Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  9 Shawwal 1445 Na: 1445 / 12
M.  Alhamisi, 18 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Yatangaza Kufariki kwa Mmoja wa Dada Mwema Sükîna Aslan

(Imetafsiriwa)

Sükîna Aslan, ambaye alikuwa miongoni mwa kina dada wa kwanza nchini Uturuki ambaye alibeba da’wah na kujitolea maisha yake kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kama mwanamke mwema na muumini, alisalimisha roho yake jana kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema.

[إنّا لله وإنّا إليهِ رَاجعُون]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Surat Al-Baqara:156]

Sükîna alikuwa akipokea matibabu ya ugonjwa mkali kwa miaka 17. Tunashuhudia kwamba alivumilia ugonjwa wake na dhiki zake kwa subira, na alikuwa mwanamke aliyejitolea katika kazi yake ya da’wah na kwa familia yake. Tunaomba kwamba dada yetu mpendwa aweze kufinikwa katika rehma pana ya Mwenyezi Mungu na kwamba familia yake ipate subira. Tunatoa rambirambi zetu kwa jamaa zake, wapendwa, na kina dada katika da’wah. Mwenyezi Mungu aifanye mitihani aliyovumilia iwe kafara kwa dhambi zake na kumlipa kwa pepo.

[إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُمْ بِغَيْرِ حِسَابٍ]

“Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.” [Surat Az-Zumar:10]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu