Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  22 Dhu al-Hijjah 1442 Na: 1442 / 08
M.  Jumapili, 01 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 Urusi Yajaribu Kudumisha Ushawishi Wake Eneo la Asia ya Kati

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 31/07/2021, tovuti ya KUN.UZ ilichapisha habari: Wanajeshi wa Wilaya ya Kati ya Kijeshi ya Jeshi la Urusi walifika Uzbekistan kushiriki mazoezi ya pamoja katika ya Uzbek na Urusi katika uwanja wa mafunzo wa Termez huko Surkhan Darya. Hili lilitangazwa na Wizara ya Ulinzi ya Uzbek, na mazoezi haya yatafanyika kuanzia Julai 30 hadi Agosti 10 ambapo karibu wanajeshi 1,500 kutoka jeshi la Urusi na Uzbek watashiriki. Mazoezi haya yanafanyika huku hali inazidi kuwa mbaya nchini Afghanistan kutokana na kukola moto kwa takaruki kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Taliban. Ni muhimu kutaja kwamba wanajeshi wa Urusi pia walishiriki kwenye mazoezi karibu na mpaka wa Tajikistan na Afghanistan.

Urusi, ambayo inajiona kama mrithi wa Muungano wa zamani wa Kisovieti, inaziona nchi za Asia ya Kati kama uwanja wake wa nyuma. Kwa hivyo, inapinga kupenya kwa dola zingine za kikoloni, haswa Amerika, katika "uwanja" huu. Urusi yapinga kupelekwa kwa kambi za kijeshi za Amerika eneo la Asia ya Kati, haswa nchini Uzbekistan na Tajikistan, baada ya majeshi ya Amerika kujiondoa kutoka Afghanistan. Hili linaweza kueleweka kutoka kwa maneno ya Mkurugenzi wa Huduma ya Ujasusi wa Kigeni ya Urusi, Sergey Naryshkin, ambaye alisema: "Urusi inatumai kuwa nchi jirani ya Afghanistan zitakataa kupeleka kambi za Amerika katika eneo hilo." Urusi inajua vizuri kwamba Amerika inakusudia kutoka nje kwa mlango wa mbele nchini Afghanistan na kurudi tena kupitia mlango wa nyuma kupitia msaada wa vibaraka wake nchini Uturuki na Pakistan. Kwa mfano, mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Uturuki na Uzbekistan ambayo yalifanywa katika uwanja huo wa mafunzo kuanzia Machi 23 - 27 ya 2021 ni moja ya hatua kuelekea katika lengo hili. Moscow inakataa kuviweka vikosi vya Uturuki nchini Afghanistan baada ya kuondolewa kwa vikosi vya Amerika na NATO nchini humo.

Asia ya Kati pia ni muhimu kwa Amerika; ndio sababu Amerika haitaki kuliachia eneo hili Urusi peke yake. Hivi ndivyo Amerika ilivyo tangaza - kwa mfano - hata wakati wa kipindi cha Raisi wa zamani wa Amerika Clinton. Hili lilithibitishwa na Strobe Talbott, aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Kigeni, akisema: "Eneo hili lina akiba ya mafuta ya mapipa bilioni 233, na linakadiriwa kwa mtazamo wa maslahi ya Amerika kuwa eneo muhimu mno. Hii ndio maana akiba ya kawi ya karne ya ishirini na moja haiwezi kuachwa chini ya udhibiti wa Urusi! " Bila shaka, Urusi haiwezi kushindana na Amerika kisiasa au kiuchumi, kwa sababu sio Muungano wa Kisovyeti, ambao ulikuwa na mfumo wake na uwezo wake mkubwa wa kiuchumi na kijeshi, lakini pamoja na hayo, Urusi inajaribu kutopoteza kabisa windo hilo.

Jambo jengine ambalo linaiogopesha Urusi zaidi ya kupenya kwa ushawishi wa Amerika ni kuongezeka kwa mwamko wa Kiislamu katika eneo hili. Urusi inajua vizuri kuwa Hizb ut Tahrir pia inafanya kazi nchini Afghanistan, ambayo inaweza kuwaelekeza Taliban katika mwelekeo sahihi na dola ya Khilafah itasimamishwa nchini Afghanistan! Kwa hivyo, operesheni za kijeshi za Urusi katika Asia ya Kati zinapaswa kutazamwa kwa mwangaza huu pia.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [TMQ: 8:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu