Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  12 Rajab 1445 Na: 1445 / 09
M.  Jumatano, 24 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Muungaji Mkono Ugaidi sio Hizb ut Tahrir, bali ni Uingereza Inayoshiriki katika Mauaji pamoja na umbile la Kiyahudi!
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Alhamisi, Januari 18, 2024, Uingereza iliidhinisha sheria ya kupiga marufuku shughuli za Hizb ut Tahrir. Bunge la House of Lords pia liliidhinisha kwa kauli moja uamuzi wa Bunge la House of Commons. Kwa uamuzi huu, shughuli za Hizb ut Tahrir zilipigwa marufuku nchini Uingereza. Waziri wa Usalama, Tom Tugendhat, alizitaja sababu za marufuku hiyo iliyowekwa na Uingereza juu ya Hizb ut Tahrir kuwa ni chuki dhidi ya Mayahudi, kusifia Kimbunga cha Al-Aqsa na kuwasifu mujahidina kuwa ni mashujaa, kutoa wito wa jihad dhidi ya 'Israel', kupinga ushoga, na kukataa na kuhujumu maadili ya Uingereza na demokrasia.

Ikiwa kwa "upinzani kwa Mayahudi" Uingereza ina maana ya upinzani na uadui kwa umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu, basi sio Hizb ut Tahrir pekee bali Waislamu wote wataona fahari na heshima kutuhumiwa kwa uhalali huo. Ikiwa Uingereza inawapenda Mayahudi sana, inaweza kuwaweka katika maeneo yake au hata kuwapa jimbo nchini Uingereza. Wapinzani wa kweli wa Mayahudi ni nchi za Kikafiri za Magharibi, hasa Uingereza, kwani waliwahamisha Mayahudi kutoka katika ardhi zao hadi Palestina kwa uamuzi wa mgawanyo mnamo mwaka 1947. Wakati Ujerumani ya Nazi iliua Mayahudi milioni 6 kwa utaratibu, haikutoa ulinzi kwa Mayahudi. Hali hii inadhihirisha unafiki na usaliti wa Uingereza na nchi za Magharibi.

Hizb ut Tahrir kusifu Kimbunga cha Al-Aqsa, kuwasifu mujahidina kama mashujaa, na kuyataka majeshi kushiriki katika jihad dhidi ya umbile la Kiyahudi kumechukuliwa kuwa ni "uungaji mkono wa ugaidi" na serikali ya Uingereza. Hata hivyo, Hizb ut Tahrir haifurahishwi tu na upinzani wa Gaza bali pia inaunga mkono upinzani na jihad dhidi ya uvamizi wa Uingereza na uvamizi wa Kiyahudi unaoendelea tangu mwaka 1948. Kwa hiyo, inatoa wito kwa majeshi ya Umma wa Kiislamu kukomesha uvamizi huo, wito ambao unaitia hofu Uingereza, Marekani, na nchi zote za Magharibi. Ni lazima ifahamike kwamba upinzani na jihad dhidi ya uvamizi ili kulinda Dini yao, Ardhi Iliyobarikiwa, na maisha yao sio ugaidi. Ugaidi halisi ni ule ukatili uliofanywa na Mayahudi wanakalia kwa mabavu, ambao waliwaua Waislamu 30,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, waliiangamiza Gaza yote, wakaweka njaa na kiu kwa watu, na uungaji mkono wa Uingereza kwa ukatili huu na ugaidi kwa nguvu zake zote. Kwa sababu hii, sio Hizb ut Tahrir inayounga mkono ugaidi bali nchi za Magharibi zinashiriki katika mauaji ya umbile la Kiyahudi.

Sababu nyingine ya kupiga marufuku Hizb ut Tahrir ni tuhma zake za "kukataa na kuhujumu maadili ya Kiingereza na demokrasia." Demokrasia wala maadili ya Kiingereza hayakubalika kwa Waislamu, kwani sisi tukiwa Waislamu tunapinga demokrasia na maadili ya Kimagharibi kwa msingi wa imani yetu. Tumejitolea tu kwa maadili ya Kiislamu. Kwa hivyo, Uingereza imejitolea vipi kwa maadili yake? Kama kweli Uingereza inaamini katika demokrasia, uhuru na uhuru wa fikra, isingepiga marufuku Hizb ut Tahrir. Iwapo inaamini haki za binadamu, amani na sheria, ingesimama na wanadamu, na sio umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu, na ingepinga mauaji ya halaiki huko Gaza. Kwa sababu hii, wao ndio wasioyaamini maadili ya Kiingereza, na kuyahujumu maadili hayo, na hivyo kuyavunja masanamu waliyoyaunda wenyewe. Hali hii ni kiashiria cha wazi cha kushindwa kwa Magharibi kafiri katika kukabiliana na Uislamu.

Ubepari unaporomoka, na Uislamu unazidi kuibuka. Sio Waislamu tu; watu wote wanatafuta ufumbuzi na tiba katika Uislamu na mfumo wake wa utawala, Khilafah. Sababu kuu ya Uingereza kuiregesha marufuku hii ni itikadi ya Kiislamu iliyotabanniwa na Hizb ut Tahrir na mradi wake wa Khilafah ambao inalenga kuutekeleza. Ni muhimu kutosahau kwamba Hizb ut Tahrir haijawahi kujisalimisha kwa uharamishwaji na haijabaki kufungwa na minyororo. Hata hivyo, kupigwa marufuku kwa Hizb ut Tahrir iliyo halali kisheria na maadui wa Mwenyezi Mungu na Waislamu hakuwezi kuleta manufaa yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu na umma wa Kiislamu. Mashinikizo hayo yanazidisha azma ya Hizb ut Tahrir na yanaonyesha kwamba Khilafah Rashida iko karibu.

[مَتَى نَصْرُ اللّٰهِ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللّٰهِ قَر۪يبٌ] “Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.” [Surat Al-Baqara:214]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu