Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  22 Rabi' I 1443 Na: 1443/05
M.  Jumanne, 12 Oktoba 2021

Mashirika ya Kilafi Yaliyoundwa na Urasilimali kama vile Rothschilds Huleta tu Umaskini Pekee kwa Nchi Yetu
(Imetafsiriwa)

Mnamo Septemba 30, Shavkat Mirziyoyev alipokea ujumbe wa Rothschild. Alisema katika mkutano huo kuwa "Fursa za kuongeza ushirikiano wa kunufaishana, ubinafsishaji wa kampuni zinazomilikiwa na serikali, kurekebisha sekta ya benki, kuvutia huduma za hali ya juu za ushauri katika kuimarisha utengenezaji wa divai na vile vile kutekeleza mipango ya ubadilishanaji ya kibinadamu yalisisitizwa. Makubaliano yalifikiwa ya kuunda kikundi kitakachofanya kazi pamoja ili kuchunguza fursa mpya na kuandaa miradi mwanana ya ushirikiano." Mkutano huo pia ulibaini uzoefu mzuri wa maingiliano katika utekelezaji wa shughuli za uuzaji wa hisa ya serikali katika Coca-Cola Uzbekistan kwa mwekezaji wa kigeni ilibainika.

Rothschilds wanakadiriwa kuwa moja ya familia tajiri zaidi ulimwenguni. Familia hii ni ya asili ya Kiyahudi na ni moja ya wawakilishi mashuhuri wa mfumo katili wa kirasilimali. Lazima tutanabahishe wakati biashara kama hiyo ya familia ya Kiyahudi inapowasili nchini kwetu, ambayo haizingatii utukufu wa chochote isipokuwa masilahi yake. Lakini, serikali ya Uzbekistan inawakaribisha kwa mikono miwili na upole. Rais Mirziyoyev mwenyewe alipokea ujumbe ulioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Rothschild & Co, Baron Eric de Rothschild. Hii inaonyesha kwamba serikali ya Uzbek haisiti kuuza nchi yetu, pamoja na watu wake, wanaoishi ndani yake, kwa makombo duni yaliyotupwa na mashirika makubwa ya kirasilimali!

Sisi Waislamu lazima tuchukulie umakini wa ziara kam hizo; kwani tukionyesha kutojali, watanyakua ukoko wa mwisho wa mkate mikononi mwetu! Makubaliano haya na ushirikiano yanatumikia tu masilahi ya kampuni za kirasilimali pekee; kwa sababu hata kama watatoa msaada wa kibinadamu, kuna maslahi fulani nyuma yake, haswa Mayahudi ambao wako mbele ya kila mtu katika suala hili. Kama ambavyo wanawachukia Waislamu nchini Palestina, pia wanatuchukia sisi kwa njia ile ile. Hakuna tofauti katika hilo. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاء بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Surah Al-Maidah 5:51]; na maneno yake (swt) ni uthibitisho dhahiri wa maneno yetu.

Huku serikali ya Uzbek inamkasirikia Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwafanya wao marafiki [Mayahudi na Wakristo], jitahidini, enyi Waislamu, kukataa hili kata kata na kuizuia serikali kutenda vitendo hivyo vilivyo haramishwa. Kama Waislamu, tumeagizwa kuamrisha mema na kukataza maovu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu