Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  27 Jumada II 1444 Na: 1444 / 07
M.  Ijumaa, 20 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mtu Mwengine katika Mashababu wa Hizb ut Tahrir Ajiunga na Msafara wa Mashahidi!
(Imetafsiriwa)

(مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً)

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Surah Al-Ahzab 33:23]

Kuvuja damu kwa Umma wa Kiislamu hususan Waislamu wa Uzbekistan kunaendelea, kwa habari ya kuuawa shahidi kijana mwengine shupavu wa Ummah, Ndugu Mamajanov Israeljan Abdul Mukhtarovich, ambaye alijiunga na misafara ya mashahidi mnamo Januari 18, 2023. Ndugu Israeljan, alizaliwa Mei 26, 1970 katika mji wa Karasov, Mkoa wa Andijan, aliuawa shahidi katika Gereza la Utawala Maalum nambari 17 katika wilaya ya Karaul Bazar ya Mkoa wa Bukhara. Mnamo 1997, utawala wa dhalimu wa Kiyahudi Karimov ulimfunga Ndugu Israeljan kwa tuhuma za kuwa mfuasi wa Hizb ut Tahrir. "Dhambi" lake pekee ilikuwa ni kufanya kazi ya kuregesha maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida na kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu (swt)! Walimtesa sana katika magereza ya Jaslik, Andijan, Bukhara na magereza mengine. Hata hivyo, utawala dhalimu haukuweza kuvunja ari yake. Alisimama kidete kwenye njia ya haki kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hii ilitokana na Imani yake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kujiamini kwake katika fikra na madhumuni aliyobeba. Kwa hivyo, aliweza kujidumisha kama mfano bora wa subira, uthabiti na azma. Tunatumai kwamba Ndugu yetu Israeljan amezifanyia biashara nafsi na mali yake kwa Mwenyezi Mungu (swt), ili Mwenyezi Mungu (swt) amemchukue kama shahidi na kumwagilia kwa damu yake mti wa Uislamu. Hatumsifu yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu (swt).

Ikumbukwe pia hapa kwamba serikali ya sasa ya Mirziyoyev inakemea juu ya kutorudia ukatili uliofanywa na utawala uliopita, na pia kuhusu haki za binadamu na kujali watu. Hata hivyo, bado inawaweka gerezani Mashababu thabiti wa Hizb ut Tahrir, kama vile Israeljan ambao ni watoto jasiri wa watu hawa!! Leo, watu wa Uzbekistan, hasa wazee, wanawake, watoto na wagonjwa wanaokaa kwenye baridi kali ya msimu wa baridi, bila gesi au umeme, kwa mara nyengine tena wanashuhudia uwongo wa madai ya serikali hii na kiwango cha "kujali" kwake watu. Maafisa wa serikali hii wanasubiri hesabu ngumu sana, katika Khilafah Rashida itakayosimamishwa hivi karibuni, inshaaAllah. Ama hisabu ya Mwenyezi Mungu (swt) Siku ya Kiyama itakuwa kali zaidi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amkubali Ndugu yetu Israeljan miongoni mwa mashahidi, na amjaalie furaha ya kuwa karibu na Mitume (as), wakweli, mashahidi na watu wema katika kiti cha haki pamoja na Mmiliki wa Nguvu zote.

Tunatoa rambirambi kwa mke mvumilivu wa Ndugu Israeljan, ambaye alitembea kutoka jela moja hadi jengine kwa muda wa miaka 25, na kwa watoto wake na jamaa wengine, tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awajaalie subira, uthabiti, na faraja, na awakusanye pamoja naye Akhera katika Pepo pana mithili ya mbingu na ardhi, ambapo hakuna dhiki, usumbufu, au kutengana. Tumehuzunishwa kwa kuondoka kwako, ewe Israeljan, na hatusemi ila yale tu yanayomridhisha Mola wetu Mlezi, Mwenye nguvu na Mtukufu, (إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ) “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Surah Al-Baqarah 2:156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu