Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  9 Jumada II 1444 Na: 1444 / 06
M.  Jumatatu, 02 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watoto 19 walikuwa Wahasiriwa Waliofuata wa Utawala wa Kinyama

(Imetafsiriwa)

Katika ajenda siku hizi ni kashfa kuhusu dawa ya kikohozi ya Doc-1 Max inayotengezwa nchini India ambayo imepoteza maisha ya watoto 19 nchini mwetu hadi sasa. Vyombo vikuu vya habari vya kigeni pia vinaangazia suala hilo. Hakika, haishangazi kwamba huduma za afya na maduka ya dawa yamegeuka kuwa biashara yenye faida sana. Na sasa watoto wanalipia hili! Na ikiwa serikali iliwafuta kazi maafisa wengi katika uwanja huu kama wahusika, tunaamini kwamba sababu kuu ya hilo sio tu mfumo wa afya ulioharibiwa, lakini pia mfumo wa kibepari ulioleta sekta hii katika hali hii; kwa sababu mfumo huu unaotekelezwa kwetu leo ndio uliogeuza uwanja wa matibabu kuwa biashara ya kuhujumu afya za watu. Uwanja huu umekuwa ukijihusisha na ufisadi, rushwa, kuruhusu ushirikiano kati ya madaktari na wanafamasia, ukosefu wa udhibiti wa dawa zinazoingia nchini, pamoja na hali ya kutokuwa na nia ya kujali afya za watu wake, ambayo ni moja ya kazi zake kuu. Sababu kuu ya haya yote ni mfumo huu. Kwa sababu kama matokeo ya utabikishaji wa mfumo kama huo maadili mengine yote yametengwa, na kupata thamani ya kimada pekee imekuwa ndio lengo kuu. Na sekta ya matibabu haileta faida kwa serikali, kinyume chake, inahitaji gharama kubwa. Kwa hivyo, katika nchi za kidemokrasia, sekta hii inapewa watu binafsi, na serikali inakwepa majukumu yake. Matokeo yake, afya ya watu inakuwa tegemezi kwa "huruma" ya makampuni machache makubwa ya dawa na kliniki za kibinafsi.

Vifo vya watoto na kulipia matatizo ya matibabu kwa maisha yao yasiyo na hatia kiliwashtua na kuwaudhi watu wa nchi hii. Waandishi wa habari, wataalamu na wanaharakati kote nchini wanasema hili linazidi kutovumilika na kwamba mageuzi makubwa lazima yafanywe. Haiwezekani tena kubeba sio hali hii tu bali pia ukweli kwamba hospitali 3 kubwa za saratani katika nchi yetu zimeuzwa hivi karibuni, na ukweli kwamba huku watu wakiugua magonjwa mazito zaidi wanageukia umma kwa msaada kwa sababu hawana pesa za matibabu kutokana na uzembe wa serikali katika majukumu yake. Lakini ni lazima kwa wasomi kutambua kwamba mabadiliko ya kweli yatatokea sio tu katika eneo moja bali kupitia mabadiliko ya mfumo unaotabikishwa. Lazima waelewe kwamba mfumo wa kibepari na demokrasia yake inayonuka uvundo huwaletea watu masaibu hayo. Wazingatie kuwa mfumo wa kibepari ndio chanzo cha balaa na matatizo yote, na wazingatie kutekeleza mfumo mbadala. Na lazima watambue kwamba mfumo huo upo nao ni mfumo wa Uislamu ambao watu wetu wanauamini, kwa sababu ni dola inayoongozwa kwa sheria ya Kiislamu pekee ndiyo inayoweza kudhamini hifadhi na ulinzi wa afya ya binadamu. Ama mifumo ya leo ya kinyama, inageuza tu afya ya binadamu kuwa chanzo cha mapato. Hivyo basi, kuregea katika mfumo wa Kiislamu ni suala nyeti na hatima kwa Waislamu katika nchi yetu.

(أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْماً لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ)

“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Ma’ida: 50]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu