambia watawala ambao wamesimama bila ya kufanya chochote dhidi ya mauaji yanayofanywa na umbile nyakuzi la Kiyahudi: "Enyi watawala! Kwa nini hamchukui hatua za kuhisika kuiokoa Palestina? Kwa nini mnaogopa? Mnamuogopa nani? Je! Ni Marekani kafiri au Magharibi Mkoloni? Je! Hamjui kuwa Mwenyezi Mungu tunayemuamini ana uwezo wa kila kitu? Yeyote anayemtegemea Mola wake kamwe hatatelekezwa, na yeyote aliye na Mwenyezi Mungu kama mshirika kamwe hatashindwa."

Kuhusu jukumu la wanazuoni na viongozi wa maoni katika kuwahisabu watawala, tulisema: "Mavazi haya matatu hayana vifungo: kadhi, mwanachuoni, na imam ... Kadhi huhukumu kwa uadilifu bila kumpendelea mtu yeyote. Mwanachuoni hutangaza haki bila kumjali mtu yeyote. Ama Imam, yeye ndiye mlinzi wa hifadhi katika wadhifa wa Mtume mtukufu (saw). Machoni mwa watu hawa watatu, haki huyapiku maslahi mengine yoyote. Na Mwenyezi Mungu huwakirimu wale wanaoheshimu njia ya haki."

Na hatimaye, tulipeleka ujumbe ufuatao kwa Waislamu: "Njia pekee ya kukomesha ukatili huu ni kutuma majeshi Al-Aqsa na kukabiliana nguvu kwa nguvu. Huu ndio wito na matakwa ya Waislamu wa Gaza. Jukumu la msingi la watu binafsi na halaiki ni kuwashinikiza watawala kupeleka majeshi hadi Al-Aqsa. Suluhisho la msingi na pekee kwa ukombozi wa Palestina ni kusimamishwa Khilafah Rashida."

Tungependa pia kutoa shukrani zetu kwa wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na Waislamu wote walioshiriki katika matembezi yetu na kuzungumza maneno ya mshikamano. Mwenyezi Mungu awaridhie Waislamu wote waliojitokeza barabarani kusimama na watu wa Palestina na kuwakumbusha watawala juu ya majukumu yao. Tunamuomba Mwenyezi Mungu, Mtukufu, kuipa ushindi Gaza na Palestina yote kupitia Khalifa Rashid (Khalif muongofu) na viongozi wenye ujasiri. Amin.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu