Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki

H.  4 Rabi' II 1446 Na: 1446 / 01
M.  Jumatatu, 07 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwaka Mzima Umepita, Na Nchi 57 Hazijachukua Hatua Yoyote!
(Imetafsiriwa)

Miaka 76 imepita tangu Mayahudi waliponyakua Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa, na mwaka mzima umepita tangu operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa dhidi ya uvamizi, mauaji na mauaji ya halaiki. Kwa Kimbunga cha Al-Aqsa, ilidhihirika wazi kwamba umbile nyakuzi la Kiyahudi kwa hakika ni simba marara wa karatasi, na kwamba kuwepo kwake kunaendelea kutokana na usaliti wa tawala za vibaraka. Kwa hiyo, taswira yake ambayo tawala hizi ziliichora, kwamba jeshi lake haliwezi kushindwa, iliharibiwa. Kimbunga cha Al-Aqsa mnamo tarehe 7 Oktoba 2023 kilivuruga mipango ya uhalalisha mahusiano wa tawala zote za eneo hilo, haswa Uturuki na Saudi Arabia, ambazo zilikuwa zikiamiliana na umbile nyakuzi la Kiyahudi.

Umbile la Kiyahudi, linaloungwa mkono na kafiri Amerika na nchi zengine za kikoloni za Magharibi, limeua zaidi ya mashahidi 41,000 miongoni mwa ndugu zetu huko Gaza tangu Oktoba 7, 2023. Limetumia tani 100,000 za mabomu katika mauaji 3,650 katika mwaka mmoja. Limechoma na kuharibu hospitali, shule, vyuo vikuu, misikiti, makaazi na hata mahema. Ndugu na dada zetu wamehukumiwa njaa na kiu kutokana na kuzingirwa kwa Gaza. Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Waislamu walijaa viwanjani, waliandamana hadi kwenye afisi za balozi, na kuwataka watawala kuchukua hatua. Wanazuoni wametoa fatwa zinazotaka kukusanywa kwa majeshi ili kuikomboa Gaza na Palestina. Hata hivyo, tawala katika nchi za Kiislamu hazijaitikia wito wao, wala hazikubaliani na fatwa za wanazuoni. Zimeridhika na kulaani na kuzungumza mara kwa mara kuhusu mpango wa suluhisho la dola mbili ambao Amerika imewafundisha kwa moyo.

Sisi, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki, tumefanya mamia ya amali katika mwaka uliopita, ikiwa ni pamoja na kuandaa matembezi, kutoa taarifa kwa vyombo vya habari, kufanya makongamano, paneli za majadiliano, na kufanya mahojiano, ili kuwanusuru ndugu zetu huko Gaza. Vile vile tumetoa wito madhubuti, wa wazi na wa dhati wa kukomesha uvamizi huo kwa kusema, “Majeshi kwenda Al-Aqsa.” Hata hivyo, hakuna hatua zilizochukuliwa kukomesha mauaji ya halaiki huko Gaza. Leo, katika kukumbuka mwaka wa kwanza wa Kimbunga cha Al-Aqsa mnamo tarehe 7 Oktoba mwaka huu, tulifanya matembezi na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari yenye kichwa, “Mwaka Mzima Umepita, Na Nchi 57 Hazijachukua Hatua Yoyote!” katika miji 16 tofauti kote Uturuki; jijini Istanbul, Ankara, Adana, Mersin, Hatay, Şanlıurfa, Siverek, Van, Tetouan, Gaziantep, Konya, Karaman, Aksaray, Duzce, pamoja na Izmir na Aydın.

Tukawahutubia tena watawala katika taarifa yetu kwa vyombo vya habari na tukasema: “Enyi Watawala: Jihadharini na kusahau kwamba umbile nyakuzi la Kiyahudi halifahamu maneno. Halifahamu mazungumzo, usitishaji mapigano, diplomasia, na ususiaji. Linafahamu tu nguvu na vita. Suluhisho pekee kwa hili ni kuyakusanya majeshi na kuwaondoa wanyakuzi kutoka katika ardhi iliyobarikiwa waliyoipora. Basi, kabla ya kuchelewa, tiini amri ya Mola wenu Al-Aziz Al-Qadir.”

Pia tuliwahutubia Waislamu na kuwaambia: “Enyi Waislamu, Gaza imetuonyesha kwamba viongozi 57 sio sawa na Khalifa mmoja. Gaza imetuonyesha kwamba hakuna njia nyengine ya kuinusuru Palestina isipokuwa kupitia Khilafah, kwa sababu Khilafah maana yake ni umoja wa Ummah na kuondolewa kwa mipaka ya bandia baina yao. Khilafah Rashida ndio mfumo pekee wa serikali utakaohakikisha umoja wa Umma wa Kiislamu uliogawanyika na uliosambaratika na itawakusanya Waislamu chini ya paa moja kwa mara nyingine tena. Khilafah Rashida ni mamlaka inayothamini damu, maisha na heshima ya Waislamu. Khilafah Rashida ni uongozi unaojibu kilio cha wanyonge katika bahari kwa kuyakusanya majeshi. Kwa hiyo, kinachopaswa kufanywa ni kumuweka Khalifa Muongofu ambaye atakusanya majeshi ili kuliondosha umbile la Kiyahudi. Wakati umefika sasa wa kufanya kazi kuelekea kusimamisha Khilafah Rashida.”

Mwenyezi Mungu awabariki Waislamu wote walioshiriki katika amali zetu, wanazuoni na watoaji maoni, waliotangaza haki kwa Gaza na Palestina na kuwawajibisha watawala, makundi na umati walioiweka Gaza kwenye ajenda zao, na Umma wote ambao moyo wao unapiga kwa Gaza. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Awaongoze Waislamu waisimamishe Khilafah Rashida kwa njia ya Utume itakayoikomboa Gaza na Palestina yote kutoka kwa Mayahudi, na Atujaalie ushindi Wake mikononi mwa Khalifa Mwongofu na viongozi mashujaa... Ewe Mwenyezi Mungu, Amin.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Uturuki

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-turkiye.org
E-Mail: bilgi@hizb-turkiye.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu